Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hapana mkuu ukweli ni kwamba maandamano huchukuliwa ni kama vurugu kwa watanzania waliyo wengi huona hivyo, hasa wanapoona na polisi wametanda ndipo watu wanapoamua kukaa nyumbani kukwepa hizo vurugu. Hivyo hiyo tunayoita mikwara ya polisi inafanya kazi.
 
Kenya maaskari walikuwepo, watu sio waoga na watu waliandamama

Huko Nchi za afrika kaskazini kwa waarabu maaskari walikuwepo (arab spring) na watu waliandamana mpaka viongozi walitoka madarakani.


Sri Lanka maaskari walikuwepo, watu waliandamana mpaka viongozi walitoka madarakani


Bangladesh maaskari walikuwepo, watu waliandamana mpaka viongozi walitoka madarakani.


Maaskari kuwepo Tanzania sio changamoto.


Narudia tena
Hakuna mtu muoga sana kama Mtanzania, hata mimi ni muoga sana.
 
We ulisha wahi kuona wapi commander wa kikosi anaka frontline?
Na pia hata kama haendi mstari wa mbele lakini huwa hasemi kuwa atakuwepo kama alivyosema Mbowe ambaye mwishowe haonekani.
 
Uki
Ukifika wakati sahihi watu wataandamana tu, nakuhakikishia maandamano yatakuwa makubwa na yenye mafanikio kuliko unavyodhani.

Ni ngumu chama cha siasa kuanzisha maandamano na yakafanikiwa.
Wanasiasa hawajawahi kuwa upande wa wananchi, hawaaminiki
 
Huo wakati labda kije kizazi cha 2010 au 2020.

Au ccm wawe na mgogoro na vyombo vya ulinzi na usalama, labda maaskari waitoa ccm systematically au wawapindue.



Hiki kizazi ni kioga, hata mimi ni muoga 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…