Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu, Coplo Hafidh Abdallah Mohamed atoa ushahidi wake, kesi kuendelea Jumatatu 01 November 2021

Shahidi wa Tatu Koplo Hafidh Mohamed akihojiwa na Wakili wa utetezi John Mallya Mahakamani leo;

MALLYA: Kwenye ripoti yako umesema hapa kuna errors. Je kuna errors ngapi?

KOPLO HAFIDH: Hiyo hiyo moja.

MALLYA: moja inakua error au errors?

KOPLO HAFIDH: Inategemea.

MALLYA: Maana ya terrorist ni nini?

KOPLO HAFIDH: Ni ugaidi.

MALLYA: Na Terrorism maana yake nini?

KOPLO HAFIDH: Ni masuala ya utalii.

(Mahakama inaangua kicheko)

MALLYA: Narudia tena. Terrorist umesema ni Ugaidi sio?

KOPLO HAFIDH: Ndio.

MALLYA: Na terrorism maana yake nini?

KOPLO HAFIDH: Ni masuala ya utalii.

Mahakama inaangua kicheko, hadi Jaji anashindwa kujizuia.! 🤣🤣
 
Shahidi wa Tatu Koplo Hafidh Mohamed akihojiwa na Wakili wa utetezi John Mallya Mahakamani leo;

MALLYA: Kwenye ripoti yako umesema hapa kuna errors...
Yaani Waafrika ni shida tupu. Yaani Mwaafrika akishindwa kuelezea maana ya kiingereza inakuwa ni kicheko na inaanzishiwa thread hapa JF!! Ujinga mtupu!
 
Kwani wewe nani kakwambia Mbowe Gaidi yule ni Mtalii 100%,ndio maana leo yuko Keko kesho Hai keshokutwa Arusha.Huo ni utalii.
 
Yaani Waafrika ni shida tupu. Yaani Mwaafrika akishindwa kuelezea maana ya kiingereza inakuwa ni kicheko na inaanzishiwa thread hapa JF!! Ujinga mtupu!
Ungepita kulia ukaenda zako bila ya kucoment lolote.
Kinachokuma ni nini?

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kwamba Katika Ushahidi wako wote hujataja Jina la Silaha aliyekamatwa nazo, Kwanini hukutaja

Shahidi: Kwanza sijui Adamoo...
Waliifanyia riheso wakati wakitengeneza muvi....

Akakariri...
 
Shahidi wa Tatu Koplo Hafidh Mohamed akihojiwa na Wakili wa utetezi John Mallya Mahakamani leo;

MALLYA: Kwenye ripoti yako umesema hapa kuna errors. Je kuna errors ngapi?...
Huyo ni mtalii tena wa ndani Kwa Sasa anatalii kwenye Moja ya gereza na mahakamo Moja . 🏃
 
Kuna mtu humu JF ananeno lake anasema huu ni weledi wa kitanzania. Lengo la kumleta huyu shahidi wa leo ni lipi haswa? kama yeye si wa fingerprint wamlete huyo wa fingerprint, sio hizi story za leo.
 
Yaani Waafrika ni shida tupu. Yaani Mwaafrika akishindwa kuelezea maana ya kiingereza inakuwa ni kicheko na inaanzishiwa thread hapa JF!! Ujinga mtupu!
Lazima tucheke, maana kama hujui unatakiwa useme "sijui".

Sasa ukijifanya unajua wakati huji lazima tucheke tu, maana hamna namna tena...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…