Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

bunge la ccm na kamati zake ni kupoteza muda!tume ya wataalamu si wanasiasa, iratibu maoni ya wananchi na kutoka na kitu cha kueleweka

JF hebu saidieni kuelimisha tofauti ya mcakato wa kuandika katiba na uandikaji wa katiba!!! Sijui kama ninaelewa vibaya kwamba katika hatua ya mwanzo ssa ni kupata ridhaa ya kitaifa mchakato uchukue sura ipi-chombo gani kisimamie utekelezaji; muda gani unakubalika kitaifa; wadau ni akina nani???? nk; kabla ya kuanza kazi yenyewe-kama tunayumba hivi ni heri tuazime nakala ya Kenya turekebishe kisha tutumie-lakini hii ya kila mmoja anakuja na thoery yake intia shaka kama tutakuja kuwa na kitu cha maana!!!!!!!!!! Tukumbuke hii ndiyo mara ya kwanza taifa hili kuandika katiba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Bila kuwa na mwongozo mmoja uliokubalika kitaifa kupitia bunge sasa hawa wanaotaka kutufanya tuogope kutumia bunge hatimaye watuambie chombo gani halali kitapitisha muswada wa katiba mpya kuwa sheria????????????????????????
 
ndugu..rais ni wa watanzania.. tumemchaguaa watanzania.. razima achague kamati ya kuuna katiba, naungana na shivji na general
 
Hapana, Jimy naòna uko sahihi.. Kama rais amesha önyesha nia ya kubadili wabunge wake hawatakuwa agaist it, na hi ni advantage ya kupata nafasi ya kujadili na hasa mswada wa marekebisho ya katiba na namna ya kurekebisha ktb, kama ni kwa tume au ni kupitia bunge. Lakini hoja inayopelekwa bungeni iko sahihi na naona itaungwa mkono na wabunge wote!

Rais gani! Mnamaanisha JK? Thubutu yenu.
kwa taarifa kama katiba mpya itaonyesha mwelekeo ufuatao:
* kama itaonekana kuondoa uwezekano wa CCM kuanguka 2015
* kama itaonekana katiba mpya itazuia au kumfanya Rais awajibike baada ya kutoka madarakani endapo kafanya uovu kama hali ilivyo kwa JK sasa.
* endapo itaonekana katiba mpya itagusa au kutishia mtiririko wa kambi ya JK, RA na EL ktk kumwandaa mrithi wa JK ambalo ndio lengo kamilifu lao kuhakikisha mtandao wao wa kula nchi chini ya RA hauvunjwi.

JK ataitisha kambi ya wabunge wake kuyeyusha hoja na hatimae mob yake itasapoti, na hatimae wataweka viraka tu ili kuwanusuru.
 
Sijapenda maneno ya mabele malando kwamba damu ya watu ambao hawana hatia kugeuzwa wino wa kuandikia katiba.....kuna na watu wengine wenye mawazo kwamba ili mabadiliko yatokee lazima damu imwagiike... Hayo mawazo hayafai na ni yakuleta uchochezi....nchi yetu ni ya amani na katiba yetu mpya tutaipata kwa amani...

Mahatma ghandi ..violence bring more harm more than goodness.
 
Sipendi mtz anasema tuna amani. Tuna amani kwenye dimbwi la umasiki.
 
Ni kweli inawezekana kabisa JK aliongea ili kupooza munkari ya waTZ kuhusu katiba,what if kama hayuko serious na hili swala anaweza ku mobilize wabunge wake wakagomea katiba na kutaka kuweka viraka swala ambalo watanzania hatutaki,shivji may be right!!!!!!
Rais gani! Mnamaanisha JK? Thubutu yenu.
kwa taarifa kama katiba mpya itaonyesha mwelekeo ufuatao:
* kama itaonekana kuondoa uwezekano wa CCM kuanguka 2015
* kama itaonekana katiba mpya itazuia au kumfanya Rais awajibike baada ya kutoka madarakani endapo kafanya uovu kama hali ilivyo kwa JK sasa.
* endapo itaonekana katiba mpya itagusa au kutishia mtiririko wa kambi ya JK, RA na EL ktk kumwandaa mrithi wa JK ambalo ndio lengo kamilifu lao kuhakikisha mtandao wao wa kula nchi chini ya RA hauvunjwi.

JK ataitisha kambi ya wabunge wake kuyeyusha hoja na hatimae mob yake itasapoti, na hatimae wataweka viraka tu ili kuwanusuru.
 
amewaambia endapo swala la katiba mpya litaenda bungeni ccm watutunga katiba yao na kuungwa mkono na wabunge wengi wa ccm. kwa hivyo bado katiba haitakuwa na maslahi kwa chadema na taifa kwa ujumla.
jee kwa hali hiyo hii hoja ya Mnyika tuifanyeje? au chadema na wanamageuzi wafanyeje ili kuipiga chenga ccm?
 
WANAZUONI wameshauri Katiba mpya iandaliwe kwa kushirikisha wananchi tofauti na zilivyoandaliwa Katiba zilizotangulia.

Hilo linatokana na ukweli kuwa wananchi wataridhika kuwa na Katiba ambayo wameshiriki kuielewa, kuijadili, kuiamua na kuilinda kwa maslahi yao.

Wakichangia mada katika kongamano la Katiba lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) jana, wanazuoni hao walisema mchakato wa Katiba mpya ni lazima ushirikishe wananchi kikamilifu kwani ndio moja ya upungufu ulio katika Katiba ya sasa na zilizotangulia.

Profesa Issa Shivji katika mada yake, alisema Mamlaka yoyote inatokana na watu kwani ndiyo dhana halisi ya Katiba, hivyo kushirikisha wananchi katika mchakato wa Katiba mpya ni muafaka kitaifa, kwani ni mali ya wananchi.

Profesa Shivji ambaye pia ni Mtaalamu wa Sheria alisema Katiba mpya inahitajika kwani kihistoria, katiba zote zilizopita nchini, wananchi hawakushirikishwa wakati uhalali wa Katiba unategemea ilivyotungwa na ushirikishwaji wa wananchi na upungufu huo hauwezi kurekebishwa kwa kupitia Bunge.

Alisema tangu uhuru zimekuwapo katiba tano; mwaka 1961, 1962, 1964, 1965 na 1977, ambazo zote alisema zilitungwa bila kushirikisha wananchi.

“Katiba lazima iwe na uhalali wa kisiasa na kisheria kwa kushirikisha wananchi ili wapate Katiba wanayoielewa na kuilinda … wananchi wanapaswa kupewa nafasi ya kutosha kujadili Katiba mpya kwa maslahi yao,” alisema.

Alipendekeza wakati wa mchakato wa Katiba lazima uwepo muafaka wa kitaifa, kisheria na iwepo mijadala midogo kuanzia ngazi ya chini hadi kongamano la kitaifa.

Profesa Shivji ambaye alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema mjadala
wa Katiba usipelekwe bungeni, kwani kitakuwa ndicho chanzo cha kuwagawa wananchi na kukipa nguvu ya Chama Tawala kuweka mambo ya maslahi kwake kutokana na kuwa na wabunge wengi.

“Huu ni mchakato wa kisiasa, hauhitaji sheria, kwa hiyo wananchi wapewe nafasi ya kujadili, Bunge litaingia katika mjadala baada ya mchakato huo wa kisiasa … kila kundi likianzisha mjadala huu, tutakuwa na nguvu ya kumshinikiza Rais, hivyo tuhakikishe mjadala unakuwa wa wananchi,” alisema.

Jenerali Ulimwengu katika mada yake, alikiri kuwa Watanzania hawajawahi kujadili wala kuandika Katiba yao, lakini sasa fursa imefika ya kuandika Katiba itakayokuwa ya maslahi kwao.

Ulimwengu alisema tabia au dhana iliyojengwa na baadhi ya watawala waliozoea kurekebisha Katiba kwa maslahi binafsi ndiyo inayofanya baadhi yao kupinga hoja ya kuanzisha mchakato wa Katiba mpya.

Alisema mtazamo huo umepitwa na wakati na viongozi wanapaswa kufahamu anayetakiwa sasa kushika hatamu ni mwananchi kupitia Katiba mpya itakayoundwa kwa kuwashirikisha.

Ulimwengu alisema hatua hii ya kutaka Katiba mpya ni nafasi ya Watanzania kujisanifu upya na serikali yenye busara itakuwa inasoma ishara za nyakati na inapaswa kufahamu wakati wa kuacha.

Kwa mujibu wa Ulimwengu, Katiba mpya itafanikiwa iwapo Watanzania watakuwa na utashi wa kitaifa na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kujitambua ili wawe na maadili ya kitaifa.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema suala la kutaka kuwa na Katiba mpya lisichukuliwe kama njia ya Watanzania kujiua, iwe fursa ya kisiasa na kama utakuwapo mshikamano wa kitaifa, Katiba mpya itafanikiwa, vinginevyo kila mmoja akilibeba mwenyewe itashindikana.

Profesa Gaudense Mpangala alisema sababu ya kutaka Katiba mpya ni kuepusha Taifa kuingia kwenye migogoro na umwagaji damu, mambo ambayo yametokea katika nchi zingine jirani.

Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alitoa hadhari kuwa iwapo ripoti ya Tume itakayoundwa na Rais itapelekwa kwenye vyombo vya Katiba, mambo yatakuwa yale yale, hivyo akatoa angalizo la kuhakikisha hilo halitokei na kusisitiza pia mshikamano wa kitaifa kwa alichoeleza kuwa kitasaidia kwenye mchakato wa Katiba mpya.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Ananilea Nkya, aliitaka Serikali kuwekeza kwa wananchi kwa kuwa na mijadala mbalimbali ya kuwaelimisha kuhusu suala zima la Katiba na mchakato wa Katiba mpya.

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ibrahim Kaduma, alisema ili kuandika Katiba mpya ni lazima Watanzania wafahamu kwanza ni nini maadili yake ya kitaifa.

Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani, ambaye alikaribishwa kama mgeni kwenye kongamano hilo, alisema amesikia mada, maoni na michango kuhusu matakwa ya Katiba mpya na hivyo atakwenda kuyafanyia kazi.

“Nimekuja kama watu wengine, nimekaribishwa kusikiliza mjadala, nimesikia, nimeyapokea nitakwenda kuyafanyia kazi, kwa hiyo kwa sasa siwezi kusema lolote zaidi,” alisema.

Chanzo: Habari Leo
 
Ruta,
kama nilimwelewa vema Shivji alisema kuwa Bunge limejaa CCM kwa hiyo ni rahisi kupitisha matakwa ya Sisi em. Kwa hiyo akashauri kuwa ni rahisi kumshinikiza rais kuliko Bunge. Kwa maana nyingine aliona alternative zote zikiwa flawed akaona bora ya rais.
Hata hivyo tusisahau kuwa nao ni binadamu ambao waweza kosea na ni watanzania ambao wanaruhusiwa kutoa maoni yako. Nawe pia una haki ya kutoa uonacho vyema.

Ili tukichanganya yote tupate kitu solid. So let us go!
 
Mimi sikubahatika kuangalia kongamano la katiba UDSM leo nimesikia kulikua na mambo matamu sana naomba mwnye video yake atuwekee humu jamvini tushuhudiee .
 
Wakimbizi mmeshaamka mmeanza kuchochea vurugu wakati sie wenyewe, yaani Watanzania wazalendo tunaojenga hii nchi, tumewasikia vema, yaani loud and clear Shivji na Ulimwengu. Kama mna hoja sana kwenye kongamano lijalo msikose.
 
Ndugu yangu shida ni usafiri wa kutoka Kigoma kuja Dar. Na bahati mbaya huko Manyovu niliko hata umeme hakuna, hivyo sijui itv huko haipo.
 
Basi umefanya jitihada hadi ukaweza kuposti hapa muda huu. Kwa maana hiyo, unaweza kujitahidi kupata usafiri wa kutoka Kigoma ili kongamano lijalo usikose.
 
Mimi sikubahatika kuangalia kongamano la katiba UDSM leo nimesikia kulikua na mambo matamu sana naomba mwnye video yake atuwekee humu jamvini tushuhudiee .
Kuna thread ya special request ya DVD, ambayo haijaungwa mkono na inakufa sasa, Iunge mkono may be dr atai consider :smile-big:
 
Sijapenda maneno ya mabele malando kwamba damu ya watu ambao hawana hatia kugeuzwa wino wa kuandikia katiba.....kuna na watu wengine wenye mawazo kwamba ili mabadiliko yatokee lazima damu imwagiike... Hayo mawazo hayafai na ni yakuleta uchochezi....nchi yetu ni ya amani na katiba yetu mpya tutaipata kwa amani...

Mahatma ghandi ..violence bring more harm more than goodness.

mkuu unajifariji tu.
 
Mpuuzeni huyuShivji-ameishi na utawala wa Hayati Nyerere miaka mingapi? iweje leo aseme maneno yenye mantiki ya kutuyumbisha????????
Huyu ni ndumila kuwili!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Watu wa aina yako mpo wengi na ndiyo mnatusababisha tuzunguke pale pale kwa miaka nenda rudi...utapata hasara gani kutathmini unalozungumza kabla ya kulitoa?
Pia nitoe angalizo, km ukishindwa kuelewa kitu usifikiri wengi pia hawakuelewa sawa nawe hivyo kutumia maneno ya wingi km "kutuyumbisha" unajumuisha wengine wasio vilaza km wewe...Issa Shivji ni mwanazuoni mkomavu,kutomwelewa si kitu kibaya hasa ikizingatiwa kiwango cha uelewa kinatofautiana kati ya mtu na mtu...km hukumwelewa leo utamwelewa kesho,mwezi ujao hata mwakani,muhimu tembea na tafakuri kichwani!
 
Mjadala wa Katiba mpya: Shivji awaonya wapinzani, wananchi

na Nasra Abdallah

amka2.gif
PAZIA la mjadala wa Katiba mpya limefunguliwa huku wanasiasa wa vyama vya upinzani na wananchi wakionywa kuwa macho na mjadala huo utakapopelekwa bungeni ili CCM isiupindishe.
Tahadhari hiyo ilitolewa jana na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Issa Shivji, kwenye kongamano la kujadili Katiba mpya lililoandaliwa na Jumuiya ya wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA).
Profesa Shivji alisema ni bora suala hili likabakia mikononi mwa wananchi ili walijadili kwa kina na ikiwezekana kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kuliko kulipeleka bungeni ambako CCM inaweza kutumia wingi wa wabunge kulinda masilahi yake.
Tahadhari hiyo ya Shivji, ilitokana na hoja ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), kuonyesha wasiwasi wake na kutaka suala hilo lipelekwe bungeni kwanza ili lifanyiwe marekebisho kwenye baadhi ya vipengele vya sheria, ibara ya 98, inayosema Bunge ndilo lenye mamlaka ya kubadilisha Katiba.
Akijibu hoja hiyo, Shivji alisema Bunge halina uwezo wa kupinga Katiba na kwenye Katiba hakuna sheria inayopinga mjadala wa kitaifa kama huo.
Alisema hata kama itatokea mchakato huo ukapelekwa bungeni, kamwe sheria hizo anazozitaka (Mnyika) zibadilishwe hazitawezekana.
Naye kada wa CHADEMA, Mabere Marando, alisema kuwa mpaka sasa Katiba mpya imeshaanza kuandikwa kutokana na tukio la vurugu zilizotokea hivi karibuni mjini Arusha.
Marando alisema damu iliyomwagika katika vurugu hizo ndio wino wa kwanza wa kuandikia dibaji ya katiba hiyo na harakati bado zinaendelea.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ibrahim Lipumba, alisema katika ilani ya CCM hakukuwa na suala la katiba wala katika hotuba ya rais aliyoitoa bungeni hakukuwa na suala hilo, hivyo kuna haja ya kuwa na mshikamano katika suala hili, kwani bila hivyo nchi inaweza kuingia kwenye machafuko.
Mwandishi mkongwe, Jenerali Ulimwengu, alisema katiba iliyopo msingi wake ni falsafa za Waingereza na hata mabadiliko yaliyokuwa yakifanywa mara kwa mara hayakuwashirikisha wananchi.
"Baada ya uhuru hakukuwa na mchakato wa kuwaweka wananchi pamoja na kuona jinsi gani ya kuendesha nchi yao, zaidi walishirikishwa viongozi wa chama na wataalamu wachache kunyofoa na kurekebisha katiba hiyo.
"Katika hili ningependa tujipe muda zaidi wa kujenga Katiba mpya na si kuvipa nguvu vyama vya siasa na kazi ya tume iwe ya kuratibu mijadala tu," alisema.
Ulimwengu alisema haoni kama kuna gharama kubwa ya mchakato wa uundwaji wa Katiba ukilinganisha na machafuko yanayoweza kutokea baadaye.
Alibainisha kuwa kinachotakiwa ni kuona wananchi wa kawaida wanakuwa na madaraka juu ya maisha yao na matumizi ya rasilimali zao badala ya watawala kuendelea kuishikilia mifumo ya kikoloni.
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi Wanawake (TAMWA), Ananelia Nkya, alisema kwa muda mrefu amekuwa akifuatilia mijadala hiyo katika vyombo vya habari, lakini suala la ushirikishwaji wa wanawake umekuwa mdogo ukilinganisha na wanaume.
Mkurugenzi huyo aliitaka serikali kuhakikisha inawekeza katika kuwawezesha wananchi kujua ni nini kilichopo katika Katiba iliyopo kwanza, kwa kutumia redio, televisheni na magazeti inayoyamiliki na vyombo vingine vya habari.
Mchangia mada mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Aristoto Steven, alisema viongozi wa nchi hii kwa muda mrefu wamekuwa wagumu wa kusikia, hivyo kwake anaona midahalo, makongamano na semina vinaweza kuwa bure.
Kutokana na sababu hiyo, Steven alipendekeza vyama vya siasa kwa kushirikiana na wananchi kushinikiza suala hilo kwa kuitisha maandamano kwani lugha nyepesi na za kubembeleza haziwezi kuleta Katiba mpya.
Dk. Azaveri Lweitama, alisema hakuna haja ya kuwazodoa viongozi ambao awali walionekana kupinga uundwaji wa Katiba mpya, pia hoja ya Mnyika ya mjadala huo kwenda bungeni na kuweza kupigiwa kura, anauunga mkono ili wananchi wajue ni kina nani hasa wanaopinga ili wapate pa kuanzia.
Profesa Lwaitama alisema kuwapo kwa Waziri Kombani katika kongamano hilo la jana ni kielelezo tosha cha kuendelea kujadiliwa kwa mchakato wa katiba.
Katika kongamano hilo, lililoanza majira ya saa nne asubuhi na kumalizika saa nane, wananchi wengi waliohudhuria walionekana kuunga mkono hoja ya kuundwa kwa Katiba mpya na si kurekebishwa wala kuwekwa viraka, sababu kubwa ikiwa katiba zote zilizorekebishwa huko nyuma hazikushirikisha wananchi.
 
Mjadala wa Katiba mpya: Shivji awaonya wapinzani, wananchi

na Nasra Abdallah

amka2.gif
PAZIA la mjadala wa Katiba mpya limefunguliwa huku wanasiasa wa vyama vya upinzani na wananchi wakionywa kuwa macho na mjadala huo utakapopelekwa bungeni ili CCM isiupindishe.
Tahadhari hiyo ilitolewa jana na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Issa Shivji, kwenye kongamano la kujadili Katiba mpya lililoandaliwa na Jumuiya ya wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA).
Profesa Shivji alisema ni bora suala hili likabakia mikononi mwa wananchi ili walijadili kwa kina na ikiwezekana kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kuliko kulipeleka bungeni ambako CCM inaweza kutumia wingi wa wabunge kulinda masilahi yake.
Tahadhari hiyo ya Shivji, ilitokana na hoja ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), kuonyesha wasiwasi wake na kutaka suala hilo lipelekwe bungeni kwanza ili lifanyiwe marekebisho kwenye baadhi ya vipengele vya sheria, ibara ya 98, inayosema Bunge ndilo lenye mamlaka ya kubadilisha Katiba.
Akijibu hoja hiyo, Shivji alisema Bunge halina uwezo wa kupinga Katiba na kwenye Katiba hakuna sheria inayopinga mjadala wa kitaifa kama huo.
Alisema hata kama itatokea mchakato huo ukapelekwa bungeni, kamwe sheria hizo anazozitaka (Mnyika) zibadilishwe hazitawezekana.
Naye kada wa CHADEMA, Mabere Marando, alisema kuwa mpaka sasa Katiba mpya imeshaanza kuandikwa kutokana na tukio la vurugu zilizotokea hivi karibuni mjini Arusha.
Marando alisema damu iliyomwagika katika vurugu hizo ndio wino wa kwanza wa kuandikia dibaji ya katiba hiyo na harakati bado zinaendelea.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ibrahim Lipumba, alisema katika ilani ya CCM hakukuwa na suala la katiba wala katika hotuba ya rais aliyoitoa bungeni hakukuwa na suala hilo, hivyo kuna haja ya kuwa na mshikamano katika suala hili, kwani bila hivyo nchi inaweza kuingia kwenye machafuko.
Mwandishi mkongwe, Jenerali Ulimwengu, alisema katiba iliyopo msingi wake ni falsafa za Waingereza na hata mabadiliko yaliyokuwa yakifanywa mara kwa mara hayakuwashirikisha wananchi.
“Baada ya uhuru hakukuwa na mchakato wa kuwaweka wananchi pamoja na kuona jinsi gani ya kuendesha nchi yao, zaidi walishirikishwa viongozi wa chama na wataalamu wachache kunyofoa na kurekebisha katiba hiyo.
“Katika hili ningependa tujipe muda zaidi wa kujenga Katiba mpya na si kuvipa nguvu vyama vya siasa na kazi ya tume iwe ya kuratibu mijadala tu,” alisema.
Ulimwengu alisema haoni kama kuna gharama kubwa ya mchakato wa uundwaji wa Katiba ukilinganisha na machafuko yanayoweza kutokea baadaye.
Alibainisha kuwa kinachotakiwa ni kuona wananchi wa kawaida wanakuwa na madaraka juu ya maisha yao na matumizi ya rasilimali zao badala ya watawala kuendelea kuishikilia mifumo ya kikoloni.
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi Wanawake (TAMWA), Ananelia Nkya, alisema kwa muda mrefu amekuwa akifuatilia mijadala hiyo katika vyombo vya habari, lakini suala la ushirikishwaji wa wanawake umekuwa mdogo ukilinganisha na wanaume.
Mkurugenzi huyo aliitaka serikali kuhakikisha inawekeza katika kuwawezesha wananchi kujua ni nini kilichopo katika Katiba iliyopo kwanza, kwa kutumia redio, televisheni na magazeti inayoyamiliki na vyombo vingine vya habari.
Mchangia mada mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Aristoto Steven, alisema viongozi wa nchi hii kwa muda mrefu wamekuwa wagumu wa kusikia, hivyo kwake anaona midahalo, makongamano na semina vinaweza kuwa bure.
Kutokana na sababu hiyo, Steven alipendekeza vyama vya siasa kwa kushirikiana na wananchi kushinikiza suala hilo kwa kuitisha maandamano kwani lugha nyepesi na za kubembeleza haziwezi kuleta Katiba mpya.
Dk. Azaveri Lweitama, alisema hakuna haja ya kuwazodoa viongozi ambao awali walionekana kupinga uundwaji wa Katiba mpya, pia hoja ya Mnyika ya mjadala huo kwenda bungeni na kuweza kupigiwa kura, anauunga mkono ili wananchi wajue ni kina nani hasa wanaopinga ili wapate pa kuanzia.
Profesa Lwaitama alisema kuwapo kwa Waziri Kombani katika kongamano hilo la jana ni kielelezo tosha cha kuendelea kujadiliwa kwa mchakato wa katiba.
Katika kongamano hilo, lililoanza majira ya saa nne asubuhi na kumalizika saa nane, wananchi wengi waliohudhuria walionekana kuunga mkono hoja ya kuundwa kwa Katiba mpya na si kurekebishwa wala kuwekwa viraka, sababu kubwa ikiwa katiba zote zilizorekebishwa huko nyuma hazikushirikisha wananchi.
 
Profesa Shivji alisema ni bora suala hili likabakia mikononi mwa wananchi ili walijadili kwa kina na ikiwezekana kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kuliko kulipeleka bungeni ambako CCM inaweza kutumia wingi wa wabunge kulinda masilahi yake.
Tahadhari hiyo ya Shivji, ilitokana na hoja ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), kuonyesha wasiwasi wake na kutaka suala hilo lipelekwe bungeni kwanza ili lifanyiwe marekebisho kwenye baadhi ya vipengele vya sheria, ibara ya 98, inayosema Bunge ndilo lenye mamlaka ya kubadilisha Katiba.
Akijibu hoja hiyo, Shivji alisema Bunge halina uwezo wa kupinga Katiba na kwenye Katiba hakuna sheria inayopinga mjadala wa kitaifa kama huo.

Tatizo la professa Shivji ni kushindwa kubainisha ya kuwa bila ya bunge kurekebisha sheria na kuruhusu mchakato huu wa katiba mpya kujikita kwa nguvu ya sheria tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.........lazima suala lote hili likaundiwa sheria na mengineyo yote yafuate...................................
 
Na wewe tatizo lako nini?
 
Back
Top Bottom