Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

Maoni ya Mwanazuoni Prof. Dr. Issa Shivji ni kuwa hoja ya Mhe. John Mnyika itatekwa na CCM ikiwasilishwa Bungeni. Maoni ya Mwanataaluma Dr. Azaveli Lwaitama ni kuwa hoja ya Katiba Mpya ipelekwe kila sehemu na kwa kila mtu; iwe Bungeni, Misikitini, Makanisani, Sokoni, Vyuo vyote, Shule zote, Vijiji vyote, Miji yote ili watu wote watoe maoni yao. Hoja hiyo itakapojadiliwa Bungeni, CCM wakiamua kuwa na mtazamo hasi, Watanzania ambao sasa hawadanganyiki watajua kutofautisha pumba na mchele.
Big up Mnyika
 
Shukrani sana na Hongereni waheshimiwa wote mliotuwezesha kufatilia mjadala huu hata huku kusiko na Luninga wala, Big up kwenu wana JF
wazalendo mliokuwa mkiripoti live. Nimepata mambo mengi ya msingi kwa kazi yenu njema. Mbarikiwe.
 
@genius brain, we chalii akili zako za kuku, we uwezo wa kufikir mdogo , na huna uchungu na kizaz kijacho , cjui nkwambiaje , 2nahitaji katiba mpya hata wasomi wanaunga mkono sasa unaleta ujinga ujinga2.
 
Kutokana na dhamira ya Mnyika kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni, mtoa mada wa leo Prof. ISSA SHIVJI amewaonya CHADEMA kuwa suala hilo wasilipeleke bungeni kwani hatari yake ni kuwa suala hilo litatekwa na CCM kwa vile wao ni wengi na kuamua walitakalo. Alisema ya kwamba CDM wafikirie zaidi ya jambo hilo kuliko hivi sasa ambapo wanaonyesha wanajadili mambo ya katiba kwa jazba na kishabiki

Ahsante Shivji kwa kuwa mkweli.

Kichwa cha habari hutokana na habari husika na kwa maana hiyo kichwa cha habari chapaswa kuwa 'Kongamano la katiba : Shivji awaonya Mnyika na CHADEMA'

Ni wazo zuri la Prof.Shivji kwa kuwa CCM wako wengi na wanaweza kuichakachua hoja ya kina mnyika na kuifanya ya kwao.
 
Mnyika alikuwa na malengo sahihi kupeleka hoja bungeni,sasa Prof Shivji kamshauri tofauti.....ni kiasi cha kusonga mbele na mchakato wa katiba mpya,haya ya amemuumbua sijui yana tija gani tena????Katiba ni yetu sote na tusaidiane kuhakikisha mchakato unaanza na unamalizika kwa sisi kupata katiba mpya na inayokidhi mahitaji,mtizamo tu.
 
Kazi kubwa ambayo Profesa Shivji na Jenerali Ulimwengu wameifanya leo imetibuliwa na wao wote wawili kuiunga mkono Tume batili ya JK kwa hali yoyote ile.....................JK hana mamlaka ya klsheria ya kutuundia Tume hivyo wanazuoni hawa walichemsha sana waliposema hawaoni kuwa ina matatizo ila tatizo ni muundo wake, hadidu za rejea na itapeleka wapi taarifa yao...................................

Tatizo la katiba iliyopo ni ushirikishwaji sasa hii Tume ya Raisi itakuwa imechaguliwa kwa vigezo vipi wakati upatikanaji wake haukutoa nafasi na fursa sawa kwa raia wote kushiriki katika kuziomba nafasi hizo?

Itakuwaje Tume ambayo haikupatikana kwa misingi ya kiutu tuitegemee iende kutujengea misingi ya kiutu?

Utaratibu ufaao ni Bunge kutunga sheria ya kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya...................Tume ya wataalamu ya kuratibu zoezi hilo iwepo lakini ipatikane kwa Bunge kuzitangaza nafasi na sifa zake kwenye magazeti ili kutoa fursa sawa ya raia wote wenye sifa kuziomba...............................na kamati maalumu ya Bunge ichuje na kuteua wastahiki ambao watapigiwa kura Bungeni na wakipitishwa basi Raisi ndiyo awateue.....................................Bila kutoa fursa sawa kwa wote usitegemee hiyo itakuwa ni katiba mpya.....................la hasha.

Mawazo mengine ya namna ya kuuunda Mkutano mkuu ninayauinga mkono kuwa wajumbe wake wachaguliwe moja kwa moja kupitia majimbo ya uchaguzi yaliyopo na wabunge au watumishi serikalini wasishiri kwenye Mkutano huo wa kikatiba.............................
 
Jenerali Ulimwengu alimaliza pale pale aliposema "...inafika mahali mtu anateuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mkoa... kwa sababu ni hawala yake..., mteliwa huyo wananchi wakimpelekea malalamiko anawajibu hovyo hovyo atakavyo kwa sababu tu hawezi kuwajibishwa na hawala yake..! Watu ukumbini walishangiliaje, inaonekana kama ilimgusa mtu pale!

Jenerali alipendekeza wakuu wa wilaya na mikoa wachaguliwe na wananchi wa eneo husika ili awajibike kwao moja kwa moja na umma uwe na sauti ya mwisho katika matumizi ya rasilimali za eneo lao. Nili ipenda sana hoja hii! Big up Ulimwengu!

Huyu ulimwengu jamani ni mjenzi makini wa taifa hata kule ikulu wanajua.Ukisoma na kutafakari kwa makini vitabu vyake na makala magazetini utagundua huwa hakurupuki?Kama rais ana mamlaka ya kumteua kila mtu bila hata sifa,ndio mwanya mkuu wa kuchomeka hawara zake.Kwa katiba yetu ilivyo mkuu wa nchi anaweza kukutana na msichana mrembo katika mji fulani nchini na baadaye kama watakubaliana akaamua kumpigia simu na kumwambia kuwa amemteua kuwa mkuu wa wilaya walipokutana.Katiba mpya ni lazima wala sio ombi kwa kuwa katiba ni ya wananchi.
 
Kutokana na dhamira ya Mnyika kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni, mtoa mada wa leo Prof. ISSA SHIVJI amewaonya CHADEMA kuwa suala hilo wasilipeleke bungeni kwani hatari yake ni kuwa suala hilo litatekwa na CCM kwa vile wao ni wengi na kuamua walitakalo. Alisema ya kwamba CDM wafikirie zaidi ya jambo hilo kuliko hivi sasa ambapo wanaonyesha wanajadili mambo ya katiba kwa jazba na kishabiki

Ahsante Shivji kwa kuwa mkweli.

Miss Garbagebrain tofautisha ushauri na kuumbua..
 
Kitendo cha rais ku-own process ya kuwateua wajumbe wa kamati ya katiba hakiwezi kuungwa mkono. Nakubaliana na mawazo yako.
 
Kutokana na dhamira ya Mnyika kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni, mtoa mada wa leo Prof. ISSA SHIVJI amewaonya CHADEMA kuwa suala hilo wasilipeleke bungeni kwani hatari yake ni kuwa suala hilo litatekwa na CCM kwa vile wao ni wengi na kuamua walitakalo. Alisema ya kwamba CDM wafikirie zaidi ya jambo hilo kuliko hivi sasa ambapo wanaonyesha wanajadili mambo ya katiba kwa jazba na kishabiki

Ahsante Shivji kwa kuwa mkweli.


Kaka Mnyika hajaumbuliwa ila amepewa ushauri tusiwe tunaongea ki-layman jamani hii haitujengi positively kwani Mnyika ni adui yko au nawe ndio ni walewale. Ukisema kaumbuliwa ni kama vile Mnyika hakuwa na nia ya dhati ya kile alichokisimamia, mimi naona ushauri aliotoa Pro. Shivji kwa nafasi na ujuvi wake kitaaluma ni lazima si ajabu kujua ambalo kijana makini kama Mnyika hakuwa amelibaini kutokana na umri wake katika siasa lakini cha msingi hapa ni nia yake dhati kuchangia katika kuleta mabadiliko chanya nchini. KWA PAMOJA TUTASHINDA UDHALIMU WA MAFISADI.
 
Kutokana na dhamira ya Mnyika kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni, mtoa mada wa leo Prof. ISSA SHIVJI amewaonya CHADEMA kuwa suala hilo wasilipeleke bungeni kwani hatari yake ni kuwa suala hilo litatekwa na CCM kwa vile wao ni wengi na kuamua walitakalo. Alisema ya kwamba CDM wafikirie zaidi ya jambo hilo kuliko hivi sasa ambapo wanaonyesha wanajadili mambo ya katiba kwa jazba na kishabiki

Ahsante Shivji kwa kuwa mkweli.

Jamani msisahau hawa memba wa Jamii Forums ni wapinga mabadiliko na ant-CHADEMA maarufu:

Malaria Sugu,Dar es Salaam,Zomba,Mhadhiri,Zena,Jeykey,GeniusBrain ,W.J.Malecela,.....

Halafu huyu mtu Pumba kabisa

GeniusBrain
JF Senior Expert Member

Join Date Wed Nov 2010
Posts 387
Thanks 0
Thanked 25 Times in 20 Posts Rep Power 21
 
tunapenda kuwataarifu wananchi ambao hawataweza kufika ckd kuwa kongamano la katiba kesho litaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha itv. Tunawashukuru sana itv kwa moyo wa uzalendo.

Karibuni

kitila
hongera comrade kwa kutoa mchango muhimu katika kuweka misingi ya tanzania mpya
 
Hata kupeleka bungeni bado linaweza kwama hasa ukiangalia idadi ya wabunge wa ccm walivyowengi ambao wengi wao ni fuata upepo tu, wamwshalewa na ccm hata kwa jambo la msingi wao wanaangalia maslahi ya chama badala ya taifa!
 
Uko sensitive na umaarufu. Nakushauri tafuta elimu ya complexity za binadamu unaweza kutatua tatizo lako linalokusumbua la kujiona au kujilinganisha na watu wengine.
Nadhani ni katibu kata huyu bwana.
 
Jenerali Ulimwengu alimaliza pale pale aliposema "...inafika mahali mtu anateuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mkoa... kwa sababu ni hawala yake..., mteliwa huyo wananchi wakimpelekea malalamiko anawajibu hovyo hovyo atakavyo kwa sababu tu hawezi kuwajibishwa na hawala yake..! Watu ukumbini walishangiliaje, inaonekana kama ilimgusa mtu pale!

Jenerali alipendekeza wakuu wa wilaya na mikoa wachaguliwe na wananchi wa eneo husika ili awajibike kwao moja kwa moja na umma uwe na sauti ya mwisho katika matumizi ya rasilimali za eneo lao. Nili ipenda sana hoja hii! Big up Ulimwengu!

Kwa kuwa katiba mpya inatakiwa iwe YA WANANCHI, basi Rais wa nchi itabidi aondolewe baadhi ya madaraka makubwa sana aliyo nayo. Imeonekana katika teuzi kadhaa (Jenerali amezungumzia baadhi ya wakuu wa wilaya na sababu za ajabu za kuteuliwa kwao) kuwa madaraka hayo yanatumika vibaya.

Big up UDASA ( Prof Kibogoya, Kitila et al), Pro Shivji, Jenerali Ulimwengu, ITV...

Kama alivyosema Prof Shivji, hitaji la Katiba mpya lioanishwe moja kwa moja na mahitaji ya kila siku ya wananchi. Hapo ndipo wananchi wengi wataelewa.

Mfano mmoja:
Wananchi wakifahamishwa kuwa usiri wa mikataba ya 'wawekezaji'/wachotaji na serikali ndio usaosababisha 'misamaha' mikubwa ya kodi, na hivyo kuinyima nchi yetu mapato, na matokeo yake huduma za muhimu sana kama vile ELIMU, AFYA, MAJI, UMEME na MIUNDOMBINU, ambazo zingeweza kutolewa kwa kutumia kodi hizo kama zingekusanywa bila 'kusamehewa' (yaani BURE kwa maana kuwa mwananchi hatalipia moja kwa moja tena, bali zitatoka kwenye makusanyo ya KODI).

Hapa mwananchi ataelewa umuhimu wa katiba mpya.
 
"Tunachotakiwa kudai ni KATIBA kwa sababu nchi yetu haijawahi kuwa na KATIBA"

ndugu wanajf,nimejaribu kusikiliza kwa makini kongamano la katiba liliondaliwa na Udasa na mojawapo ya mambo muhimu ya liyosemwa ni kwamba mfumo 'katiba' wa sasa si halali kisiasa na kuna mashaka ya uhalali wake kisheria.
Kwa mujibu wa watoa mada katiba ni muafaka wa kitaifa hivyo ni muhimu kushirikisha wananchi.
Mfumo tulionao sasa ambao ndio tunauchukulia kama 'katiba' hakuwahi hata maramoja kuwashirikisha wananchi.Hivi karibuni tumeona wanasiasa na makundi mbalimbali na hata sisi wana JF tukidai katiba mpya as if katiba ya Tanzania iliwahi kuwepo,kulingana na maelezo ya leo naomba tuanze kudai Katiba na siyo katiba mpya.
Hoja ya kwamba mfumo 'katiba' tulionao umepitwa na wakati au una mapungufu zimeonekana si hoja tena this is why majibu ya Kombani na Werema yalikuwa rahisi kwa maswali magumu.kumbe sasa watanzania tunatakiwa kudai katiba kwani hatunayo!
Ulimwengu ametuambia kuwa kizazi chetu ni cha faster faster,twanga kotekote n.k. Hivyo kuna ugumu kupata katiba ndani ya miaka 5.Nakubaliana naye,na hii ni kutokana na ukweli kwamba hatujawahi kuwa na katiba au mungozo halali ulioshirikisha wananchi.kwa kuwa HATUNA KATIBA ni muhimu kazi ya kuipata katiba halali ya nchi yetu ipewe priority kuanzia leo hii.sitegemei kama tunaweza kurudi kwenye misingi kama ile ya mwana TANU chini ya uongozi na mfumo chakachuzi tulionao.hivyo ni muhimu kwa wanaharakati na wasomi kukomaa ili tupate katiba.

Binafsi nimefurahishwa na kitendo cha wanazuoni kuamka na kutuonyesha njia na sio kuwaachia wanasiasa ambao kwa mujibu wa prof shivji huwa hawapendi siasa bali hupenda madaraka.

WanaJF Nawasilisha....
 
Nimeona Prof Shivji amewashambulia Chadema (subtly), mara nyingi sana. Baada ya kuwaza sana nimeona anaweza akawa na personal reasons. Najua watu wanaogopa kusema ukweli kuhusu maoni yake.

(1) Prof Shivji bado anataka tujenge socialism. Why is everybody afraid to update him on the fact that socialism has failed here and everywhere?

(2) Siamini kwamba Prof Shivji hafahamu kwamba njia ya kuteua Tume ya Rais ni mbaya. I am forced to suspect that he supports it for personal reasons. Anajua anaweza kuwa ndiye gwiji wa sheria ambaye Rais anatarajia kumteua kuongoza hiyo tume.

(3) Baada ya kuangalia kongamano la leo, I no longer trust this distinguished Professor.
 
Sioni hatari yoyote kwa bunge ambalo ni mdau mkubwa sana katika sheria zilizopo na zijazo kushirikishwa katika mchakato mzima wa kupata katiba mpya Tanzania.Sijui itafanyika vipi bila kulihusisha bunge na CCM.
Mnyika hapeleki Rasimu ya katiba bungeni bali Hoja Binafsi kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya.
Rais ameanza kuonyesha Mchakato wake binafsi(au wa chama chake?!) na angependa kusiwe na mashinikizo yaaani watu wawe wanasema "Ndio mzee"
Mchakato wowote utakaofaulu kupitishwa na kutumika unahitaji HAMASA kumbwa ya wananchi na mashinikizo kabambe ya Uma.
Sababu lazima kutakuwa na vipengele ambavyo ni visu vikali kwa watawala Bomu na wezi na hawatapenda viwepo. Vitakuwepo tu kwa mashinikizo imara ya wananchi.
 
Ulimwengu ni mtu wa kutotaka lawama, anatumia akili nyingi kuongea kitu ambacho hakitaigusa serikali na hata kama kitaigusa basi ni wachache ndio watakaomwelewa. saijui kwa sababu ya issue zake za nyuma?
 
Back
Top Bottom