Katika hali inayoonyesha kuwa serikali ya CCM sasa imekosa legitimacy (uhalali) kwa umma,na imechanganyikiwa Leo imefanya kitendo kingine cha aibu ya karne.
Kwa kutumia jeshi la polisi wamepiga wananchi mabomu katika maeneo mengi ya kampeni zake huko kusini bila sababu za msingi wakati wananchi hao wakiwa kwenye mikutano halali kabisa ya kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu ili kuvuruga mikutano halali ya mgombea wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu.
Ukiachilia Somanga, hali ya kupigapiga wananchi waliokuwa wakimsubiri Lissu imefanyika maeneo mengi mikoani humo na kusababisha taharuki na mshangao mkubwa kutoka kwa wananchi ambao walikuwa na hadhara halali ya kusikiliza mgombea kama ambavyo wananchi wa maeneo mengine ya nchi wamepata fursa.
Lisu alikuwa na ziara katika maeneo ya Masasi, Newala, Kibiti, Mkuranga, Tandahimba n.k
Ukiachilia mbali Lindi ambapo mkutano umefanyika, hata hivyo Mikutano ya Lissu imefanyiwa vurugu kubwa na jeshi la polisi ambapo wananchi wamevurumishiwa mvua ya mabomu ili kuwaondoa wasimsikilize Lissu
Kwa kweli hili linashangaza sana, CCM wana hofu gani na watu wa kusini?-Wao ndo waliwaumiza kwa kupora korosho zao, kuwapiga kwa sababu ya gesi yao na kuharibu zao lao la ufuta, Sasa wanajaribu kuficha aibu yao kwa kuzidisha uonevu juu ya uonevu kwa watu wa kusini
Msikilize Tundu Lissu hapa akielezea mkasa wa piga piga iliyowakumba wananchi wa maeneo mbalimbali siku ya leo ili kuwatimua wasisikilize mkutano wake.
HIVI NI LINI SERIKALI YA CCM ITAACHA UONEVU DHIDI YA WATU WA KUSINI?