Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

Kutokana na dhamira ya Mnyika kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni, mtoa mada wa leo Prof. ISSA SHIVJI amewaonya CHADEMA kuwa suala hilo wasilipeleke bungeni kwani hatari yake ni kuwa suala hilo litatekwa na CCM kwa vile wao ni wengi na kuamua walitakalo. Alisema ya kwamba CDM wafikirie zaidi ya jambo hilo kuliko hivi sasa ambapo wanaonyesha wanajadili mambo ya katiba kwa jazba na kishabiki

Ahsante Shivji kwa kuwa mkweli.

brain gani kwenye ID yako haijui tofauti ya kuumbua,kushauri au kueleza? Au kasome lugha ya kiswahili.
 
mleta mada shenzi taip zako! Uwe unaunganisha mada na taito kwa ufasaha
 
Mkuu, hivi haukujua kwamba ule ni mjadala? Wote wangekuwa na mawazo sawa huoni kusingekuwa na haja ya kujadili? Mi sichukulii kama ni kuumbua kama ulivyoweka title, bali ni ushauri wa Shivji tena mzuri sana kwani alitoa sababu ya kwamba ikienda bungeni, CCM watapinga kila kilicho cha wapinzani hata suala zuri la katiba, ndio maana akashauri waachiwe wananchi nje ya bunge. Aliweka bayana kwamba ni rahisi kumshinikiza rais kuliko kulishinikiza bunge. Sasa hapo amemuumbua wapi Mnyika? Halafu kuna watu humu walikuwa wanapinga katiba mpya, baada kuona rais amelazimika kuikubali, wanaanza kupinga CHADEMA! Katiba ni suala la kitaifa, si la chama, ndio maana kuna wanaharakati wengi mle wamehudhuria bila ya kupitia mwavuli wa chama, na hata UDASA walioandaa mjadala si chama cha siasa!

Oooooooh amewaumbua bana wapenda umaarufu wa kisiasa kumbe hawajui watendalo bana !
 
Great hongera Shivji, pale mjengoni sijajua hasa nia ya Mnyika, maana katika maazimio yoyote yatakayotakiwa ccm watashinda kwa wingi wao.
Wingi sio hoja hapo!
wabunge wengi wa CCMU ni bongo lala!
 
mleta mada shenzi taip zako! Uwe unaunganisha mada na taito kwa ufasaha

Mada ipo wazi kabisa na inaeleweka, tatizo ni ushabiki wa chama na ndio unakuuma , pole kijana leo wajuzi wa mambo wamewaumbua bana !
 
Nguvu ya umma hamna tena, CHADEMA kwiiiiiiiiiiiiiiiiisha wameumbuka leo vibaya , looooh.

Sijajua unachoshangilia ni kipi hasa, maana hata Shivji naye anaweza kukosea kwa kudai kuwa ni rahisi kumshinikiza JK kuliko Bunge! Je, mambo ya ufisadi aliposhinikizwa alikubali kushughulikia mambo ya Tangold, Meremeta, Deep Green Finance, etc? Je, unafikiri itakuwa rahisi kumshinikiza rais kupunguziwa madaraka yake? Usishangilie penati, subiri goli kama litakuwepo!
 
Great hongera Shivji, pale mjengoni sijajua hasa nia ya Mnyika, maana katika maazimio yoyote yatakayotakiwa ccm watashinda kwa wingi wao.

Mnyika alikuwa anatafuta umaarufu, na humu JF waona mbali tulisha muonya hilo kabla ya Shivji, naona vibaraka wake walikuwa wanabisha tu, hawakumpelekea ujumbe.
 
Nguvu ya umma hamna tena, CHADEMA kwiiiiiiiiiiiiiiiiisha wameumbuka leo vibaya , looooh.

we umetumwa, kwa taarifa yako CDM, hakitakwisha kama unavyodhani, kama ulimsikiliza dr lwaitama, naye pia alimpinga shivji , vipi hapo je DR Lwaitama naye amemuumbua Profesa shivji?
 
Mada ipo wazi kabisa na inaeleweka, tatizo ni ushabiki wa chama na ndio unakuuma , pole kijana leo wajuzi wa mambo wamewaumbua bana !

Machoni pako unaona wameumbuka.Chadema walipowasha moto wa katiba hukuona? Mbona husemi JK kaumbuka na tume yake? Hoja ya sasa Katiba iwashirikishe wananchi wote siyo ya Tume ya JK. Na ukumbuke ilani yenu ccm haina hoja ya katiba mpya.
 
Naoma kurekebisha sio ushirika, ni (muccobs) moshi university college of cooperative and business studies ushirika kilikuwa zamani
 
Kutokana na dhamira ya Mnyika kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni, mtoa mada wa leo Prof. ISSA SHIVJI amewaonya CHADEMA kuwa suala hilo wasilipeleke bungeni kwani hatari yake ni kuwa suala hilo litatekwa na CCM kwa vile wao ni wengi na kuamua walitakalo. Alisema ya kwamba CDM wafikirie zaidi ya jambo hilo kuliko hivi sasa ambapo wanaonyesha wanajadili mambo ya katiba kwa jazba na kishabiki

Ahsante Shivji kwa kuwa mkweli.

- Haya niliyasema mapema sana, lakini haina maana kwamba katiba haijadiliki isipokuwa itafutwe njia muafaka itakayokidhi matakwa ya wote, Demokrasia ni kuwasikiliza wananchi wote kwanza!

William.
 
GeniusBrain
JF Senior Expert Member

Join Date
Wed Nov 2010
Posts
387
Thanks
0
Thanked 25 Times in 20 PostsRep Power
21

I doubt your ability of understanding things and presenting your views hence I doubt your brain to be 'genius'-I question your genius on this.
 
Oooooooh amewaumbua bana wapenda umaarufu wa kisiasa kumbe hawajui watendalo bana !

Uko sensitive na umaarufu. Nakushauri tafuta elimu ya complexity za binadamu unaweza kutatua tatizo lako linalokusumbua la kujiona au kujilinganisha na watu wengine.
 
Machoni pako unaona wameumbuka.Chadema walipowasha moto wa katiba hukuona? Mbona husemi JK kaumbuka na tume yake? Hoja ya sasa Katiba iwashirikishe wananchi wote siyo ya Tume ya JK. Na ukumbuke ilani yenu ccm haina hoja ya katiba mpya.

Leo Chadema walipewa kinaga ubaga, Katiba mpya hawajaanza kudai wao. Wasijidai! Au hukusikia mjadala wa katiba?
 
Hakika nasikitishwa na kichwa cha habari yako unaonekana si mwanamapinduzi kwa jinsi ulivyoandika habari yako na kuishabikia badala ya kuonesha muelekeo ufaao kwa taifa linaloangamizwa na mafisadi. Amakweli mzoea punda hapandi farasi.
 
Mnyika alikuwa anatafuta umaarufu, na humu JF waona mbali tulisha muonya hilo kabla ya Shivji, naona vibaraka wake walikuwa wanabisha tu, hawakumpelekea ujumbe.

Mnyika anatimiza wajibu wake kama Mbunge. Na bado mimi naamini hoja yake ina nafasi yake ya kujadiliwa. Kama itazimwa na wabunge wa CCM itakuwa vyema mlango huo utakuwa umefungwa utafunguliwa mlango mwingine mpaka kieleweke.

Mjadala umetoa mada haukutoa azimio wala mkakati wa kufuatwa. Wenye mtindio wa ubongo wameona umehitimisha upatikanaji wa katiba mpya. Wanasahau kuwa ilikuwa fursa ya watu kutoa taaluma zao na kuwapa waamuzi (wabunge na "watawala") nyenzo za kufanyia kazi.

Kwa maana nyingine facts zimewekwa hadhara wewe na mimi tuchague pumba na mchele. Mnyika achague mkakati bora wa kuwasilisha hoja yake. Wenye vichwa vya panzi warukie wanachoweza kukirukia KASHFA.
 
Mnyika alikuwa anatafuta umaarufu, na humu JF waona mbali tulisha muonya hilo kabla ya Shivji, naona vibaraka wake walikuwa wanabisha tu, hawakumpelekea ujumbe.
Zombies supporting each other.
 
Sijaona haja ya kuchukulia suala hili kishabiki kama linavyo jadiliwa hapa jamvini prof Shivuji katoa mtazamo wake na sio matokeo ya utafiti.......Na lengo hapo sio ku denounce CDM na hata hivyo mabadiliko ya katiba haya lengi CDM kushika madaraka kwa kuidondosha CCM na dhani kama kuna mtu mwenye malengo hayo basi anakosea sana.........

Mabadiliko ya katiba ni mahitaji ya watanzania kwa sasa na sio chama fulani ingawa CDM wamepanda mbegu hii nakupokelewa vizuri kabisa na jamii ingawa huko nyuma mbegu hii ilipandwa na wengine kama CUF lakini walishindwa kuisimamia.Hatahivyo hatuwezi kusema kwasababu mbegu hii ime pandwa na CDM basi ni mahitaji ya CDM pekeyao, haya nimahitaji ya nchi kwa sasa hivyo inapaswa kujadiliwa kwakina na watu wote.

Hivyo mtazamo wa Prof kama mwanazuoni hauwezi kubezwa au kushangiliwa kwa kusema amewaponda CDM au Mnyika huu ni mchango wake ambao unahitaji pia kutazamwa na kupimwa......huwezi kusema mjadala huu bungeni uta tekwa na ccm kwa sababu inawabunge wengi, pengine mtazamo huu sio sahii kwa mfano mdogo tu wa bunge lililopita wa bunge wa upinzani walikuwa wa chache kuliko sasa lakini hoja nzito ziliibuliwa bungeni na serikali ya ccm iliwajibika kwa utendaji wake mbovu............hivyo huwezi sema prof katoa agizo mawazo yake ya tekelezwe hapa katoa mtazamo wake ambao pia unahitaji kuangaliwa .....

Kama tukitumia Constitution assembly ili kupata katiba mpya tutapita wapi kama sio bungeni? hivyo hili jambao halihitaji ushabiki bali linahitaji uelewa wakina na mijadala mikubwa kama uliofanyika leo lazima iwe mingi hatimaye tutapata kitu sahihi tunacho hitaji kama jamii nzima ya Tanzania bila ushabiki wa kimakundi...........
 
Back
Top Bottom