Pre GE2025 Yaliyojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Leo ni siku iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania. Siku ya maandamano ya wananchi wakiongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Chama hiko; amefafanua kwamba lengo la maandamano hayo ni kupinga wimbi na matendo mabaya yanayoendelea nchini ya utekaji nyara, kupotea kwa watu na mauajo ya raia. Wananchi wamelinyooshea kidole jeshi la polisi kutokana na mazingira ya upoteaji wa watu. Watu wengi wameripotiwa kupotea baada ya kuitwa vituo vya polisi.

======

Siku ya waliyosema chadema kufanya maanadamano kwaajili ya kupinga utekaji na watu kuuliwa na watu wasiyojulikana imefika,

Tangazo hili lilitolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Septemba 11, 2024, ambapo alisema wataingia barabarani endapo wanachama wao waliopotea hawatarudisha na kama serikali haitawajibika ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa viongozi husika.

Ratiba ya maandamano ilitolewa Jumamosi tar 21 Septemba 2024 baada ya kuwa serikali haijatekeleza takwa lolote kati ya yale yaliyotolewa na CHADEMA kuhakikisha kuna uwajibikaji.

Fuatilia uzi huu kwa matukio ya moja kwa moja kwa siku ya leo na yatakayojiri kwenye maandamano hayo.


=======UPDATES======
20240923_082553.jpg

Magomeni muda huu. Naelekea katikati ya mji nifike Mnazi Mmoja

Asubuhi imeanza kwa taarifa ya Lissu kuzingirwa na polisi na kutakiwa kwenda kuripoti katika ofisi ya RCO Kinondoni, ambapo amekubali kwenda kuitikia wito.

Lissu 2.jpg

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameeleza kupitia mitandao ya kijamii kuwa tangu jana usiku mpaka asubuhi ya leo Septemba 23, 2024 Jeshi la Polisi limefunga barabara zote zinazoelelea nyumbani kwa mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe.

Chama hicho kimeeleza kuwa watumiaji wote wa barabara hiyo wanasimamishwa na kukaguliwa, wakiulizwa kama wanaenda kwenye maandamano.

Chade.PNG


CHADEMA wameripoti kuwa mapema leo Jeshi la Polisi wameingia nyumbani kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara kisha kuondoka nae bila kusema wanampeleka wapi.

CHADEMA lISSU.png

CHADEMA imeripoti kuwa Jeshi la Polisi limemzuia Dr. Lilian Mtei, Mke wa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe akiwa anatoka nyumbani kwake Mikocheni, Dar es salaam.


WAKILI WA CHADEMA: TUNDU LISSU AMEKAMATWA AKIWA NYUMBANI KWAKE TEGETA
Wakili wa Chadema, Hekima Mwasipu amesema Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu amekamatwa na polisi asubuhi ya leo Jumatatu, Septemba 23, 2024.

“Lissu amekamatwa nyumbani kwake Tegeta na amepelekwa Kituo cha Polisi Mbweni na mimi kama wakili niko njiani nakwenda huko kujua sababu za kukamatwa kwake

MAKONDA: KAKA YANGU MBOWE KUMBE UPO ARUSHA NA HAUSEMI
Wakati Chama Cha Demokrasia na Maendelei Chadema kikitangaza kufanya Maandamano ya amani leo Jijini Dar Es salaam chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amechapisha mtandaoni mwake akisema anazo taarifa kuwa Mwenyekiti Mbowe yupo Arusha na hivyo kumualika ofisini kwake Jijini Arusha. Makonda ameandika "Kaka yangu Mbowe kumbe umeingia Arusha na hausemi. Karibu Ofisini basi ukiamua Kutoka"

Makonda.PNG

MBOWE AJITOKEZA MAGOMENI, AKAMATWA NA POLISI

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amekamatwa na Polisi eneo la Magomeni, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 23, 2024.

Kabla ya Mbowe kukamatwa, alifika eneo hilo akiwa na gari dogo, kisha kuanza kuzungumza na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Mbowe, wameamua kuwekea mkazo suala la maaandamano, baada ya maombi ya mahitaji, ikiwemo kutaka kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, viongozi waandamizi wa ulinzi na usalama kama sehemu ya uwajibikaji.


Baba mlezi wa Deusdedith Soka amejitokeza katika maandamano ya amani Ilala Sokoni. Azungumzia kupotea kwa Soka.


Jeshi la Polisi likiendelea kuwakamata waandamanaji maeneo ya Ilala Boma.

JESHI LA POLISI LATHIBITISHA KUWAKAMATA WAANDAMANAJI 14 IKIWEMO VIONGOZI WA CHADEMA
Jeshi la Polisi limetoa taarifa rasimi ya kuwakamata watu 14 ikiwemo baadhi ya Viongozi wa Chadema, Mwenyekiti Freeman Mbowe, Lissu na Lema, ambapo wamedai kuwa viongozi hao wamekamatwa kufuatia mpango wa maandamano.

Wanawashikiria kwa sasa wanahojiwa kwa ajili ya hatua za kisheria.

Kamanda Muliro ametangaza kuwakamata viongozi mbalimbali wa CHADEMA ikiwemo Freeman Mbowe, Tundu Lissu pamoja na Godbless Lema.


Waliokamatwa.jpg
 
Back
Top Bottom