Yaliyojiri Kesi ya Mbowe: RPC Kingai aeleza Mbowe alivyopanga kumdhuru Ole Sabaya. Kesi yaahirishwa hadi 27 Oktoba 2021

Yaliyojiri Kesi ya Mbowe: RPC Kingai aeleza Mbowe alivyopanga kumdhuru Ole Sabaya. Kesi yaahirishwa hadi 27 Oktoba 2021

Kwani huyu kingai wakati anawakamata hawa watuhumiwa yeye alikuwa RC wa mkoa gani ? Make mi sielewi nasikia hawa walikamatiwa moshi lakini yeye ni Rpc kinondoni kanda maalum Dar mwenye kuelewa anisaidie
 
RPC Kingai ameeleza hatua kwa hatua bila kuacha shaka jinsi Freeman Mbowe alivyopanga kumuuwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Ole Lengai Sabaya kwa kutumia perfume ya sumu kwa madai kuwa Sabaya alikuwa anatishia nafasi ya Mbowe kuendelea kuwa mbunge wa jimbo la Hai.

====
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai akisoma maelezo ya mshtakiwa wa pili katika kesi ya uhujumu uchumi, Adam Kasekwa amesema mtuhumiwa huyo alisema Freeman Mbowe alipanga kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Katika ushahidi alioutoa leo, Oktoba 26, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Kingai amesoma maelezo ya mtuhumiwa huyo kwamba Mbowe alisema Sabaya anahatarisha nafasi yake ya kuendelea kuwa mbunge wa Hai.

Ifuatayo ni sehemu ya maelezo ya mshtakiwa Adamu kama yalivyosomwa na RPC Kingai:

“Mbowe alituelekeza tufuatilie nyendo zake na tumdhuru kwa spray ya sumu. Ling'wenya alifuatilia mtu wa kupata sumu. Tarehe 27 tulirudi Dar na magari mawili pamoja na Mbowe na mlinzi wake.

“Baada ya kufika Dar tulifikishwa Mikocheni mimi na Ling'wenya tulipewa Sh200,000 tujiandae.Baadaye tulipewa nauli turudi Moshi. Agosti Mosi saa 11 alfajiri Mbowe alituita akasema tutekeleze maelekezo ya kumdhuru Sabaya.

“Akituonesha picha ya Sabaya na maeneo anauyopenda kutembelea. Alituelekeza baada ya kazi ya Sabaya turudi Dar kutekeleza kazi nyingine nyeti kulipua vituo vya mafuta na kushinikiza maandamano ili Serikaki ionekane imeshindwa maana inatuchukia sisi wapinzani.

“Yeye aliondoka kurudi Dar sisi tukabaki kutekeleza kumdhuru Sabaya Tarehe 3 Atosti tulienda eneo la Rao Madukani kwa dada yake Ling'wenya ili kubana matumizi maana Mheshimiwa alituachia Sh150,000

“Tulikamatwa na askari tukituhumiwa kukutwa na dawa za kulevya na kupanga njama za ugaidi. Tuhuma hizo ni za kweli na pia kukutwa na silaha ni za kweli na nilikutwa na simu yangu ya Itel.

“Nilisaini hati ya kuchukuliwa mali na askari nao wakasaini. Nikachukuliwa kwenda Central Moshi. Uthibitisho haya maelezo ni ya kweli kwa saini.

“Muda wa kumaliza kuandika maelezo hayo ilkiuwa ni saa 3"

Wakili wa Serikali Mwandamizi SSA Kidando alimtaka ACP Kingai aelezee alichoelezwa na mshtakiwa huyo wa pili Adamu.

ACP Kingai :Alikiri kukutana na wenzake kwa ajili kwenda kwa Mbowe, alikiri kupewa nauli kwenda Moshi kukutana na Mbowe, alikiri kuwepo Moshi tarehe 24 -26 Julai 2020, alikiri kuwepo yeye na wenzake wawili akiwemo Ling'wenya na mtu mwingine.

“Alikiri tarehe 25 usiku kufanya mkutano yeye na Ling'wenya, Moses Lujenje maarufu Kakobe, Hassan Bwire na Freeman Mbowe"

SSA Kidando: Nini kiliendelea?

ACP Kingai : Alikiri kwenye mkutano alielekezwa na Mbowe kumdhuru DC Sabaya kwa njia yoyote ile.

SSA Kidando: Kitu gani kingine alikueleza?

ACP Kingai: Shahidi pia alikiri kupewa pesa na Mbowe Sh150,000 kukidhi mahitaji hapo Moshi, alikiri Agosti Mosi 2020 alfajiri Mbowe aliwaita tena na kuwapa maelekezo, kwamba wahakikishe wanayafanyia kazi.

“Kumdhuru Sabaya na ili wawe na uhakika Mbowe aliwaonyesha picha ya Sabaya kupitia simu yake, aliwalekeza wamalize kazi hiyo ya Moshi halafu warudi Dar kufanya kazi nyingine nyeti.

“Alitaja kazi hiyo kwamba walipanga wakalipue vituo vya mafuta, lakini pia kufanya vurugu kwenye masoko na maeno ya watu wengi”.
 
Jeshi lilifukuza mtu mwenye ugonjwa wa akili

Maana yake hata Kama maelezo aliyoyatoa hakuteswa kuyatoa lakini Ni chizi hivyo maelezo yake hayana ukweli wowote.

Mtu chizi anawezaje kutoa maelezo?

Halafu sabaya Mahakama imeshaonyesha Ni jambazi! Kuna kosa gani kwangu Mimi kumuua jambazi ambaye ananifatilia mpaka kwenye hotel yangu kuniua?.

Hapa hakuna kesi ya ugaidi Ni porojo tu
 
RPC Kingai ameeleza hatua kwa hatua bila kuacha shaka jinsi Freeman Mbowe alivyopanga kumuuwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Ole Lengai Sabaya kwa kutumia perfume ya sumu kwa madai kuwa Sabaya alikuwa anatishia nafasi ya Mbowe kuendelea kuwa mbunge wa jimbo la Hai.

Umejitahidi kweli kweli kuripoti
 
RPC Kingai ameeleza hatua kwa hatua bila kuacha shaka jinsi Freeman Mbowe alivyopanga kumuuwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Ole Lengai Sabaya kwa kutumia perfume ya sumu kwa madai kuwa Sabaya alikuwa anatishia nafasi ya Mbowe kuendelea kuwa mbunge wa jimbo la Hai.

sawa TU. ILA TUJUA TU UKWELI
 
Aaaa,Kama sio kudharirishana hii ndio Nini sasa?
* Nikaue mtu Hai
+ Nikakate miti iringa
*Nikachome vituo vya mafuta morogoro
Malipo 150,000/= watu wawili!
Mbona haingii akilini kwa muandika maelezo hata kwa mtoa maelezo pia, au nyinyi mnaonaje ndugu zangu.
Maana Mimi ninavyo jua hata kwa wale wazee wa Robbin hood za macho mekundu kule Shinyanga huwa nasikia wanapewa mpaka maksai 5 x 700,000/=
Makomandoo 75.000/= kazi 3 za kigaidi?
Akili yangu inakataa hata mzee wa Robbin hood hawaezi kubari hiyo biashara.
 
Muendelezo wa kesi vipi update mbona haziji tena
 
Aaaa,Kama sio kudharirishana hii ndio Nini sasa?
* Nikaue mtu Hai
+ Nikakate miti iringa
*Nikachome vituo vya mafuta morogoro
Malipo 150,000/= watu wawili!
Mbona haingii akilini kwa muandika maelezo hata kwa mtoa maelezo pia, au nyinyi mnaonaje ndugu zangu.
Maana Mimi ninavyo jua hata kwa wale wazee wa Robbin hood za macho mekundu kule Shinyanga huwa nasikia wanapewa mpaka maksai 5 x 700,000/=
Makomandoo 75.000/= kazi 3 za kigaidi?
Akili yangu inakataa hata mzee wa Robbin hood hawaezi kubari hiyo biashara.
Kesi ya kipumbavu kabisa
 
Bado najiuliza, ili ugaidi ufanyike kuna namna mbili..

Lazima wahusika kwa maana ya watekeleza ugaidi wawe employed kwa malipo fulani, SIJAONA POPOTE PANAPOONYESHA MALIPO YAO YA KAZI AU MAKUBALIANO YA MALIPO..

wahusika wa ugaidi wanakuwa ni waumini wa ideology fulani, wanakuwa wamejitolea kufa kwa ajili ya itikadi yao ambayo hapa ni CDM... HAKUNA NILIPOONA HAWA WALIKUWA WANACHAMA WA CDM AU WANA KADI YA UANACHAMA WA CDM AU KUNA MAHALA WALIKAA KWA MUDA KUWA BRAINWASHED..

sasa ugaidi huo walikuwa wanautekeleza kwa namna ipi...
 
Tayari baadhi ya Wadau wa Maendeleo, akiwemo Mwakilishi wa Ubalozi wa Canada wamewasili Mahakamani.


Hadi saa 3:30 asubuhi hii Watuhumiwa walikuwa bado hawajaletwa Mahakamani.

====

Hatimaye Mbowe na wenzake wameletwa Mahakamani

Jaji Joachim Tiganga ameingia Mahakamani

Wakili wa serikali Robert Kidando anatambulisha Jopo lake
1. Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulumanywa Majigo
6. Jenitreza Kitali

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo Lake
1. Peter kibatala
2. Jeremiah Mtobesya
3. Michael Mwangasa
4. Nashon Nkungu
5. Dickson Matata
6. Alex Massaba
7. Jonathan Mndeme
8. Hadija Aron 9.
Idd Msawanga

Jaji anaomba Kuwaona Washitakiwa wote 1,2,3 na 4

Wanainuka Kwa kutajwa kwa Namba

Wakili wa Serikali anaomba kesi Kuendelea na Shahidi yupo tayari Lakini Kabla ya Kuendelea anaomba kufuatilia kuhusiana mabadiriko yaliyopalekea mpaka Mheshimiwa Jaji Kuja mwingine kwa mujibu ya kifungu cha 299 CPA (Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai).

JAJI: Upande wa utetezi

Peter Kibatala: hatotatumia Haki ya kumuita tena Shahidi kwa kesi Inayoendelea hapa.

Jaji anaandika.

JAJI: wote mnafahamu na mlikwepo siku ya tarehe 20 mwezi huu na Jaji aliyekuwepo alielekeza Jaji Mwingine atakuja kuendelea na Kesi hii, Na Jaji Mwingine Ndiyo Mimi, kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 Kifungu cha 299.

JAJI: Kwamba Upande wa Utetezi Mnahaki ya a Kumuita tena shahidi kwa kuwa Mmesema hamna nia nitawaruhusu Upande wa Jamhuri Kumuita sasa Shahidi wao tuweze Kuendelea. Mawakili wote Wanainuka ishara ya Kukubaliana na Uamuzi wa Jaji na Kupokea Maelekezo ya Mahakama.

Wakili wa Serikali anatoka Kwenda Kumuita Shahidi wa leo.

Mahakama ipo Kimya

ACP KINGAI anaingia na Kupanda Kizimbani.

Robert Kidando Wakili wa Serikali anamtaarifu Jaji Kuwa Shahidi amefika.

JAJI: Majina yako Tafadhali

SHAHIDI: ACP Ramadhan Kingai

JAJI: Unakumbuka Uliwahi Kufika Mahakamani, ukaapishwa kutoa Ushahidi, Mahakama inakukumbusha Upo chini ya Kiapo hicho. SHAHIDI: sawa Mheshimiwa

JAJI: Mtakumbuka Mawakili kuwa Siku ya Tarehe 20 Jaji alipokea Kielelezo, baada ya Kupokelewa Kinatakiwa Kusomwa Mahakamani. Naomba Kuanzia hapo Shahidi akabidhiwe Kielelezo aweze Kusoma Kielelezo.

WAKILI WA SERIKALI: Soma Sasa Kielelezo Kuanzia kurasa ya kwanza.

SHAHIDI: Adama Kasekwa anaishi Chalinze Maelezo ya Onyo Chini kifungu cha Sheria ya Makosa ya Jinai Sura ya 20. MIMI kingai nakuonya wewe Adam Kasekwa

SHAHIDI: Ulazimishwi kusema lolote Pia unaweza Kualika Ndugu, Jamaa au Mwanasheria Kushuhudia utoajo wako Maelezo. Mtuhumiwa akasaini na Mimi nikasaini.

MAJIBU YA ONYO

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo..

MIMI Adam Kasekwa anaonya na Kingai Chini ya Kifungu cha 24 cha Sheria Mwenendo wa Makosa ya Jinai Silazimishwi na yoyote Kutoa Maelezo yangu. Je, Upo tayari Kutoa Maelezo Yako.

Jibu, Ndiyo Nipo tayari.

Shahidi anasoma kielelezo: Maelezo yamechukuliwa Katika Ofisi ya RCO ilala MIMI Adam Kasekwa Nimezaliwa Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Ileje... Mwaka 2011 nilijiunga na Recruting Maktopora. Nikachaguliwa Kujiung na Mafunzo Ukomando 92KJ.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Mwaka 2014 niliteukiwa kwenda kituo cha Msangani Kujifunza ulinzi, amani na nikachaguliwa Kwenda DR Congo. Mwaka 2017 nilimaliza Mkataba na kurejea Nilipata malipo na Kumuoa Mke wangu Lilian ambaye naishi naye Mpaka Leo.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Nimepata naye Mtoto Mmoja. Nilirudi nikaa Miezi 6 kazini Nikaugua Ugonjwa wa aKili Nikaachishwa kazi na kulipwa mafao ya Millioni 4 na Laki 6.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Je unamfahamu Luteni Denis? Ndiyo, nilikuwa Mkinga Mawasiliano hayapatikani. Niliporudi nikaambiwa mwenzangu ananitafuta.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Niliporudi nyumbani nilimpigia Simu Mwenzangu Mohammed Ling'wenya Kwamba Kuna kazi ya VIP protection. Akaniambia inabidi twende Morogoro Kumuona Luteni Urio. Tulipoenda akatuambia Kuna kazi ya VIP protection ya kumlinda Freeman Mbowe

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Akatupatia TSh 21,000 nauli ya Kwenda Moshi. Siku hiyo hiyo tulirudi Chalinze na kuanza Safari ya kwenda Moshi Tulipokelewa na Dereva wake anayeitwa Willy Alitupokea na Pick Up Nyeupe yenye maandishi ya M4C.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Tukaenda Mpaka Kwenye Hotel Ya Mheshimiwa Mbowe Huko tulimkuta Khalfani Bwire aliyetutambulisha kwa Mbowe, "Mkuu wale Vijana tuliowaagiza ndiyo hawa hapa." MBOWE akatueleza Kuwa Sabaya anamvuruga sana na anamvuruga wapiga Kura.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Kwamba anawatisha Wapiga kura wake kiasi cha Kuhatarisha Kurudi kwake. Na kwamba, akatuelekeza tumdhuru Kwa Njia yoyote. Akatuelekeza Maeneo yake ya Moshi na Arusha.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Tulipanga kumdhuru kwa Spray Spray ya sumu alitafuta Mohammed Ling'wenya

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Siku inayofuata tulikuwa Mimi na Mohammed na wanachana wawili siwakumbuki Majina Baada ya Kufika Dar es Salaam Tulimfikisha Mheshimiwa Mbowe Nyumbani

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Akatukabidhi TSh Laki 2 kwaaajili ya Kununua Nguo. Kwa sababu Kesho yake tulikuwa tunampokea Mheshimiwa Lissu. Na Siku ya tarehe 27 Julai Mbowe alitutumia Kila moja TSh 78 Elfu ya Nauli Ya Kwenda Moshi.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: SIKU ya Tarehe 01 August Tulienda Moshi Tukamkuta Mbowe akiwa na Khalfani Bwire Akatuelekeza Kuwa tufanye ile kazi yake Haraka Akatuelekeza Maeneo anayokaa Sabaya kama vile Milestone PIA Akatuelekeza Tuje DSM, Kuchoma Vituo Vya Mafuta.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Kwamba yeye anatachochea maandamano ILi Serikali ionekane Imeshindwa Kuandaa Uchaguzi. Tulienda Maeneo ya Boma Ng'ombe Njia ya kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kumfuatilia.

Siku ya terehe 03 tulienda Maeneo ya RAU madukani kwa ajili ya kubana Matumizi. Kwa sababu Mheshimiwa alituachia Pesa Laki Moja na Nusu kwa ajili ya kukaa, isingetosha. Tulienda Kukaa kwa Dada yake kukaa kwaajili ya Kubana Matumizi.

Swala la Kupanga Ugaidi ni la kweli Na swala la a kukutwa na Silaha ni la kweli Wakati Polisi wananikamata pia walinikuta na Heroine Baada ya kuchukua Vitu hivyo Askari walisaini na Mimi nikasaini na Polisi walichukua Vitu hivyo kwenda Central

Baada ya Maelezo hayo Adam Kasekwa akasaini Na Mimi Kingai nikasaini Baada ya Kuchukua Maelezo hayo Muda ulikuwa ni saaa tatu.

Wakili wa Serikali: ACP Kingai Kutokana na Maelezo uliyoyasoma hapa mahakamani Yeye alikuelza nini Kutokana na Maelezo Uliyoyasoma Mahakamani Shahidi: alikiri kuwa anamfahamu Luteni Urio. Alikiri Kupewa Maelekezo ya kazi kutoka kwa Mheshimiwa Mbowe

Shahidi: Alikiri Pia alipewa Maelekezo ya kazi Kutoka akwa Mbowe Kupitia Kwa Luteni Deni Urio. Alikiri Pia kuwapo Moshi tarehe 24 Mwezi wa 07, 2020

Shahidi: Alikiri Pia kuwapo Moshi na wenzake Mohammed Ling'wenya na Mwenzake aliyemtaja Kwa Jina la Kakobe. Baada ya Ufutailiaji tukamfahamu ni Moses Lijenje. Alikiri Pia kufanya Mkutano yeye na wenzake wanne.

Yeye Mwenyewe, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya, Moses Lijenje (Aliyemtaja Kwa Jina la Kakobe) Khalfani Bwire na Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: kwa Mujibu wa Mkutano huo nini kiliendelea. Shahidi: Mbowe alitoa Maelezo kuwa Sabaya anamfanyia Vurugu, (Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai)

Wakili wa Serikali: kitu gani Kingine alikueleza Shahidi: Mtuhumiwa alikiri Kupewa Pesa 150,000/= kukidhi Mahitaji kipindi watakapokuwa hapo Moshi.

Wakili wa Serikali: tueleze Shahidi kuhusiana na kilichofuata Shahidi: Alikiri Kuwa Siku ya Tarehe 01 Mwezi wa Nane saa 11 Alfajiri kabla ya Safari ya Kuja DAR ES SALAAM Aliwaelekeza wamdhuru Ole Sabaya.

Shahidi: Akawaonyesha Picha ya Ole Sabaya Kupitia Simu yake ya mkononi Aliwapa Maelekezo Kufanya kazi hiyo na Kwamba baada ya hapo atawataka warudi Dar es Salaam. Alipanga kuwapa kazi ya kwenda Kulipua Vituo Vya Mafuta. Alipanga kufanya Vurugu kwenye masoko.

Mtobesya: OBJECTION Naomba Shahidi ajielekeze Kwenye kikichoandikwa kwenye Statement Mambo ya Kituo cha Mafuta na Masoko havijatajwa.

Jaji: Kwahiyo a some?

Mtobesya: ajielekeze kikichoandikwa hata kama ana Rudia Kuelezea, Sheria inasema Statement itajielezea Yenyewe.

JAJI: Upande wa Mashitaka

Wakili wa Serikali: Sahihi Mheshimiwa tutarekebisha.

Wakili wa Serikali: Alikueleza Lengo ilikuwa ni nini

Shahidi: Lengo ni Serikal ionekane imefeli Alikiri Pia kukamatwa na Polisi Siku ya tarehe 05 Mwezi wa 08, 2020 akiwa Rau Madukani.

Alikiri Pia kukamatwa na Pistol aina ya Ruvern ikiwa na Risasi 03.

Shahidi ACP KINGAI: Alikiri kukamatwa na Kete 58 za Madawa aina ya Heroine.

Wakili wa Serikali: baada ya kuwa umeandika Maelezo hayo, yeye ulimpeleka wapi kwa Siku hiyo.

Shahidi ACP KINGAI: ilikuwa Siku ya tarehe 07 Mwezi wa 08, 2020 nilimrudisha Mahabusu.

Wakili wa Serikali: Shughuli gani Nyingine ili endelea baada ya Shughuli hii

Shahidi ACP KINGAI: tuliendelea na Upelelezi ya Kuwatafuta watuhumiwa wengine. Maeneo ya Chang'ombe tulimkamata Khalfani Bwire.

Wakili wa Serikali: Kwa tuhuma Gani

Shahidi ACP KINGAI: Kwa tuhuma hizi hizi za Kula Njama kutenda Matendo ya Ugaidi.

Wakili wa Serikali: nini kiliendelea

Shahidi ACP KINGAI: nikimtaka Khalfani Bwire aandike Maelezo yake

Wakili wa Serikali: elezea Kuhusu Kumkamata kwake

Shahidi ACP KINGAI: baada ya a kuwasiliana na Askari aliyekuwa kwenye Pointi akiwa kwenye gari, tukielekeza Gari iingie Kituo cha polisi Chang'ombe. Tukawa tumeingia pale na Inspector Mahita na ASP Jumamne.

Jaji: ASP nani? Shahidi: Jumanne

Wakili wa Serikali: baada ya Kumkamata Mlimpeleka wapi

Shahidi: tuliekeza Superitendent Lukangira wa hapo hapo Chang'ombe. Hii ni baada ya Mtuhumiwa kutuelekeza hana Makazi hapa Dar es Salaam ni Mkazi wa Ngerengere.

Wakili wa Serikali: Nia ya Kuuliza kwake ni wapi ilikuwa ni ya nini

Shahidi: nia ilikuwa kufanikisha Shughuli za kiupepelezi

Wakili wa Serikali: baada ya Lukagingira kuandika Maelezo yake nini Kilifuata

Shahidi: Tukawa tunaendelea Kufuatilia Makazi yake, Tofauti na Taarifa alivyokuwa ametoa yeye kwakuwa tulijua haiwezekani awe kila Siku anaenda Ngerengere.

Wakili wa Serikali: Wakati Unapata Taarifa ana makazi Wilaya ya Temeke, elezea Sasa Maelezo yalikuwa yanaandikiwa wapi

Shahidi: Maelezo yalikuwa yanachukuliwa Kituo cha Polisi Chang'ombe na Mimi niliweka Bass Central polisi (Ilala).

Wakili wa Serikali: baada ya Kutoa Maelekezo Hatua Kuchukua Maelezo Isimame, nini kilifuata

Shahidi: tulipata Taarifa Mtuhumiwa anakaa Temeke Makangarawe, Tuliungana na Detective John wa Temeke na RCO kwa ajili ya kwenda Kumpekua Makazi yake.

Wakili wa Serikali: Mlienda sehemu ipi haswa huko Mkangarawe

Shahidi: Ule Mtaa Jina Limenitoka

Wakili wa Serikali: Uliwezaje Kuutambua sasa

Shahidi: tukielekezwa na Watu hadi Nyumba alipokuwa amepanga Mtuhumiwa.

Wakili wa Serikali: Elezea sasa hiyo Shughuli ilifanyikaje na Khalfani Bwire alikuwa wapi.

Shahidi: Tuliongozana na Mtuhumiwa, Tukamtafuta Mwenyekiti wa Ule mtaa, Tukamkuta na Mwenye nyumba aliyempangisha Khalfani Bwire na hata Mke wake alikwepo.

Wakili wa Serikali: huyu Mwenyekiti ni wanini?

Shahidi: Ni Mwenyekiti wa Mtaa

Wakili wa Serikali: Nini Kilifuata

Shahidi: Nilimuelekeza ASP Jumanne Kwa Kushirikiana na Detective John Kutoka Ofisi ya RCO Temeke na kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Mtaa na hata Mke wake.

Wakili wa Serikali: Elezea sasa Katika Upekuzi huo Mlikuta nini?

Shahidi: Vitu mbalimbali vilipatikana kama Uniforms za JWTZ, Masharti ya JWTZ, Tshirt za JWZT, name tags za kwake za JWTZ.

Wakili wa Serikali: baada ya Kupata Uniforms na Vifaa Mbalimbali nini Kilifanyika baada ya Kupata Vitu hivyo.

Shahidi: Viliorodheshwa katika Hati ya Uchukuaji Mali. Wakati wa Upekuzi tulikuta Kidaftari kilichokuwa na Ramani na Majina ya Vituo Vya Mafuta.

Wakili wa Serikali: baada ya kuorodhesha kitu gani kilifanyika

Shahidi: baada ya Kuwa Viliorodheshwa yaliandikwa Majina ya walioshuhudia Upekuzi huo. Pia wakasaini Hati ya Uchukuaji Mali. Mtuhumiwa pia alisaini Hati ya Uchukuaji Mali na aliyepekua alisaini Hati hiyo.

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukamilisha Hati ya Uchukuaji Mali, Kitu gani Kiliendelea

Shahidi: Nilikuwa nimeelekeza Mashahidi walioshuhudia waandikwe Maelezo pale pale

Wakili wa Serikali: baada ya Kukamilisha

Shahidi: Tulichukua Vitu tulivyo orodhesha na Mtuhumiwa akarudishwa a kituo Cha Polisi.

Wakili wa Serikali: Kituo gani cha Polisi Shahidi: Chang'ombe

Wakili wa Serikali: Baada ya kumrudisha Kituo cha Polisi Chang'ombe Kitu gani pia Kiliendelea.

Shahidi: Mtuhumiwa tulimkamata na Kidaftari chenye Ramani ya Vituo Vya Mafuta Dar es salaam, Soko la Kilombero Arusha.

Tukachukua Sampuli za Miandiko ya Watuhumiwa wote. Lakini pia tuliendelea na hatua ya kuwatafuta watuhumiwa wengine

Wakili wa Serikali: watuhumiwa gani wengine Mlikuwa mnawatafuta

Shahidi: Watuhumiwa wengine tuliokuwa tunawafutilia ni Mtu alikuwa anaitwa Gabriel, Lijenje, Malima, Khalid na Jamaa Mmoja anaitwa Kaaya.

Wakili wa Serikali: nini hatima ya hao mliokuwa mnawafuatilia

Shahidi: Ukimuondoa Mtu Mmoja anaitwa Malima, Watuhumiwa wote walifikishwa mahakamani.

Wakili wa Serikali: vipi kuhusu moses Lijenje Shahidi: bado hatujafanikiwa Kumpata

Wakili wa Serikali: Hapa Mahakamani kuna Washitakiwa Wanne inakuwa je hao wengine hawapo Mahakamani kama Walifumgukiwa Mashitaka

Shahidi: walifutiwa Mashitaka baada ya Kuonekana Ushahidi hakuwa wakutosha ukilinganisha na wenzao.

Wakili wa Serikali: ACP kingai katika Ushahidi wako tangu Mwanzoni umezungumzia kukamatwa Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Khalfani Bwire Vipi ukamatwaji wake Mshitakiwa wa Nne.

Shahidi: Freeman Mbowe alikamatwa 21 July 2020 akiwa Mwanza

Wakili wa Serikali: Kwa tuhuma gani

Shahidi: Kwa tuhuma hizi hizi

Wakili wa Serikali: Wakati Unatoa Ushahidi wako Ulizungumzia kukamatwa hawa wengine Mwaka 2020 na huyu 2021 elezea Ilikuwa je hapa Mahakamani.

Shahidi: Tulikuwa tunajirishisha haswa uhusika wake. Tulikuwa bado tunaendelea Kufuatilia mawasiliano Na Uchunguzi wa Forensic ambao ulikuwa unahusiana na Shauri hili

Wakili wa Serikali: Sababu ukamataji ulifanyika 21 July Mwaka 2020, ni lini taarifa zilifahamika rasmi.

Shahidi: Zilifahamika Mwanzoni July 2020

Wakili wa Serikali: wakati anakamatwa Upelelezi ulikuwa umefikia Hatua gani

Shahidi: Upelelezi wetu kwa muda huo tunamkamata ulikuwa umekamilika.

Wakili wa Serikali: Upelelezi wa aina gani ulikuwa unaendelea kwa Mshitakiwa nne

Shahidi: Tulifanya Forensic na Divices za Kieletronic tuliokuwa tunafuatilia Kujiridhisha dhidi yake na Tuhuma zilizokuwa zinamkabili.

Wakili wa Serikali: wakati Unatoa Ushahidi wako Mwanzoni ulisema Ulielezea Kuwa Umelekeza kufungua Jalada la Tuhuma za Kigaidi.

Shahidi: Kulingana na Taarifa ambazo tulikuwa tumezipata kwa Luteni Urio na aina Ya Vitendo vilivyokuwa Vimepangwa na Watuhumiwa Ilikuwa ni Kudhuru Viongozi wa Serikali, kufanya Vurugu sehemu zenye watu wengi, Kulipua Vituo Vya Mafuta, Hata Miti kwenye highway kukatwa Kuzuiwa Magari yasipite, Hasa katika Barabara ya Morogoro kwenda Iringa.

Wakili wa Serikali: Ukatafsiri ni Vitendo gani

Shahidi: Vitendo vyenye kuleta hofu kwa Wanachi Kujiona hawapo salama, Ni Vitendo vinavyoleta Tafsiri la Shitaka la Ugaidi

Wakili wa Serikali: ulisema katika Taarifa ya Luteni Urio ulisema walipanga Kuonyesha kuwa Nchi haitawaliki.

Mtobesya: OBJECTION kaka yangu Wakili Msomi ajielekeze Kwenye fact siyo Opinion Maana huyo ni Shahidi wa Fact, He is doing too Much Sasa Maana Mwanzo tulijua ameteleza.

Wakili wa Serikali: Sawa Mheshimiwa Jaji nitaomba nijielekeze sawa Sasa.

Wakili wa serikali: Vitendo hivi vilipangwa Vifanyike wapi

Shahidi: Mwanza, Moshi, Dar es Salaam na Arusha

Wakili wa Serikali: Vilikuwa Vifanyike Lini

Shahidi: Kabla ya Uchaguzi wa Mwaka Jana

Wakili wa Serikali: ni hayo tu Kwa sasa Mheshimiwa Jaji

Jaji: Upande wa utetezi

Mtobesya: Asante Mheshimiwa Jaji nitaomba niendelee kwa Niaba ya Mshitakiwa wa kwanza.

Mtobesya: ni sahihi Shahidi wewe ulikuwa ni sehemu ya waliokuwa wanahusika na upelelezi wa Kesi hii

Shahidi: ni sahihi

Mtobesya: ni sahihi kuwa Baada ya kupokea Maelezo kwa DCI BOAZI mkafungua Jalada

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji ni lini Mlifungua Jalada

Shahidi: Yalikuwa Majalada Mawili la upelelezi na Kesi

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Lilifunguliwa Jalada la Uchunguzi

Mtobesya: Uchunguzi au Upelelezi

Shahidi: yote ni yale yele labda useme unataka Jalada gani

Mtobesya: wewe Ndiye unayetoa Ushahidi

Shahidi: Sawa Mwanzo Lilifumguliwa Jalada la Uchunguzi wa Kula njama. Ilikuwa July Mwaka Jana.

Mtobesya: yote Mawili Mlifungua kwa Pamoja au Tofauti

Shahidi: Kuna Utaratibu wa Kiupelelezi labda kwa sababu ujawa mpelelezi Ndiyo Maana Unahangaika Kuna Jalada la Awali la Uchunguzi lakini unapopata Taarifa unafungua Jalada la Kesi ya kula njama Lilifunguliwa na Mkaguzi wa Polisi Msaidizi anaitwa Swila

MTOBESYA: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kabla hamjawakamata Watuhumiwa Mlikuwa mmekusanya Taarifa zipi kwa wakati huo

Shahidi: Taarifa za kutaka kuwadhuru Viongozi wa Serikali, Kufanya Maandamano ya siyo na Kikomo, Taarifa za Kukata Miti na Kufanya Uporaji Magari yasipite na Kutaka Nchi isitawarike

MTOBESYA: kwa hiyo hizo Taarifa ndiyo zilitengeneza Kosa la Kula Njama

Shahidi: Sahihi

Mtobesya: Mwambie Mheshimiwa Jaji hizo Taarifa Mlizipata kabla au Baada ya Kumchukua Maelezo Mshitakiwa wa Pili

Shahidi: Kabla

MTOBESYA: kabla ya Kesi Ndogo unakumbuka ulisema Urio aliwapatia Taarifa kuwa Vijana wamepatikana, Unakumbuka ulisema tarehe Ngapi.

Shahidi: Ilikuwa tarehe 04 Mwezi wa Saba Mwaka Jana

MTOBESYA: wakati unaelezea (Kusoma) unakumbuka Kielelezo ulipata wasaa wakujua Urio alishiriki Vipi katika swala hili?

Shahidi: sijaelewa Vizuri

MTOBESYA: Statement hii ambayo unasema uliandika unakumbuka Urio alishiriki namna gani?

Shahidi: naomba Jaji anisomee anapoparejea

Jaji: labda tuweke, Ushiriki wa urio ulikuwa Vipi

Shahidi: Urio ameshiriki kwa kuwatafuta Vijana, ameshiriki kuwapatia nauli na ameshiriki Kutafuta Vijana waliofukuzwa Jeshi

Mtobesya: Umesema kwenye Maelezo alifanya hayo Tarehe ngapi

Shahidi: Sikumbuki tarehe

MTOBESYA: sasa nije kwenye Maelezo uliyoyachukua, kwa ajili ya Kumbukumbu Unakubaliana na Mimi Kuwa kuna namna tatu za Kuchukuliwa Maelezo. moja, Kwa Anateyetaka Kuchukuliwa Maelezo kuomba Karatasi na kalamu na kuandika Mwenyewe. Pili, kwa anayehojiwa kuongozwa Tatu, kwa njia ya Maswali na Majibu Wewe ukichagua Njia gani?

Shahidi: Mimi nilitumia Maswali na Majibu

Mtobesya: naomba niishie hapa

Wakili Malya: naomba Kielelezo (Statement) Mahakama inampatia John Malya

Wakili Malya: Unasimu ya mkononi

Shahidi: Ndiyo

Wakili Malya: unaweza kututajia EMEI namba ya Simu yako

Shahidi: Hapana Siwezi

Wakili Malya: kwanini..?

Shahidi: Sijaamua kuishika

Wakili Malya: Una ya mtu yoyote wa Karibu yako unayoikumbuka

Shahidi: Hapana

Wakili Malya: sasa Katika maelezo Adam alikutajia EMEI namba Kutoka wapi

Shahidi: Alikuwa na kikaratasi

Wakili Malya: Ulizungumza kwamba Mshtakiwa alikuwa na kikaratasi?

Shahidi: Sikuzungumza

Wakili Malya: ni sahihi unapoandika Maelezo unaandika kwa usahihi kabisa

Shahidi: Sahihi Kabisa

Wakili Malya: kwa uelewa wako Unapotaja Sheria, kwa Mbele Mwaka Unatajwa, Maana ya Kuwa na Miaka katika Sheria.

Shahidi: Mimi siyo Mwanasheria

Wakili Malya: Nafahamu wewe siyo Mwanasheria ila Umeandika Mwenyewe Vifungu Vya Sheria ili Mtu ajue Haki yake

Shahidi: Ndiyo nafahamu. Sasa Unatoa somo

Wakili Malya: Kwa hiyo wewe Unaweza kuandika Mwaka wowote tu.

Shahidi: am not aware of It

Wakili Malya: kwa hiyo wewe Unaweza Kuandika Sheria na Mwaka ukaweka Wowote tu

Shahidi: Hapana naweka na Sheria

Wakili Malya: na Mwaka kama imefanyika amendment Zake? Sasa Kwa Maelezo hayo uliyoyashika Tusomee hapa.

Shahidi: Cap 20 REV 2018

Wakili Malya: sasa hiyo Sheria Hakuna. Wewe umechukua Maelezo ya Onyo kwa Sheria ambayo haipo, Unasemaje kwa hilo

Shahidi: Hiyo ni Typing Error kwa sababu imechapwa. Ile niliyoandika kwa Mkono wangu huenda sikuandika hivi.

WAKILI mallya: wakati unaisoma hapa Mahakamani Ulisema hapa kwamba hii siyo au ulikariri ukawa unaisoma tu Hapa

Shahidi: kwenye eneo hili Onyo Chini ya Kifungu Cap Rev 2002 badala Ya kusomeka 2018.

Wakili Malya: kwa hiyo ulipaswa Kusomeka Vinginevyo siyo hiyo

Shahidi: Ndiyo

MALYA: ushawahi Kusikia Kiongozi wa Polisi Liberatus Barrow aliuwawa

Shahidi: Ndiyo Wakili Malya: aliuwawa?

Shahidi: Ndiyo WAKILI

Mallya: waliomuua Walikamatwa Ndiyo

Shahidi: Ndiyo

WAKILI mallya: walishitakiwa na Makosa gani?

SHAHIDI: mauaji

WAKILI mallya: Lakini Kumdhuru Sabaya ni Ugaidi?

Shahidi: kuleta Vurugu kwenye Masoko, Kukata Miti Barabara, Kuzia Magari yasipite ni Vitendo vingeleta hofu na Wasiwasi Vitendo hivi Vinaashiria ni Vitendo Vya Ugaidi.

Wakili Mallya: umerudi Viongozi sana Ukimtoa lengai Ole Sabaya Kiongozi Mwingine nani..?

Shahidi: ni Maelezo ya Adam Kasekwa, Siyo ya kwangu

Wakili Mallya: ulipomkamatia Adamoo Moshi na Kilichokufanya usichukue Maelezo Moshi ni sababu zipi

Shahidi: Sababu za Kiupelelezi

Mallya: wakati Unatoka Moshi ulipitia Njia ipi ya Chalinze au Bagamoyo

Shahidi: Msata

Mallya: ulitoka Msata kwenda Central Njia kuna Mbweni na Oysterbay kwanini uliamua kwenda Central

Shahidi: Sababu za Maelezo na Pili Ndipo kesi ilipofunguliwa

Wakili Mallya: Wewe kwa sasa ni RPC KINONDONI Je unafahamu kuwa Kinondoni inajitegemea

Shahidi: Ndiyo, zikiwa Chini ya Kanda Maalum Dar es Salaam

Wakili Mallya: ulieza Mahakama Kwanini Huyu achukuliwe Maelezo Temeke Mkoa Mwingine wa Kipolisi na kwanini hakusafirishwa kama wenzie kuja Mkoa wa Ilala

Shahidi: Hapana sikueleza

Wakili Mallya: umesema Yalifunguliwa Majalada mawili

Shahidi: Ndiyo

Wakili Mallya: nani alifungua hayo Majalada Shahidi: Inspector swila

Wakili Mallya: Umemtaja Sabaya, Alikuwa Mkuu wa Wilaya wa wapi Vile?

Shahidi: Hai

Wakili Mallya: je pale Hai Pana Ofisi ya Mkuu wa upelelezi?

Shahidi: Ndiyo

WAKILI: mallya Je Kilimanjaro Kuna Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi?

Shahidi: Ndiyo

Wakili Mallya: Ni hayo tu

JAJI: naomba Tubreak Kwa Lisa limoja Tutarudi hapa Saa 7 na Dakika 20

Jaji anatoka

Mpaka sasa saa saba na nusu, Jaji hajaingia.

Mahakama imerejea

Wakili Robert Kidando anaomba Kumtambulisha Wakili Nasorro Katuga

Jaji: nilipo Break tulikuwa tumemaliza Maswali ya Dodoso ya Wakili wa Mshitakiwa wa Pili, Nipo sahihi..? Wawakili wa Pande zote Mbili wanaitikia, NDIYO

Jaji: namruhusu Wakili wa Mshtakiwa wa tatu aendelee, WAKILI MATATA
Lissu naye angekuwepo apige maswali ya kutosha mpaka ajinyee huyu mzee mpuuzi
 
Hii kesi ipo very technical kwenye baadhi ya maeneo shahidi aliposema alifukuzwa kazi kwa sababu za ugonjwa wa kichaa upande wa utetezi wajitahidi wapate hicho kielelezo waje wakitumie kwenye utetezi

kwa kuwa plan A ya kupinga kielelezo imeshindikana basi plan B wakati wa utetezi wajielekeze kwenye mental status ya mtuhumiwa wakati anahojiwa.

manake kwa kichaa kama huyu wakati anahojiwa hakuna uthibitisho wa kitaalam unaosapoti kwamba mentally alikuwa fit.

na shahidi wa jamuhuri hajazungumzia chochote aidha wakati wanamuhoji kulikuwa na medical proof kwamba alikuwa timamu..ushahidi wa kichaa thamani yake ni ndogo sana.

Vijana wa utetezi barabara hiyo nimewapa
 
Back
Top Bottom