Yaliyojiri kwenye Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) 13 June 2015

Yaliyojiri kwenye Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) 13 June 2015

Nilisema mjiandae kwa dhoruba kali ndio tumerudi hivyo, yametimia.
Halafu sioni mantiki ya kuweka tuzo zote kwa ujumla ilhali kipindi diamond anakusanya tuzo zote hizo Ali Kiba alijipa likizo ya muziki.
Sasa karudi tuwapambanishe kwa wakati huu.

mbona husemi Alikiba alitangulia kuanza muziki?

Anyway 25-8 = ???
 
Diamond hivi karibuni alitoa kauli kuwa "Ali Kiba anakula makombo yake" akimaanisha uhusiano wa Ali Kiba na Jokate Mwegelo eti Jokate ni makombo ya Diamond!

Hilo ni tusi na alipaswa kuomba radhi na kuonyesha kujutia kauli yake hiyo! Hivi mtu na akili yake timamu tena kioo cha jamii kwenye nchi ya maadili unatoa kauli kama hiyo?

Hamuwezi amini lakini hata hizo tuzo mbili ilikuwa ni kumhurumia tu kwani hakustahili! Ni lazima afunzwe adabu!

Tukianza kutoa lugha chafu kama hizo hatujengani kisanii! Jokate naye ni msanii na hapaswi kudhalilishwa na mwanaume kisa eti alimpa penzi!

Hapana huyu ni lazima ajirudi na ajuwe kuwa yeye ni kioo cha kujenga jamii na siyo kuibomoa! Nadhani hilo ni onyo kali kwake!

Watanzania hawapendi Maendeleo.
 
Kigezo kikuu cha Kushinda KTMA ni wingi wa kura, je wewe ulipiga kura kuziwezesha hizo nyimbo zako uzipendazo kushinda Tuzo?

we nae na haka ka kigezo kako ka kupiga kura umekakomaliaaaa!!! kwahiyo leo ngassa akimshinda kwa kura maradona ndo mana ake ye ni bora?? hua kuna na kura za maruhani wakat mwingine mazee,, na btw hawa majaji walikuja kufanya nini baiskeli wewe?
 
Ni kweli kabisa mdomo wake ndo umemponza

Huyu ni mdhalilishaji wa kwanza wa wanawake.
Tena aache kumdhalilisha baba yake mzazi kwa kumsema sema kuwa alimterekeza.Ugomvi wa mama na baba ni siri sana.
 
Okay I see. Kumbe hivi ndio vilikuwa vigezo vya kumpata mtunzi bora, mtumbuizaji bora na wimbo bora tuzo za KTMA? Death of bongo fleva.

Bongo flavour will never die.
Wasanii wanaotaka kuiua watakufa wao.
 
Acheni timu zisizokua na maana mtawapoteza hao wasanii..

Ali Kiba anafurahia sana hili bifu maana linamlipa ila atambue Dai akishuka yeye atapotea Kabisaa kwenye game.

Ray alianzisha ligi na Kanumba. Matokeo mnayaona sasa.

Tuache ushabiki #team_sapoti_mzikimzuri
 
Absolutely right. ..ligi ianzie hapo.

+Ha haa haa 😀😀😀
yaan nyie wajanja kwa hiyo mnataka ligi ianzie mnapopataka nyie? Hiyo sio fair!

+ligi ya mond na Kiba imeanza toka bifu lao lianze haya toka bifu lianze Mondi kachukua tuzo kibao! Hizo hamzihesabu?
 
Asante sana baby wangu Mdakuzi. Pia wewe nakupongeza maana ni mmoja kati ya Team Kiba ambao tumempigania sana Kiba humu JF na nje ya JF.

Hakika sasa tunayaona matunda ya umoja na mshikamano wetu. Ni jukumu letu sote kuhakikisha mshikamano huu unadumu na tunazidi kutoa support zaidi kwa King wetu Kiba.
 
Mmmmmmh hizo tunzo kichefuchefu mno! Ally kiba hakustahili kabebwa sana! Wimbo mmoja categories zote? Nasseb yuko juu sana

Kwani huyo diamond alikua na nyimbo gani za maana za kushindana na Mwana?
Hivi mdogo mdogo nao ni wimbo wa kusema ni wimbo bora? Afadhali nitampata wapi video yake imetulia.
 
Kwani huyo diamond alikua na nyimbo gani za maana za kushindana na Mwana?
Hivi mdogo mdogo nao ni wimbo wa kusema ni wimbo bora? Afadhali nitampata wapi video yake imetulia.

best ndo nn ht kuntag si nlikwambia ngosha kajaaa....?!!!
mbaya weweee...!!!
 
nyie nao na huu msemo wa"huko kwa wenzetu" mnaboa sana shenzy taip.. cheki na kingereza chako cha huko kwa wenzetu.. mnalala na makaratasi kudadadensa


mkuu
sijaona sababu ya kuwaka kwako. Mimi natoa facts tuu.

Unaweza ukampigia Davido na wengine tuu .

Choice is yours...
 
Avemaria
Hahahahaaa, eti walitaka diamond ashinde ila alivyoshinda Kiba ndio ikawa nongwa. Huyo diamond asubiri tuzo za taarab mwakani huko apambane na mzee Yusuph sio King Kiba. Tena marufuku kumpambanisha King wetu na waimba taarab...lol
 
Hahahahaaa, umeua mkuu tajirijasiri Itabidi umtungie King wimbo mmoja matata maana naona una kipaji kizuri sana cha kutunga.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom