Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

Huo ni ushauri na si uumbuaji. Badilisha heading ya topic isomeke: Shivji aishauri Chadema isipeleke hoja ya katiba bungeni.
 
Jamani wana JF Prof Shivji ameongea kwenye kongamano leo kwamba kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni ni hatari kwani CCM watachukua advantage ya uwingi wao bungeni kuikwamisha,does it make sense,kweli bado tuna bunge la watu wa kujali maslahi ya chama,naomba michango kwa hili.

Wao wapeleke tu but lastly "People's power shall work"
 
Great hongera Shivji, pale mjengoni sijajua hasa nia ya Mnyika, maana katika maazimio yoyote yatakayotakiwa ccm watashinda kwa wingi wao.
 
Kutokana na dhamira ya Mnyika kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni, mtoa mada wa leo Prof. ISSA SHIVJI amewaonya CHADEMA kuwa suala hilo wasilipeleke bungeni kwani hatari yake ni kuwa suala hilo litatekwa na CCM kwa vile wao ni wengi na kuamua walitakalo. Alisema ya kwamba CDM wafikirie zaidi ya jambo hilo kuliko hivi sasa ambapo wanaonyesha wanajadili mambo ya katiba kwa jazba na kishabiki

Ahsante Shivji kwa kuwa mkweli.

crap!! mtapona lini mtindio wa ubongo nyie wa%$££££nge vibaraka wa mafisadi?
 
Hapana, Jimy naòna uko sahihi.. Kama rais amesha önyesha nia ya kubadili wabunge wake hawatakuwa agaist it, na hi ni advantage ya kupata nafasi ya kujadili na hasa mswada wa marekebisho ya katiba na namna ya kurekebisha ktb, kama ni kwa tume au ni kupitia bunge. Lakini hoja inayopelekwa bungeni iko sahihi na naona itaungwa mkono na wabunge wote!
 
Huo ni ushauri na si uumbuaji. Badilisha heading ya topic isomeke: Shivji aishauri Chadema isipeleke hoja ya katiba bungeni.

Neno zuri ni uumbuaji kwani CHADEMA nzima hawakuliona hili, duh kweli CHADEMA ni chama kichanga kisiasa sana !
 
Somebody must do the job, this guy is JK

Hata ingetumika tume, bunge kuna watu watalalamika tu..

kilichopo rais lete katiba achana na walalamishi...
 
Kutokana na dhamira ya Mnyika kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni, mtoa mada wa leo Prof. ISSA SHIVJI amewaonya CHADEMA kuwa suala hilo wasilipeleke bungeni kwani hatari yake ni kuwa suala hilo litatekwa na CCM kwa vile wao ni wengi na kuamua walitakalo. Alisema ya kwamba CDM wafikirie zaidi ya jambo hilo kuliko hivi sasa ambapo wanaonyesha wanajadili mambo ya katiba kwa jazba na kishabiki

Ahsante Shivji kwa kuwa mkweli.

Hakumuumbua tu Mnyika pekee yake! alimuumbua hata Tundu Lisu kwa kutumia jazba nyingi kwenye mambo yanayohitaji tafakuri ya kina, uchambuzi na uvumilivu.
 
Mkuu, hivi haukujua kwamba ule ni mjadala? Wote wangekuwa na mawazo sawa huoni kusingekuwa na haja ya kujadili? Mi sichukulii kama ni kuumbua kama ulivyoweka title, bali ni ushauri wa Shivji tena mzuri sana kwani alitoa sababu ya kwamba ikienda bungeni, CCM watapinga kila kilicho cha wapinzani hata suala zuri la katiba, ndio maana akashauri waachiwe wananchi nje ya bunge. Aliweka bayana kwamba ni rahisi kumshinikiza rais kuliko kulishinikiza bunge. Sasa hapo amemuumbua wapi Mnyika? Halafu kuna watu humu walikuwa wanapinga katiba mpya, baada kuona rais amelazimika kuikubali, wanaanza kupinga CHADEMA! Katiba ni suala la kitaifa, si la chama, ndio maana kuna wanaharakati wengi mle wamehudhuria bila ya kupitia mwavuli wa chama, na hata UDASA walioandaa mjadala si chama cha siasa!
 
Kwenye hoja hiyo John Mnyika yupo sahihi , ni lazima Bunge liruhusu kipengere cha wananchi kupiga maoni kwani kipengere hicho hakipo>
Ndiyo maana Prof Lwaitama amemtaka Mnyika aendelee na taratibu za Bunge.

Naomba tusiwe washabiki wa vyama tujenge hoja!!!
 
Neno zuri ni uumbuaji kwani CHADEMA nzima hawakuliona hili, duh kweli CHADEMA ni chama kichanga kisiasa sana !
Kumbe hata kule Diamond Jubilee kwenye kikao cha waisilamu (aka baraza la kahawa) mlikuwa mnafuatilia yanayoongelewa Nkrumah? Safi sana!
 
Naomba next time ukipata hii chance ya kuangalia utumegee na sisi kidogo ambao hatukuweza kuangalia kwenye TV

Nakubali kuwa nilijisahau kwa kuwa siku wamealikwa Hamad Rashid na Freeman Mbowe pale Movenpick, umeme ghafla ulikatika na haukurudi mpaka wanamaliza. Niliweza kufuatilia kupitia Blackberry na mimi sikufanya hivo leo. Next time MwanaJf mwenzangu!
 
Back
Top Bottom