Hongera Ali Kiba na hongera zaidi kwa Team Kiba kwani mmeonesha namna ya kuunga mkono msanii. Mmempigania wakati wote hadi kufikia mafanikio haya.
Ikumbukwe kwamba ndio kwanza Kiba ana miezi kumi na moja tangu arejee kwenye muziki na ametoa nyimbo mbili tu na video moja, lakini tayari kakusanya Tuzo saba ambazo naweza kusema zilikuwa ngumu sana.
Kama hujui ugumu wa kuondoka ktk muziki kwa miaka mitatu na kurejea kwa nguvu hizi ndani ya miezi 11 huwezi mpongeza Kiba na Team Kiba kwa matokeo haya.
Ila kwa faida yako tu nenda kawaulize Dudubaya, Mr Nice, Q Chillah na wengineo juu ya namna ilivyo ngumu kurudi kwenye muziki na kutamba tena.
Pia napongeza mwamko mkubwa wa kuunga mkono wanamuziki wetu wenyewe, nadhani nao wataongeza bidii ili kutoangusha mashabiki wao. Ila naomba na Team za wanamuziki wengine wazuri zizaliwe.
Kuliko kuwaachia wahuni wanaojiita OSATA kuufanya huu muziki kama mali yao kwa kulazimisha kuwazika wazoefu ili game litawaliwe na chipukizi kila siku.
Wanamuziki kama Kassim Mganga wanaweza kukuliza ukisikiliza wimbo wake wa Subira alioimba na Bella kwa jinsi ulivyo mzuri kwa kuimbwa na kuandikwa, lakini miungu watu OSATA wanalazimisha apotee.
Pia, nikupongeze
nifah wangu kwa maneno mazuri ya kuanzisha uzi huu.
Ova