Yaliyojiri Kesi ya Mbowe: RPC Kingai aeleza Mbowe alivyopanga kumdhuru Ole Sabaya. Kesi yaahirishwa hadi 27 Oktoba 2021

Kwani huyu kingai wakati anawakamata hawa watuhumiwa yeye alikuwa RC wa mkoa gani ? Make mi sielewi nasikia hawa walikamatiwa moshi lakini yeye ni Rpc kinondoni kanda maalum Dar mwenye kuelewa anisaidie
 
RPC Kingai ameeleza hatua kwa hatua bila kuacha shaka jinsi Freeman Mbowe alivyopanga kumuuwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Ole Lengai Sabaya kwa kutumia perfume ya sumu kwa madai kuwa Sabaya alikuwa anatishia nafasi ya Mbowe kuendelea kuwa mbunge wa jimbo la Hai.

====
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai akisoma maelezo ya mshtakiwa wa pili katika kesi ya uhujumu uchumi, Adam Kasekwa amesema mtuhumiwa huyo alisema Freeman Mbowe alipanga kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Katika ushahidi alioutoa leo, Oktoba 26, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Kingai amesoma maelezo ya mtuhumiwa huyo kwamba Mbowe alisema Sabaya anahatarisha nafasi yake ya kuendelea kuwa mbunge wa Hai.

Ifuatayo ni sehemu ya maelezo ya mshtakiwa Adamu kama yalivyosomwa na RPC Kingai:

“Mbowe alituelekeza tufuatilie nyendo zake na tumdhuru kwa spray ya sumu. Ling'wenya alifuatilia mtu wa kupata sumu. Tarehe 27 tulirudi Dar na magari mawili pamoja na Mbowe na mlinzi wake.

“Baada ya kufika Dar tulifikishwa Mikocheni mimi na Ling'wenya tulipewa Sh200,000 tujiandae.Baadaye tulipewa nauli turudi Moshi. Agosti Mosi saa 11 alfajiri Mbowe alituita akasema tutekeleze maelekezo ya kumdhuru Sabaya.

“Akituonesha picha ya Sabaya na maeneo anauyopenda kutembelea. Alituelekeza baada ya kazi ya Sabaya turudi Dar kutekeleza kazi nyingine nyeti kulipua vituo vya mafuta na kushinikiza maandamano ili Serikaki ionekane imeshindwa maana inatuchukia sisi wapinzani.

“Yeye aliondoka kurudi Dar sisi tukabaki kutekeleza kumdhuru Sabaya Tarehe 3 Atosti tulienda eneo la Rao Madukani kwa dada yake Ling'wenya ili kubana matumizi maana Mheshimiwa alituachia Sh150,000

“Tulikamatwa na askari tukituhumiwa kukutwa na dawa za kulevya na kupanga njama za ugaidi. Tuhuma hizo ni za kweli na pia kukutwa na silaha ni za kweli na nilikutwa na simu yangu ya Itel.

“Nilisaini hati ya kuchukuliwa mali na askari nao wakasaini. Nikachukuliwa kwenda Central Moshi. Uthibitisho haya maelezo ni ya kweli kwa saini.

“Muda wa kumaliza kuandika maelezo hayo ilkiuwa ni saa 3"

Wakili wa Serikali Mwandamizi SSA Kidando alimtaka ACP Kingai aelezee alichoelezwa na mshtakiwa huyo wa pili Adamu.

ACP Kingai :Alikiri kukutana na wenzake kwa ajili kwenda kwa Mbowe, alikiri kupewa nauli kwenda Moshi kukutana na Mbowe, alikiri kuwepo Moshi tarehe 24 -26 Julai 2020, alikiri kuwepo yeye na wenzake wawili akiwemo Ling'wenya na mtu mwingine.

“Alikiri tarehe 25 usiku kufanya mkutano yeye na Ling'wenya, Moses Lujenje maarufu Kakobe, Hassan Bwire na Freeman Mbowe"

SSA Kidando: Nini kiliendelea?

ACP Kingai : Alikiri kwenye mkutano alielekezwa na Mbowe kumdhuru DC Sabaya kwa njia yoyote ile.

SSA Kidando: Kitu gani kingine alikueleza?

ACP Kingai: Shahidi pia alikiri kupewa pesa na Mbowe Sh150,000 kukidhi mahitaji hapo Moshi, alikiri Agosti Mosi 2020 alfajiri Mbowe aliwaita tena na kuwapa maelekezo, kwamba wahakikishe wanayafanyia kazi.

“Kumdhuru Sabaya na ili wawe na uhakika Mbowe aliwaonyesha picha ya Sabaya kupitia simu yake, aliwalekeza wamalize kazi hiyo ya Moshi halafu warudi Dar kufanya kazi nyingine nyeti.

“Alitaja kazi hiyo kwamba walipanga wakalipue vituo vya mafuta, lakini pia kufanya vurugu kwenye masoko na maeno ya watu wengi”.
 
Jeshi lilifukuza mtu mwenye ugonjwa wa akili

Maana yake hata Kama maelezo aliyoyatoa hakuteswa kuyatoa lakini Ni chizi hivyo maelezo yake hayana ukweli wowote.

Mtu chizi anawezaje kutoa maelezo?

Halafu sabaya Mahakama imeshaonyesha Ni jambazi! Kuna kosa gani kwangu Mimi kumuua jambazi ambaye ananifatilia mpaka kwenye hotel yangu kuniua?.

Hapa hakuna kesi ya ugaidi Ni porojo tu
 
Umejitahidi kweli kweli kuripoti
 
sawa TU. ILA TUJUA TU UKWELI
 
Aaaa,Kama sio kudharirishana hii ndio Nini sasa?
* Nikaue mtu Hai
+ Nikakate miti iringa
*Nikachome vituo vya mafuta morogoro
Malipo 150,000/= watu wawili!
Mbona haingii akilini kwa muandika maelezo hata kwa mtoa maelezo pia, au nyinyi mnaonaje ndugu zangu.
Maana Mimi ninavyo jua hata kwa wale wazee wa Robbin hood za macho mekundu kule Shinyanga huwa nasikia wanapewa mpaka maksai 5 x 700,000/=
Makomandoo 75.000/= kazi 3 za kigaidi?
Akili yangu inakataa hata mzee wa Robbin hood hawaezi kubari hiyo biashara.
 
Muendelezo wa kesi vipi update mbona haziji tena
 
Kesi ya kipumbavu kabisa
 
Bado najiuliza, ili ugaidi ufanyike kuna namna mbili..

Lazima wahusika kwa maana ya watekeleza ugaidi wawe employed kwa malipo fulani, SIJAONA POPOTE PANAPOONYESHA MALIPO YAO YA KAZI AU MAKUBALIANO YA MALIPO..

wahusika wa ugaidi wanakuwa ni waumini wa ideology fulani, wanakuwa wamejitolea kufa kwa ajili ya itikadi yao ambayo hapa ni CDM... HAKUNA NILIPOONA HAWA WALIKUWA WANACHAMA WA CDM AU WANA KADI YA UANACHAMA WA CDM AU KUNA MAHALA WALIKAA KWA MUDA KUWA BRAINWASHED..

sasa ugaidi huo walikuwa wanautekeleza kwa namna ipi...
 
Lissu naye angekuwepo apige maswali ya kutosha mpaka ajinyee huyu mzee mpuuzi
 
Hii kesi ipo very technical kwenye baadhi ya maeneo shahidi aliposema alifukuzwa kazi kwa sababu za ugonjwa wa kichaa upande wa utetezi wajitahidi wapate hicho kielelezo waje wakitumie kwenye utetezi

kwa kuwa plan A ya kupinga kielelezo imeshindikana basi plan B wakati wa utetezi wajielekeze kwenye mental status ya mtuhumiwa wakati anahojiwa.

manake kwa kichaa kama huyu wakati anahojiwa hakuna uthibitisho wa kitaalam unaosapoti kwamba mentally alikuwa fit.

na shahidi wa jamuhuri hajazungumzia chochote aidha wakati wanamuhoji kulikuwa na medical proof kwamba alikuwa timamu..ushahidi wa kichaa thamani yake ni ndogo sana.

Vijana wa utetezi barabara hiyo nimewapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…