Yaliyojiri kwenye Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) 13 June 2015

Yaliyojiri kwenye Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) 13 June 2015

Mfumo ulitumika hauangalii ubora wa msanii wala uwezo wake check BET mfano wao wanatumia majaji kama 500 kama mnakumbuka vanessa mdee alikuwa mmoja wao mwaka jana hvi ndio huwa wanachambua nani anastahili. kwa international awards huwa kuna majaji na kuna kitu inaitwa country votes inaangaliwa umepata kura kutoka kitika nchi ngap afu kila nchi idadi fulani ya kura inakuwa point moja(ndio maana tuliwashinda wanaigeria BBA na Chanel 0 mwaka jana wangekuwa wanahesabu kura hakuna hata mtu mmoja kutoka nje ya nigeria angekuja kushinda hzo Tuzo), lakini pia huwa wanakitengo kinaitwa viewers choice award ambacho hicho ndo mashabiki huwa wanachagua. Kwa Tanzania inaonekana vyote huwa wanachagua mashabiki and let face it mwaka huu ilikuwa (jokate+wema+alikiba) ilikuwa lazima ushindi tu. Ukitumia mantiki ya kura maana yake hata leo hii ukileta Ronaldo VS Ngasa kwa Tanzania hii ngasa atashinda coz ana fanbase kubwa bongo ila sio kwamba yeye ni bora.

ngassa amshinde ronaldo hapa bongoo...?!!
aahhh wapi..sina uzalendo huoo
 
Sasa tatizo lako hasa ni nini? Wewe ulitaka nani ashinde tuzo? Na kwa nini?
Na kama vigezo ni hivyo ulivyovitaja nn hasa shauku yako ya kutaka nani awe bora kwa atarajio na matamanio yako?
Ifike mahali tuwe tunakubaliana na matokeo na kujifunza kutokana na makosa.
Washindi walishapatikana na you cant do anything abt that, cha msingi next time study the criteria, follow the criteria and your priority musician will win the awards.
Kwa vigezo vya KTMA ilikuwa ni wingi wa kura, sasa hapo huwezi kulazimisha vigezo vya Awards nyingine zitumike.
Ndio maana wengi hu feli hata exams coz hawafuati maelekezo. Wewe umeambiwa "Piga kura mara nyingi zaidi kumuwezesha Mwanamuziki umpendaye ashinde tuzo" wewe hupigi kura badala yake unaleta vigezo ambavyo havipo, sasa utashindaje?

Duh.... kaka umesema niko wrong kuhusu vanesa kuwa mmoja wa majaji ndio nimeulza hao maacademy kazi yao nin haujanijibu unaleta maelezo mengine. Anyway kwangu mimi haijalishi nani kashinda wasanii wote wanafanya kazi vizuri na wanastahili pongezi, hapo nlikuwa najaribu kueleza kwanin malalamiko yamekuwa mengi sana miaka yote kwa nchi yetu ndio nikatoa mfano wa nchi zingne namna utaratibu unaenda. Kuna tatizo hapoo!?
 
Duh.... kaka umesema niko wrong kuhusu vanesa kuwa mmoja wa majaji ndio nimeulza hao maacademy kazi yao nin haujanijibu unaleta maelezo mengine. Anyway kwangu mimi haijalishi nani kashinda wasanii wote wanafanya kazi vizuri na wanastahili pongezi, hapo nlikuwa najaribu kueleza kwanin malalamiko yamekuwa mengi sana miaka yote kwa nchi yetu ndio nikatoa mfano wa nchi zingne namna utaratibu unaenda. Kuna tatizo hapoo!?

Mimi nimekuelewa mkuu na wala sikulalamikii. Ila najaribu kukupa changamoto pia kwamba inabidi sisi mashabiki tujifunze kwanza Ni nini vigezo vya Award husika, kwa mfano kwa KTMA ilikuwa ni "Mshindi anapatikana kwa Wingi wa Kura za Mashabiki" na KTMA walikuwa wanarudia rudia sana kwenye Radio TV mitandao ya kijamii magazeti nk. sasa leo hii hao wanaolalamika wanalalamika basing on what?
 
Duh! Ndio maana walienda baada ya nominees kutangazwa si eti eeeh!?

Watu walipendekeza nani na nani waingie kwenye tuzo kwa njia ya sms kazi ya wana academy ni kuchambua wote walipendekezwa na kupitisha majina matano kila kipengele baada ya hapo ndio wanapigiwa kura kumpata mshindi
 
Hii sio haki hata kidogo! Mbona ananyanyaswa hivyo? Au kwasababu sio mtanzania? Tuzo ya kibakuli ya mtunzi bora angepewa yeye na nyimbo yake ya nani kama mama
 
Hii sio haki hata kidogo! Mbona ananyanyaswa hivyo? Au kwasababu sio mtanzania? Tuzo ya kibakuli ya mtunzi bora angepewa yeye na nyimbo yake ya nani kama mama

Kigezo kikuu cha mshindi wa KTMA (Kilimanjaro Tanzania Music Awards) ilikuwa ni wingi wa kura za mashabiki kwa msanii aliyekuwa nominated kwenye kila category, Je wewe ulipiga kura? Kama hukumpigia kura basi jilaumu mwenyewe, na kama ulipiga kura basi kura yako haikutosha kumfanya awe mshindi
KUMBUKA KIGEZO CHA MSHINDI WA KTMA KTK KILA CATEGORY NI WINGI WA KURA ZA MASHABIKI.
ACHA KULALAMIKA FUATA VIGEZO NA MASHARTI YA KTMA
Ni hayo tu.
 
na ali kiba basi anyang'anywe kama sitti mtevu

Huyo Sitti Mtemvu alinyang'anywa baada ya kukiuka vigezo na masharti ya Miss Tanzania ktk kigezo cha Umri.
Ushindi wa Alikiba umezingatia vigezo na masharti yote ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) kwa maana ya

1. Alikiba alikuwa mmojawapo wa nominees ktk kila category aliyoshinda.

2. Alikiba alipigiwa kura na mashabiki kumuwezesha kushinda tuzo.

Vigezo na Masharti vilizingatiwa hivyo tuzo alizoshinda Alikiba ni halali yake.

Jipange Mwakani kupiga kura za kutosha kwa mwanamziki unayempenda.
 
Hahahahaaa, huyu jamaa sasa kazidi kwa matamkoz...siku hizi anayaita LE MUTUZ EXTRA STRAIGHT LIVE TALK!
Nimemuona tokea jana, na tusubiri tuone....
Nimesoma haya malalamiko ya le mutuz nikajiuliza huwa haonagi makada wanavyokuwa wasimamizi wa uchaguzi?
 
Back
Top Bottom