Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu, Coplo Hafidh Abdallah Mohamed atoa ushahidi wake, kesi kuendelea Jumatatu 01 November 2021

Ndio maana Watanzania wote tunataka Sheria zetu zote zitafsiriwe kwa lugha yetu ya Kiswahili, Pia Mwenendo wa kesi pamoja na Hukumu ziwe zinaandikwa kwa Lugha ya Kiswahili.
karibu 99%ya watanzania wote tunazungumza na kuandika lugha ya kiswahili lkn cha kushungaza Mahakama zetu bado zimekumbatia mfumo wa kikoloni wa matumizi ya kizungu!!
kwani kulikuwa na haja gani kumuuliza swali kwa kizungu?
angemuuliza kwa Lugha yetu ya Taifa hata mkulima wa kijijini angemjibu.
 
Sasa polisi anaulizwa unajua kesi ya ugaidi ni kubwa au ndogo?

Anajibu... sijui

Polisi hajui kama kesi ya ugaidi ni kubwa?????

Hawa ndio wale wa division 4 ya 32?
Maswali mengine siyo relevant na ushahidi anaotoa ndiyo maana anajibu hajui to cut short.
 
Yaani Waafrika ni shida tupu. Yaani Mwaafrika akishindwa kuelezea maana ya kiingereza inakuwa ni kicheko na inaanzishiwa thread hapa JF!! Ujinga mtupu!
Ujinga tu. Sidhani eti kushindwa kutofautisha terrorist na terrorism ni issue yenye mashiko
 
NAOMBA WALE WATAALAMU WA KUHIFADHI MAMBO VITABUNI WASISAHAU KUANDIKA RIWAYA HII AU TAMTHILIYA HII AU HABARI HII YA MBOWE KWENYE VITABU ILI WATOTO WETU WAJE WAONE TULIWAHI KUONGOZWA NA AINA GANI YA VIONGOZI WAWE WA CCM, VYOMBO VYA DOLA NA SERIKALI YA AINA GANI ILIKUWEPO KUANZIA MWAKA 2015 NA KUENDELEA, NA RAIS ALIYEPOKEA KIJITI TOKA KWA DIKTETA JIWE NA YEYE KUENDELEZA UTAMADUNI HUO NA KUUTHIBITISHA PASIPO SHAKA ALIPOHOJIWA NA SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA UINGEREZA YAANI BBC. NI MUHIMU SANA! WENZETU KULE UGANDA WANA HABARI ZOTE KUHUSU IDD AMIN DADA.
 
Kuna mtu humu JF ananeno lake anasema huu ni weledi wa kitanzania. Lengo la kumleta huyu shahidi wa leo ni lipi haswa? kama yeye si wa fingerprint wamlete huyo wa fingerprint, sio hizi story za leo.
Huyu aliyeletwa leo, eti ni mtaalam wa mambo hayo, kayasomea hadi nchi za nje! Botswana!
Nawajuwa vyema watu wa Botswana katika eneo hili. Bila shaka walipopelekewa mtu kama yule kumfunza alichotakiwa kujifunza, walishangaa kidogo kama nchi nzima hatuna watu wenye sifa za kufunzwa kazi hiyo!

Huko maofisini serikalini siku hizi watu wa aina hii ndio wamajazana huko. Jambo muhimu ni nani anakujuwa, na siyo uwezo ulionao.
 
Yaani Waafrika ni shida tupu. Yaani Mwaafrika akishindwa kuelezea maana ya kiingereza inakuwa ni kicheko na inaanzishiwa thread hapa JF!! Ujinga mtupu!
Ni hivi maneno hayo ya kiingereza ameyatumia Kwenye ripoti yake iliyowasilishwa hapo mahakamani Kama ushahidi.
Sasa anaulizwa aeleze maana yake kiswahili ndio kajichanganya
Hivyo basi kwa Maelezo take akina mbowe walikuwa wanamiliki silaha ili iwawezeshe kufanyia utalii.
Hoi ndio maana ya ripoti yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…