Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu, Coplo Hafidh Abdallah Mohamed atoa ushahidi wake, kesi kuendelea Jumatatu 01 November 2021

Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu, Coplo Hafidh Abdallah Mohamed atoa ushahidi wake, kesi kuendelea Jumatatu 01 November 2021

Shahidi wa Tatu Koplo Hafidh Mohamed akihojiwa na Wakili wa utetezi John Mallya Mahakamani leo;

MALLYA: Kwenye ripoti yako umesema hapa kuna errors. Je kuna errors ngapi?

KOPLO HAFIDH: Hiyo hiyo moja.

MALLYA: moja inakua error au errors?

KOPLO HAFIDH: Inategemea.

MALLYA: Maana ya terrorist ni nini?

KOPLO HAFIDH: Ni ugaidi.

MALLYA: Na Terrorism maana yake nini?

KOPLO HAFIDH: Ni masuala ya utalii.

(Mahakama inaangua kicheko)

MALLYA: Narudia tena. Terrorist umesema ni Ugaidi sio?

KOPLO HAFIDH: Ndio.

MALLYA: Na terrorism maana yake nini?

KOPLO HAFIDH: Ni masuala ya utalii.

Mahakama inaangua kicheko, hadi Jaji anashindwa kujizuia.! 🤣🤣
 
Shahidi wa Tatu Koplo Hafidh Mohamed akihojiwa na Wakili wa utetezi John Mallya Mahakamani leo;

MALLYA: Kwenye ripoti yako umesema hapa kuna errors...
Yaani Waafrika ni shida tupu. Yaani Mwaafrika akishindwa kuelezea maana ya kiingereza inakuwa ni kicheko na inaanzishiwa thread hapa JF!! Ujinga mtupu!
 
Kwani wewe nani kakwambia Mbowe Gaidi yule ni Mtalii 100%,ndio maana leo yuko Keko kesho Hai keshokutwa Arusha.Huo ni utalii.
 
Shahidi wa Tatu Koplo Hafidh Mohamed akihojiwa na Wakili wa utetezi John Mallya Mahakamani leo;

MALLYA: Kwenye ripoti yako umesema hapa kuna errors. Je kuna errors ngapi?...
Huyo ni mtalii tena wa ndani Kwa Sasa anatalii kwenye Moja ya gereza na mahakamo Moja . 🏃
 
Kama umemsikia shahidi wa leo hii, "terrorism" ni utalii, na "terrorist" ndio ugaidi.
Na hakuishia hapo tu kujichanganya, hata kuhusu eneo analojipambanua yeye kuwa ni mtaalam wake!

Haya tunayoyashuhudia mahakamani na hawa mashahidi ndiyo sura sahihi ya nchi yetu ilivyo sasa hivi.

Tumevurugika sana kama nchi.
Kuna mtu humu JF ananeno lake anasema huu ni weledi wa kitanzania. Lengo la kumleta huyu shahidi wa leo ni lipi haswa? kama yeye si wa fingerprint wamlete huyo wa fingerprint, sio hizi story za leo.
 
Yaani Waafrika ni shida tupu. Yaani Mwaafrika akishindwa kuelezea maana ya kiingereza inakuwa ni kicheko na inaanzishiwa thread hapa JF!! Ujinga mtupu!
Lazima tucheke, maana kama hujui unatakiwa useme "sijui".

Sasa ukijifanya unajua wakati huji lazima tucheke tu, maana hamna namna tena...
 
Back
Top Bottom