Maswali ya mahakamani bwana, be like
Wakili: Ulikula nini?
Shahidi: Nilikula ugali na dagaa.
Wakili: Unaweza kuelezea mahakama ulivyokula?
Shahidi: ndio, nilimega tonge.
Wakili: enhee ulimega kubwa dogo?
Shahidi: kubwa.
Wakili: enhee kilichofuata
Shahidi: nikaweka mdomoni.
Wakili: ndio, nini kikafuatia?
Shahidi: nikaanza kutafuna.
Wakili: baada ya kutafuna?
Shahidi: nikameza.
Wakili: lakini hukuelezea kama ulinawa.
Shahidi: ni kweli sikuelezea, lakini nilinawa.
Wakili: hukuelezea pia kama ulitoezea kwenye mboga.
Shahidi: ni kweli nilitoezea lakini nilisahau kusema.
Wakili: dagaa walikuwa wa mchuzi au wakavu?
Shahidi: wakavu, waliokaangwa.
Wakili: sasa mbona unatuchanganya? Unawezaje kutooezea tonge tena kubwa kwenye dagaa waliokaangwa?
Shahidi: sifahamu.
Jaji: usiseme hufahamu, sasa hufahamu una maanisha nini?
Shahidi: sikumbuki kama walikuwa wa mchuzi au wakavu.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Mahakamani kama unatoa ushahidi wa uongo, lazima wakutafute uingie kwenye 18 tu, la sivyo uwe very smart na mwenye kumbu kumbu sana, halafu kila unalojibu watarejea jibu lako baadae..
Lakini hata kumuangamiza mwenzio kisa uongo, malipo ni humu humu duniani tu.
Ndugu zangu tujifunze kwa hiki kinachoendelea, tusiwe waongo..
Lakini shahidi mkweli ni ngumu mno akatoa ushahidi wenye kuitia mahakama shaka, mkweli huiondoa mahakama shaka..
Ndugu zangu uongo ni mbaya sana, unaweza kukufunga na kukuteketeza kabisa, vitabu vyetu vya dini vinapinga na kulaani watu waongo..
Methali 19:9- Shahidi mwongo hatakosa kuadhibiwa;asemaye uongo ataangamia