Watanzania mna chuki za kutisha aisee! dah!, hivi huyu Diamond kama asingekuwa anakubalika na hao wanamuziki wa Nigeria mnadhani wangekubali kushirikiana naye kwenye muziki na hivyo kupoteza muda na pesa zao chungu nzima? Acheni chuki zenu za kutisha dhidi ya Diamond.
Tusubiri tuone kama hilo tamko ni la KTMA kweli. Ni ngumu sana kwao kuadmit madhaifu yao juu ya tuzo za jana
Wewe unamkubali chibu ila basi tu unapretend hapa uko against him😀😀😀😀😀Kwani huyo diamond alikua na nyimbo gani za maana za kushindana na Mwana?
Hivi mdogo mdogo nao ni wimbo wa kusema ni wimbo bora? Afadhali nitampata wapi video yake imetulia.
Umeongea ukweli, ila hii mambo ya #mimiteamfulani inaua game...
Unavyosema account ni fake, jitaidi uonyeshe na original.
Fitina,chuki,majungu na roho mbaya havijengi!!kuweni wazi ni kipi hasa alichowakosea mpaka muendeshe kampeni ya aina hii dhidi yake!
Ni upumbavu tu Mkuu tena wa hali ya juu kumchukia Mtanzania mwenzao kiasi hiki wakati amelipaisha Taifa nje ya mipaka ya Tanzania kuliko Mwanamuziki yeyote yule nchini.
Inasikitisha sana kuona huyu jamaa anavyochukiwa bila sababu zozote zile za msingi huku akijiingizia kipato chake cha halali kabisa bila kumkera Mtanzania yoyote yule.
Eti nyimbo zake hazikubaliki kimataifa! Mataifa gani hayo wanayozungumzia wakati Kenya, Uganda, UK, US, Canada na nchi nyingine nyingi alizowahi kufika hujaza kumbi mbali mbali za muziki.
Na mbaya zaidi unakuta MTU yuko radhi ampigia kula davido wakati diamond ni mtanzania mwenzake hii inasikitisha sana kama humpendi MTU sawa lakini linapokuja swala la utaifa kwanza na uzalendo ni muhimu kuzingatia
Wamarekani hawampendi Mayweather hasa kwa tambo zake, but walikua upande wake alipopambana na pacman. Naamini somo la uzalendo bado halijafanikiwa sana.
kweli mkuu diamond bila davido asingefika alipo sasa kimataifa ila dogo ana dharau sana.
haiwezekani ushindi wa simba ukashangiliwa jangwani
ni kweli ila ni NGUMU KUMESA.
Kwa kweli sikutegemea kabisa kama watu wangekuwa na chuki kiasi hiki dhidi ya Diamond.
Hivi kibaya alichokifaya ni kipi hasa hadi watu wamchukie hivi?
Huwa napinga sana hii kauli Mkuu "Watanzania hatupendani" lakini wakati mwingine ukiona hali halisi kama kwenye huu uzi inabidi ukubali tu hali halisi ya Mtanzania kumchukia Mtanzania mwenzie kwa chuki za kutisha wakati huo huo huyo anayechukiwa hajafanya lolote lile la kustahili kuchukiwa kiasi hicho.