Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na rushwa. Shauri kuendelea kesho Nov, 2, 2021

Shahidi wa Leo katoa Maboko matatu makubwa kweri kweriii yaani. Boko la Kwanza ni ile namna ya kuwakamata Watuhumiwa ni ya vichekesho mno. Yaani Askari wakawaeleza Watuhumiwa nyosha mikono juu mpo chini ya ulinzi ninyi magaidii.Kumbe ni Askari ndio walio tamka Kwanza Watuhumiwa ni magaidi kabla ya tuhuma hizo kuthibitishwa na chombo chochote Cha kutoa haki na ndio wao wenyewe wanaleta kesi Mahakamani ili Mahakama iwafunge. Wakati walikuwa wanajua watumiwa ni magaidi kabla ya kuwakamata lakini wakakaa nao gerezani miezi zaidi ya nane bila kuwashitaki.

Boko la pili ni kuwa Shahidi anasema alikuwa umbali wa mita kumi akishudia tukio la ukamataji lakini wakili wa utetezi akapiga hatua Saba tuu mahakamani na kumwambia aoneshe kitu kilicho ktk hatua hizo, shahidi ameshindwa kuona kitu kilichopo hatua Saba tuu Mahakamani na Kisha kuieleza Mahakama kuwa hawezi kuona umbali wa mita Saba kwakuwa anamatatizo ya macho lakini eti aliweza kuona tukio la umbali wa hatua kumi. Sasa Ushahidi wa mtu mwenye matatzo ya kuona ndio Ushahidi Mahakama inapaswa kuuchukua kuwa huyu Shahidi aliona tukio? Alipo ulizwa na wakili wa utetezi, je aliieleza Mahakama Kama siku hiyo ya tukio alivaa miwani Kama huwa anatumia?Akajibu kuwa hakueleza.

Boko la tatu na Kali kweli kweriii Shahidi anasema Askari Jumanne ndio alijitambulisha kwake kuwa ni kiongozi wa ukamataji. Wakati bwana Kingai wakati akitoa Ushahidi wake aliieleza Mahakama kuwa yeye ndiye alikuwa kiongozi wa ukamataji. Akaulizwa na wakili wa utetezi je akitokea mtu mwingine akasema yeye ndio kiongozi wa ukamataji atakuwa muongo? Shahidi Akajibu ndiooooo Kama mazuzu ya kule bungeni.
Akaulizwa unamjua Kingai? Shahidi Akajibu simjuiiiii.
Sisi Watanzania msitufanye hamnazo bwana Kingai na Mahita.
CC :Hangaya
 
Akina Mtalo ni watu wa Uru .....!!
Siwezi kukubali kirahisi. Wa Uru nawafahamu akina Mushi, Maro, Kiwia, Otaru, Komu, Temba, Kilewo, Kiwale, Ngowi, Kisima, Mauki, Kimati hawa tuko nao mjini huku miaka mingi, hao Mtalo sijawahi kuwasikia kabisa popote! Inamaana hao ndio wameganda huko migombani hadi kuja kuibuliwa na kesi hii?
 
Kuna mdau kasema ANITA VALERIAN MTALO yuko Rau Madukani anauza mbege hata saa hii, na haelewi huyo anayetoa ushahidi Dar ni nani
Ingawa hajajibu vizuri .... bado inatia shaka kama kweli huyo mama ni muuza mbege ........!!
 
Siwezi kukubali kirahisi. Wa Uru nawafahamu akina Mushi, Maro, Kiwia, Otaru, Komu, Temba, Kilewo, Kiwale, Ngowi, Kisima, Mauki, Kimati hawa tuko nao mjini huku miaka mingi, hao Mtalo sijawahi kuwasikia kabisa popote! Inamaana hao ndio wameganda huko migombani hadi kuja kuibuliwa na kesi hii?
Hayo sijui. Ila binafsi namfahamu Mtalo anayetokea Uru .....!!
 
Maswali wanayoulizwa hayana impact katika kupunguza ushahidi.
 
Shahidi wa Leo katoa Maboko matatu makubwa kweri kweriii yaani. Boko la Kwanza ni ile namna ya kuwakamata Watuhumiwa ni ya vichekesho mno. Yaani Askari wakawaeleza Watuhumiwa nyosha mikono juu mpo chini ya ulinzi ninyi magaidii.Kumbe ni Askari ndio walio tamka Kwanza Watuhumiwa ni magaidi kabla ya tuhuma hizo kuthibitishwa na chombo chochote Cha kutoa haki na ndio wao wenyewe wanaleta kesi Mahakamani ili Mahakama iwafunge. Wakati walikuwa wanajua watumiwa ni magaidi kabla ya kuwakamata lakini wakakaa nao gerezani miezi zaidi ya nane bila kuwashitaki.

Boko la pili ni kuwa Shahidi anasema alikuwa umbali wa mita kumi akishudia tukio la ukamataji lakini wakili wa utetezi akapiga hatua Saba tuu mahakamani na kumwambia aoneshe kitu kilicho ktk hatua hizo, shahidi ameshindwa kuona kitu kilichopo hatua Saba tuu Mahakamani na Kisha kuieleza Mahakama kuwa hawezi kuona umbali wa mita Saba kwakuwa anamatatizo ya macho lakini eti aliweza kuona tukio la umbali wa hatua kumi. Sasa Ushahidi wa mtu mwenye matatzo ya kuona ndio Ushahidi Mahakama inapaswa kuuchukua kuwa huyu Shahidi aliona tukio? Alipo ulizwa na wakili wa utetezi, je aliieleza Mahakama Kama siku hiyo ya tukio alivaa miwani Kama huwa anatumia?Akajibu kuwa hakueleza.

Boko la tatu na Kali kweli kweriii Shahidi anasema Askari Jumanne ndio alijitambulisha kwake kuwa ni kiongozi wa ukamataji. Wakati bwana Kingai wakati akitoa Ushahidi wake aliieleza Mahakama kuwa yeye ndiye alikuwa kiongozi wa ukamataji. Akaulizwa na wakili wa utetezi je akitokea mtu mwingine akasema yeye ndio kiongozi wa ukamataji atakuwa muongo? Shahidi Akajibu ndiooooo.
Akaulizwa unamjua Kingai? Shahidi Akajibu simjui.
Sisi Watanzania msitufanye hamnazo bwana Kingai na Mahita.
CC :Hangaya
Hayo yote hayazidi boko la nne;
SHAHIDI kuandikwa maelezo saa 7 wakati ukamataji umefanyika saa nane kasoro. Yaani maelezo yaliandikwa kabla ya tukio, mkiambiwa tukio limepikwa kihuni muwe mnaelewa.
 
Ingawa hajajibu vizuri .... bado inatia shaka kama kweli huyo mama ni muuza mbege ........!!
Jina lenyewe la kuchonga. Mimi katika kutembea kwangu nchi hii na hata Moshi nishafanya kazi inayohusiana na kukutana na watu wengi kuwaandikisha majina. Sikuwahi kuona jina hilo Mtalo. Au sijui Mtali wala Mtaro! Nimesikia akina Kitali, Otaru lakini siyo Mtalo.
Na mwenyewe umesikia ameulizwa mara mbilimbili kurekebisha spellings, jina alilotamka limepishana na lililopo kwenye orodha ya mashahidi.
 
Back
Top Bottom