Yaliyojiri Kesi ya Mbowe: RPC Kingai aeleza Mbowe alivyopanga kumdhuru Ole Sabaya. Kesi yaahirishwa hadi 27 Oktoba 2021

Yaliyojiri Kesi ya Mbowe: RPC Kingai aeleza Mbowe alivyopanga kumdhuru Ole Sabaya. Kesi yaahirishwa hadi 27 Oktoba 2021

Aibu Kaka, ni aibu...kesi inaenda kumwacha mtu uchi hii
Ushabiki tu umekujaa , tungekua hatujuhi kama Kingai na Sabaya waliteuliwa na Magufuli kufanya kazi pamoja Hai ili kumdhibiti Mheshimiwa Mbowe sawa.

Aibu yenu hii MaCCM mnaigawa nchi vipande vipande.
 
kabisa mkuu yaani jamaa alieleza straight hakuna chenga onampaka mashahidi wa ukamataji upekuzi mwenyekiti wa mtaa walishuhudia unakwepaje hapo sasa uje useme uliteswa ili useme yaani kibatala kwaakili yake ndogo aliwalisha maneno wadanganye mahakama wakafeli sasaushahidi mwaaaaaaaaaaaaaa gaid jela
Akili yako haina akili au ni makusudi tu.
 
Ushabiki tu umekujaa , tungekua hatujuhi kama Kingai na Sabaya waliteuliwa na Magufuli kufanya kazi pamoja Hai ili kumdhibiti Mheshimiwa Mbowe sawa.
Aibu yenu hii MaCCM mnaigawa nchi vipande vipande.
Nchi igawanyike kwa lipi? Alishindwa kuigawa nchi Lowassa 2015 ije kuwa leo? Hakuna takataka yeyote TZ hii anaweza kusababisha nchi igawanyike
 
Akili yako haina akili au ni makusudi tu.
Huna hoja ya kubishana na mimi maana unjuwa kabisa matendo maovu ya mbowe yana wekwa kweupeeeeeeeeeeee yaani huna cha kuniambia bora unyamaze maana unaweza kuchwekwa hadi na watoto wako kama wanasoma commet zako
 
yaani unapoteza mudakwa hizo hasirazako hapo hakuna aliyelazimishwa wale walishatoswa na mbowe wakaamua kuusema ukweli kwa maelezo yao polisi baadae mkawalisha maneno waseme waliteswa ndipo kibatala wakili njaa akafungua kesi ndogo ambayo nayo imekama maana ni janja janja tu ili kuwanasua na uhalifuwao unajisumbua tu najuwa unaakili ila kama huna akili endelea kubisha mwisho wa siku nimiaka mingi sana jela wacha tuka mlisi mkewake maana alitaka kuangamiza taifa
MaCCM aliewaroga kafa . Mimi sina hasira na kesi za kisiasa, hasa hizi ziliandaliwa kwenye uchaguzi na wapambe wa Magufuli ili kumfurahisha Magufuli.Kufunga watu mnatufunga kila siku, hakuna jipya.
 
26 October 2021



Tupo tunafuatilia kwa karibu mwenendo mzima wa kesi hii ya kihistoria.

“I’ve been reading that transcript like my Bible every night to try and get some understanding of what happened.” “But unfortunately … whatever the court subjectively believes is not important – the court has to look at the evidence in front of it.” - magistrate Prince Manyathi, the Kempton Park Regional Court South Africa

Kesi namba 16 / 2021 Mrejesho toka Mahakama Kuu Division ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, juu ya mwenendo wa kesi 26 October 2021
Shahidi: Maelezo ya Luteni Denis, Kuhusu Kukata Miti na Kutaka Kufanya Vurugu.

Kibatala: Umemueleza Jaji sehemu yoyote kwamba ulienda huko Morogoro Mpaka Iringa Kuona Miti iliyotakiwa kukatwa.?

Shahidi: Hapana Wala sijaenda

Kibatala: Umetaja Maandamano yalitakiwa kufanyika wapi hadi wapi

Shahidi: Hapana sijasema

Kibatala: we Polisi Mzoefu Miaka 18 ya Upelelezi Kazini, najua Siyo Mwanasheria ila Unasimamia Sheria je Unafahamu Mtu anapokiri anatakiwa kukiri Kila Kipengele anachoshitakiwa

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Ulizungumza Chochote Kuhusu Mshitakiwa Mbowe kuwapo Morogoro kati ya Tarehe 1 May na 20 August 2020

Shahidi: Sikuzungumza

Kibatala: Ulizungumza Katika ya Tarehe 01¬May 2020 na 20 August 2020 kuwa washitakiwa watatu walikuwa Arusha

Shahidi: Ndiyo nilizungumza ila siyo Leo

Kibatala: kwa ufahamu wako kama Mpelelezi Mkuu umewahi Kugundua kuwa Freeman Mbowe na Watuhumiwa wenzake Mkoani Morogoro

Shahidi: na Mbowe Hapana

Kibatala: Sheria inayounda Shitaka Unatakiwa kuitamka kikamilifu ili haki za Mshitakiwa ziwe zimekamilika, Unafahamu..?

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Je unafahamu sub section mbili zote zinazozungumzi hilo

Shahidi: hiyo ni Mpaka Niperuzi

Kibatala: aahhhhhh Sawa Ngoja nimpatie Sheria

JAJI: anacheka, Sasa atafahamu Vipi kuwa yenyewe

Kibatala: Nitafutie sehemu katika Maelezo kuwa Mshitakiwa wa Pili amekiri Bastola ni ya kwake

Shahidi: Hakuna Mheshimiwa Jaji

Kibatala: Nitafutie katika Maelezo ambayo Mshtakiwa amekiri kuwa Bastola hiyo alitaka kutumia kumdhuru Sabaya, Kutumia kwenye Maandamano au Kutumia Kukata Miti

Shahidi: Hilo Mheshimiwa Jajo hakuna
 
Tayari baadhi ya Wadau wa Maendeleo, akiwemo Mwakilishi wa Ubalozi wa Canada wamewasili Mahakamani.


Hadi saa 3:30 asubuhi hii Watuhumiwa walikuwa bado hawajaletwa Mahakamani.

====

Hatimaye Mbowe na wenzake wameletwa Mahakamani

Jaji Joachim Tiganga ameingia Mahakamani

Wakili wa serikali Robert Kidando anatambulisha Jopo lake
1. Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulumanywa Majigo
6. Jenitreza Kitali

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo Lake
1. Peter kibatala
2. Jeremiah Mtobesya
3. Michael Mwangasa
4. Nashon Nkungu
5. Dickson Matata
6. Alex Massaba
7. Jonathan Mndeme
8. Hadija Aron 9.
Idd Msawanga

Jaji anaomba Kuwaona Washitakiwa wote 1,2,3 na 4

Wanainuka Kwa kutajwa kwa Namba

Wakili wa Serikali anaomba kesi Kuendelea na Shahidi yupo tayari Lakini Kabla ya Kuendelea anaomba kufuatilia kuhusiana mabadiriko yaliyopalekea mpaka Mheshimiwa Jaji Kuja mwingine kwa mujibu ya kifungu cha 299 CPA (Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai).

JAJI: Upande wa utetezi

Peter Kibatala: hatotatumia Haki ya kumuita tena Shahidi kwa kesi Inayoendelea hapa.

Jaji anaandika.

JAJI: wote mnafahamu na mlikwepo siku ya tarehe 20 mwezi huu na Jaji aliyekuwepo alielekeza Jaji Mwingine atakuja kuendelea na Kesi hii, Na Jaji Mwingine Ndiyo Mimi, kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 Kifungu cha 299.

JAJI: Kwamba Upande wa Utetezi Mnahaki ya a Kumuita tena shahidi kwa kuwa Mmesema hamna nia nitawaruhusu Upande wa Jamhuri Kumuita sasa Shahidi wao tuweze Kuendelea. Mawakili wote Wanainuka ishara ya Kukubaliana na Uamuzi wa Jaji na Kupokea Maelekezo ya Mahakama.

Wakili wa Serikali anatoka Kwenda Kumuita Shahidi wa leo.

Mahakama ipo Kimya

ACP KINGAI anaingia na Kupanda Kizimbani.

Robert Kidando Wakili wa Serikali anamtaarifu Jaji Kuwa Shahidi amefika.

JAJI: Majina yako Tafadhali

SHAHIDI: ACP Ramadhan Kingai

JAJI: Unakumbuka Uliwahi Kufika Mahakamani, ukaapishwa kutoa Ushahidi, Mahakama inakukumbusha Upo chini ya Kiapo hicho. SHAHIDI: sawa Mheshimiwa

JAJI: Mtakumbuka Mawakili kuwa Siku ya Tarehe 20 Jaji alipokea Kielelezo, baada ya Kupokelewa Kinatakiwa Kusomwa Mahakamani. Naomba Kuanzia hapo Shahidi akabidhiwe Kielelezo aweze Kusoma Kielelezo.

WAKILI WA SERIKALI: Soma Sasa Kielelezo Kuanzia kurasa ya kwanza.

SHAHIDI: Adama Kasekwa anaishi Chalinze Maelezo ya Onyo Chini kifungu cha Sheria ya Makosa ya Jinai Sura ya 20. MIMI kingai nakuonya wewe Adam Kasekwa

SHAHIDI: Ulazimishwi kusema lolote Pia unaweza Kualika Ndugu, Jamaa au Mwanasheria Kushuhudia utoajo wako Maelezo. Mtuhumiwa akasaini na Mimi nikasaini.

MAJIBU YA ONYO

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo..

MIMI Adam Kasekwa anaonya na Kingai Chini ya Kifungu cha 24 cha Sheria Mwenendo wa Makosa ya Jinai Silazimishwi na yoyote Kutoa Maelezo yangu. Je, Upo tayari Kutoa Maelezo Yako.

Jibu, Ndiyo Nipo tayari.

Shahidi anasoma kielelezo: Maelezo yamechukuliwa Katika Ofisi ya RCO ilala MIMI Adam Kasekwa Nimezaliwa Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Ileje... Mwaka 2011 nilijiunga na Recruting Maktopora. Nikachaguliwa Kujiung na Mafunzo Ukomando 92KJ.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Mwaka 2014 niliteukiwa kwenda kituo cha Msangani Kujifunza ulinzi, amani na nikachaguliwa Kwenda DR Congo. Mwaka 2017 nilimaliza Mkataba na kurejea Nilipata malipo na Kumuoa Mke wangu Lilian ambaye naishi naye Mpaka Leo.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Nimepata naye Mtoto Mmoja. Nilirudi nikaa Miezi 6 kazini Nikaugua Ugonjwa wa aKili Nikaachishwa kazi na kulipwa mafao ya Millioni 4 na Laki 6.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Je unamfahamu Luteni Denis? Ndiyo, nilikuwa Mkinga Mawasiliano hayapatikani. Niliporudi nikaambiwa mwenzangu ananitafuta.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Niliporudi nyumbani nilimpigia Simu Mwenzangu Mohammed Ling'wenya Kwamba Kuna kazi ya VIP protection. Akaniambia inabidi twende Morogoro Kumuona Luteni Urio. Tulipoenda akatuambia Kuna kazi ya VIP protection ya kumlinda Freeman Mbowe

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Akatupatia TSh 21,000 nauli ya Kwenda Moshi. Siku hiyo hiyo tulirudi Chalinze na kuanza Safari ya kwenda Moshi Tulipokelewa na Dereva wake anayeitwa Willy Alitupokea na Pick Up Nyeupe yenye maandishi ya M4C.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Tukaenda Mpaka Kwenye Hotel Ya Mheshimiwa Mbowe Huko tulimkuta Khalfani Bwire aliyetutambulisha kwa Mbowe, "Mkuu wale Vijana tuliowaagiza ndiyo hawa hapa." MBOWE akatueleza Kuwa Sabaya anamvuruga sana na anamvuruga wapiga Kura.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Kwamba anawatisha Wapiga kura wake kiasi cha Kuhatarisha Kurudi kwake. Na kwamba, akatuelekeza tumdhuru Kwa Njia yoyote. Akatuelekeza Maeneo yake ya Moshi na Arusha.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Tulipanga kumdhuru kwa Spray Spray ya sumu alitafuta Mohammed Ling'wenya

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Siku inayofuata tulikuwa Mimi na Mohammed na wanachana wawili siwakumbuki Majina Baada ya Kufika Dar es Salaam Tulimfikisha Mheshimiwa Mbowe Nyumbani

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Akatukabidhi TSh Laki 2 kwaaajili ya Kununua Nguo. Kwa sababu Kesho yake tulikuwa tunampokea Mheshimiwa Lissu. Na Siku ya tarehe 27 Julai Mbowe alitutumia Kila moja TSh 78 Elfu ya Nauli Ya Kwenda Moshi.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: SIKU ya Tarehe 01 August Tulienda Moshi Tukamkuta Mbowe akiwa na Khalfani Bwire Akatuelekeza Kuwa tufanye ile kazi yake Haraka Akatuelekeza Maeneo anayokaa Sabaya kama vile Milestone PIA Akatuelekeza Tuje DSM, Kuchoma Vituo Vya Mafuta.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Kwamba yeye anatachochea maandamano ILi Serikali ionekane Imeshindwa Kuandaa Uchaguzi. Tulienda Maeneo ya Boma Ng'ombe Njia ya kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kumfuatilia.

Siku ya terehe 03 tulienda Maeneo ya RAU madukani kwa ajili ya kubana Matumizi. Kwa sababu Mheshimiwa alituachia Pesa Laki Moja na Nusu kwa ajili ya kukaa, isingetosha. Tulienda Kukaa kwa Dada yake kukaa kwaajili ya Kubana Matumizi.

Swala la Kupanga Ugaidi ni la kweli Na swala la a kukutwa na Silaha ni la kweli Wakati Polisi wananikamata pia walinikuta na Heroine Baada ya kuchukua Vitu hivyo Askari walisaini na Mimi nikasaini na Polisi walichukua Vitu hivyo kwenda Central

Baada ya Maelezo hayo Adam Kasekwa akasaini Na Mimi Kingai nikasaini Baada ya Kuchukua Maelezo hayo Muda ulikuwa ni saaa tatu.

Wakili wa Serikali: ACP Kingai Kutokana na Maelezo uliyoyasoma hapa mahakamani Yeye alikuelza nini Kutokana na Maelezo Uliyoyasoma Mahakamani Shahidi: alikiri kuwa anamfahamu Luteni Urio. Alikiri Kupewa Maelekezo ya kazi kutoka kwa Mheshimiwa Mbowe

Shahidi: Alikiri Pia alipewa Maelekezo ya kazi Kutoka akwa Mbowe Kupitia Kwa Luteni Deni Urio. Alikiri Pia kuwapo Moshi tarehe 24 Mwezi wa 07, 2020

Shahidi: Alikiri Pia kuwapo Moshi na wenzake Mohammed Ling'wenya na Mwenzake aliyemtaja Kwa Jina la Kakobe. Baada ya Ufutailiaji tukamfahamu ni Moses Lijenje. Alikiri Pia kufanya Mkutano yeye na wenzake wanne.

Yeye Mwenyewe, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya, Moses Lijenje (Aliyemtaja Kwa Jina la Kakobe) Khalfani Bwire na Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: kwa Mujibu wa Mkutano huo nini kiliendelea. Shahidi: Mbowe alitoa Maelezo kuwa Sabaya anamfanyia Vurugu, (Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai)

Wakili wa Serikali: kitu gani Kingine alikueleza Shahidi: Mtuhumiwa alikiri Kupewa Pesa 150,000/= kukidhi Mahitaji kipindi watakapokuwa hapo Moshi.

Wakili wa Serikali: tueleze Shahidi kuhusiana na kilichofuata Shahidi: Alikiri Kuwa Siku ya Tarehe 01 Mwezi wa Nane saa 11 Alfajiri kabla ya Safari ya Kuja DAR ES SALAAM Aliwaelekeza wamdhuru Ole Sabaya.

Shahidi: Akawaonyesha Picha ya Ole Sabaya Kupitia Simu yake ya mkononi Aliwapa Maelekezo Kufanya kazi hiyo na Kwamba baada ya hapo atawataka warudi Dar es Salaam. Alipanga kuwapa kazi ya kwenda Kulipua Vituo Vya Mafuta. Alipanga kufanya Vurugu kwenye masoko.

Mtobesya: OBJECTION Naomba Shahidi ajielekeze Kwenye kikichoandikwa kwenye Statement Mambo ya Kituo cha Mafuta na Masoko havijatajwa.

Jaji: Kwahiyo a some?

Mtobesya: ajielekeze kikichoandikwa hata kama ana Rudia Kuelezea, Sheria inasema Statement itajielezea Yenyewe.

JAJI: Upande wa Mashitaka

Wakili wa Serikali: Sahihi Mheshimiwa tutarekebisha.

Wakili wa Serikali: Alikueleza Lengo ilikuwa ni nini

Shahidi: Lengo ni Serikal ionekane imefeli Alikiri Pia kukamatwa na Polisi Siku ya tarehe 05 Mwezi wa 08, 2020 akiwa Rau Madukani.

Alikiri Pia kukamatwa na Pistol aina ya Ruvern ikiwa na Risasi 03.

Shahidi ACP KINGAI: Alikiri kukamatwa na Kete 58 za Madawa aina ya Heroine.

Wakili wa Serikali: baada ya kuwa umeandika Maelezo hayo, yeye ulimpeleka wapi kwa Siku hiyo.

Shahidi ACP KINGAI: ilikuwa Siku ya tarehe 07 Mwezi wa 08, 2020 nilimrudisha Mahabusu.

Wakili wa Serikali: Shughuli gani Nyingine ili endelea baada ya Shughuli hii

Shahidi ACP KINGAI: tuliendelea na Upelelezi ya Kuwatafuta watuhumiwa wengine. Maeneo ya Chang'ombe tulimkamata Khalfani Bwire.

Wakili wa Serikali: Kwa tuhuma Gani

Shahidi ACP KINGAI: Kwa tuhuma hizi hizi za Kula Njama kutenda Matendo ya Ugaidi.

Wakili wa Serikali: nini kiliendelea

Shahidi ACP KINGAI: nikimtaka Khalfani Bwire aandike Maelezo yake

Wakili wa Serikali: elezea Kuhusu Kumkamata kwake

Shahidi ACP KINGAI: baada ya a kuwasiliana na Askari aliyekuwa kwenye Pointi akiwa kwenye gari, tukielekeza Gari iingie Kituo cha polisi Chang'ombe. Tukawa tumeingia pale na Inspector Mahita na ASP Jumamne.

Jaji: ASP nani? Shahidi: Jumanne

Wakili wa Serikali: baada ya Kumkamata Mlimpeleka wapi

Shahidi: tuliekeza Superitendent Lukangira wa hapo hapo Chang'ombe. Hii ni baada ya Mtuhumiwa kutuelekeza hana Makazi hapa Dar es Salaam ni Mkazi wa Ngerengere.

Wakili wa Serikali: Nia ya Kuuliza kwake ni wapi ilikuwa ni ya nini

Shahidi: nia ilikuwa kufanikisha Shughuli za kiupepelezi

Wakili wa Serikali: baada ya Lukagingira kuandika Maelezo yake nini Kilifuata

Shahidi: Tukawa tunaendelea Kufuatilia Makazi yake, Tofauti na Taarifa alivyokuwa ametoa yeye kwakuwa tulijua haiwezekani awe kila Siku anaenda Ngerengere.

Wakili wa Serikali: Wakati Unapata Taarifa ana makazi Wilaya ya Temeke, elezea Sasa Maelezo yalikuwa yanaandikiwa wapi

Shahidi: Maelezo yalikuwa yanachukuliwa Kituo cha Polisi Chang'ombe na Mimi niliweka Bass Central polisi (Ilala).

Wakili wa Serikali: baada ya Kutoa Maelekezo Hatua Kuchukua Maelezo Isimame, nini kilifuata

Shahidi: tulipata Taarifa Mtuhumiwa anakaa Temeke Makangarawe, Tuliungana na Detective John wa Temeke na RCO kwa ajili ya kwenda Kumpekua Makazi yake.

Wakili wa Serikali: Mlienda sehemu ipi haswa huko Mkangarawe

Shahidi: Ule Mtaa Jina Limenitoka

Wakili wa Serikali: Uliwezaje Kuutambua sasa

Shahidi: tukielekezwa na Watu hadi Nyumba alipokuwa amepanga Mtuhumiwa.

Wakili wa Serikali: Elezea sasa hiyo Shughuli ilifanyikaje na Khalfani Bwire alikuwa wapi.

Shahidi: Tuliongozana na Mtuhumiwa, Tukamtafuta Mwenyekiti wa Ule mtaa, Tukamkuta na Mwenye nyumba aliyempangisha Khalfani Bwire na hata Mke wake alikwepo.

Wakili wa Serikali: huyu Mwenyekiti ni wanini?

Shahidi: Ni Mwenyekiti wa Mtaa

Wakili wa Serikali: Nini Kilifuata

Shahidi: Nilimuelekeza ASP Jumanne Kwa Kushirikiana na Detective John Kutoka Ofisi ya RCO Temeke na kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Mtaa na hata Mke wake.

Wakili wa Serikali: Elezea sasa Katika Upekuzi huo Mlikuta nini?

Shahidi: Vitu mbalimbali vilipatikana kama Uniforms za JWTZ, Masharti ya JWTZ, Tshirt za JWZT, name tags za kwake za JWTZ.

Wakili wa Serikali: baada ya Kupata Uniforms na Vifaa Mbalimbali nini Kilifanyika baada ya Kupata Vitu hivyo.

Shahidi: Viliorodheshwa katika Hati ya Uchukuaji Mali. Wakati wa Upekuzi tulikuta Kidaftari kilichokuwa na Ramani na Majina ya Vituo Vya Mafuta.

Wakili wa Serikali: baada ya kuorodhesha kitu gani kilifanyika

Shahidi: baada ya Kuwa Viliorodheshwa yaliandikwa Majina ya walioshuhudia Upekuzi huo. Pia wakasaini Hati ya Uchukuaji Mali. Mtuhumiwa pia alisaini Hati ya Uchukuaji Mali na aliyepekua alisaini Hati hiyo.

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukamilisha Hati ya Uchukuaji Mali, Kitu gani Kiliendelea

Shahidi: Nilikuwa nimeelekeza Mashahidi walioshuhudia waandikwe Maelezo pale pale

Wakili wa Serikali: baada ya Kukamilisha

Shahidi: Tulichukua Vitu tulivyo orodhesha na Mtuhumiwa akarudishwa a kituo Cha Polisi.

Wakili wa Serikali: Kituo gani cha Polisi Shahidi: Chang'ombe

Wakili wa Serikali: Baada ya kumrudisha Kituo cha Polisi Chang'ombe Kitu gani pia Kiliendelea.

Shahidi: Mtuhumiwa tulimkamata na Kidaftari chenye Ramani ya Vituo Vya Mafuta Dar es salaam, Soko la Kilombero Arusha.

Tukachukua Sampuli za Miandiko ya Watuhumiwa wote. Lakini pia tuliendelea na hatua ya kuwatafuta watuhumiwa wengine

Wakili wa Serikali: watuhumiwa gani wengine Mlikuwa mnawatafuta

Shahidi: Watuhumiwa wengine tuliokuwa tunawafutilia ni Mtu alikuwa anaitwa Gabriel, Lijenje, Malima, Khalid na Jamaa Mmoja anaitwa Kaaya.

Wakili wa Serikali: nini hatima ya hao mliokuwa mnawafuatilia

Shahidi: Ukimuondoa Mtu Mmoja anaitwa Malima, Watuhumiwa wote walifikishwa mahakamani.

Wakili wa Serikali: vipi kuhusu moses Lijenje Shahidi: bado hatujafanikiwa Kumpata

Wakili wa Serikali: Hapa Mahakamani kuna Washitakiwa Wanne inakuwa je hao wengine hawapo Mahakamani kama Walifumgukiwa Mashitaka

Shahidi: walifutiwa Mashitaka baada ya Kuonekana Ushahidi hakuwa wakutosha ukilinganisha na wenzao.

Wakili wa Serikali: ACP kingai katika Ushahidi wako tangu Mwanzoni umezungumzia kukamatwa Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Khalfani Bwire Vipi ukamatwaji wake Mshitakiwa wa Nne.

Shahidi: Freeman Mbowe alikamatwa 21 July 2020 akiwa Mwanza

Wakili wa Serikali: Kwa tuhuma gani

Shahidi: Kwa tuhuma hizi hizi

Wakili wa Serikali: Wakati Unatoa Ushahidi wako Ulizungumzia kukamatwa hawa wengine Mwaka 2020 na huyu 2021 elezea Ilikuwa je hapa Mahakamani.

Shahidi: Tulikuwa tunajirishisha haswa uhusika wake. Tulikuwa bado tunaendelea Kufuatilia mawasiliano Na Uchunguzi wa Forensic ambao ulikuwa unahusiana na Shauri hili

Wakili wa Serikali: Sababu ukamataji ulifanyika 21 July Mwaka 2020, ni lini taarifa zilifahamika rasmi.

Shahidi: Zilifahamika Mwanzoni July 2020

Wakili wa Serikali: wakati anakamatwa Upelelezi ulikuwa umefikia Hatua gani

Shahidi: Upelelezi wetu kwa muda huo tunamkamata ulikuwa umekamilika.

Wakili wa Serikali: Upelelezi wa aina gani ulikuwa unaendelea kwa Mshitakiwa nne

Shahidi: Tulifanya Forensic na Divices za Kieletronic tuliokuwa tunafuatilia Kujiridhisha dhidi yake na Tuhuma zilizokuwa zinamkabili.

Wakili wa Serikali: wakati Unatoa Ushahidi wako Mwanzoni ulisema Ulielezea Kuwa Umelekeza kufungua Jalada la Tuhuma za Kigaidi.

Shahidi: Kulingana na Taarifa ambazo tulikuwa tumezipata kwa Luteni Urio na aina Ya Vitendo vilivyokuwa Vimepangwa na Watuhumiwa Ilikuwa ni Kudhuru Viongozi wa Serikali, kufanya Vurugu sehemu zenye watu wengi, Kulipua Vituo Vya Mafuta, Hata Miti kwenye highway kukatwa Kuzuiwa Magari yasipite, Hasa katika Barabara ya Morogoro kwenda Iringa.

Wakili wa Serikali: Ukatafsiri ni Vitendo gani

Shahidi: Vitendo vyenye kuleta hofu kwa Wanachi Kujiona hawapo salama, Ni Vitendo vinavyoleta Tafsiri la Shitaka la Ugaidi

Wakili wa Serikali: ulisema katika Taarifa ya Luteni Urio ulisema walipanga Kuonyesha kuwa Nchi haitawaliki.

Mtobesya: OBJECTION kaka yangu Wakili Msomi ajielekeze Kwenye fact siyo Opinion Maana huyo ni Shahidi wa Fact, He is doing too Much Sasa Maana Mwanzo tulijua ameteleza.

Wakili wa Serikali: Sawa Mheshimiwa Jaji nitaomba nijielekeze sawa Sasa.

Wakili wa serikali: Vitendo hivi vilipangwa Vifanyike wapi

Shahidi: Mwanza, Moshi, Dar es Salaam na Arusha

Wakili wa Serikali: Vilikuwa Vifanyike Lini

Shahidi: Kabla ya Uchaguzi wa Mwaka Jana

Wakili wa Serikali: ni hayo tu Kwa sasa Mheshimiwa Jaji

Jaji: Upande wa utetezi

Mtobesya: Asante Mheshimiwa Jaji nitaomba niendelee kwa Niaba ya Mshitakiwa wa kwanza.

Mtobesya: ni sahihi Shahidi wewe ulikuwa ni sehemu ya waliokuwa wanahusika na upelelezi wa Kesi hii

Shahidi: ni sahihi

Mtobesya: ni sahihi kuwa Baada ya kupokea Maelezo kwa DCI BOAZI mkafungua Jalada

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji ni lini Mlifungua Jalada

Shahidi: Yalikuwa Majalada Mawili la upelelezi na Kesi

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Lilifunguliwa Jalada la Uchunguzi

Mtobesya: Uchunguzi au Upelelezi

Shahidi: yote ni yale yele labda useme unataka Jalada gani

Mtobesya: wewe Ndiye unayetoa Ushahidi

Shahidi: Sawa Mwanzo Lilifumguliwa Jalada la Uchunguzi wa Kula njama. Ilikuwa July Mwaka Jana.
Mkuu kama itawezekana kila au baada ya updates moja kuwe na alama inayoitenganisha na nyingine ili itupe wepesi wa kuyatafuta maandishi yanayofuata.
 
Sawa, fungeni tu watu na makesi ya kisiasa na CHADEMA ifuteni. Ili CCM isipoteze chaguzi. Chama dola ehee
Bado hakijapatikana chama mbadala wa kuongoza nchi hii, vilivyopo vyote ni vya kihuni na wachumia tumbo, wapo wapi akina Mdee, Slaa, Mashinji, Lowassa n.k., n.k., watu waliwaamini na kuwapigania, wengine walipoteza na maisha yao, mwisho wa siku kwa njaa zao za kipuuzi wakasaliti mapambano!! In short bado hakuna wapinzani makini TZ wa kupewa nchi...
 
huna hoja ya kubishana na mimi maana unjuwa kabisa matendo maovu ya mbowe yana wekwa kweupeeeeeeeeeeee yaani huna cha kuniambia bora unyamaze maana unaweza kuchwekwa hadi na watoto wako kama wanasoma commet zako
Haaa haaa just haa haa MaCCM mnaangaika humu kupiga propaganda ili uongo e Kingai uonekane, ila ni ukweli MaCCM mmekwama. Kesi ya kisiasa na yauongo. Lengo ni kuifuta CHADEMA inawanyima MaCCM kushinda chaguzi.
 
Tuache ushabiki...

Mawakili wa Mbowe waumize vichwa kupambana na kesi na wapenzi na mashabiki tuache siasa...tuwape uhuru mawakili wapambane na kesi kwa vifungu vya sheria kumchomoa au kumnusuru mwenyekiti..

Kuna vingi hatuvijui, acha mapambano ya kisheria yaendelee, ikiwezekana na TL aje naye kuongeza nguvu...hii ngoma haijakaa sawa...
 
Mawakili wa Bwana Mwamba wanauliza maswali ya kipuuzi sana, kabla hajachelewa awatoe hawa vilaza
 
Bado hakijapatikana chama mbadala wa kuongoza nchi hii, vilivyopo vyote ni vya kihuni na wachumia tumbo, wapo wapi akina Mdee, Slaa, Mashinji, Lowassa n.k., n.k., watu waliwaamini na kuwapigania, wengine walipoteza na maisha yao, mwisho wa siku kwa njaa zao za kipuuzi wakasaliti mapambano!! In short bado hakuna wapinzani makini TZ wa kupewa nchi...
Acheni kuwapa watu kesi za kisiasa na zauongo, kuiba na kukimbia na masanduku ya kura haitoshi . Uamini ulichoandika.😃
 
Walianza kuchoma ofisi zao na kusingizia CCM! Wakapiga mabomu mkutano wao wenyewe na kusingizia polisi.

Wakaona mchezo umenoga wakaamua kulipua “nchi”, uroho wa madaraka kwa gharama yeyote.

Sasa ni wazi hata aliyemuua Akwilina ni nani.
 
Back
Top Bottom