Kwenye suala la kutafuta haki kuna njia nyingine nyingi tu mana kuna majukwaa mengi ya UN yanayosikiliza na kusimamia haki za binadamu wote kwa kwa ujumla.
Kwanini watu wasitumie njia ya kuandaa midahalo ya kujadili changamoto za nchi zao na kuzifikisha katika manukwaa ya kimataifa pale inapobidi?
Bora kutumia njia ya migomo katika utendaji ili kupata suluhu ya matatizo katika nchi kuliko kuandamana kitu ambacho mwisho wake tunajiandalia njia za machafuko wenyewe.
Kwanini kama ni kupata haki ya kubadili katiba wananchi wenyewe wasiwe katika mstari wa mbele kwenye kuidai na isipopatikana basi ifuatiwe na migomo katika utendaji wa shughuli za uzalishaji kitu ambacho ni lazma Serikali iguswe moja kwa moja mana haiwezi kujiendesha bila ya fedha zinazotokana na uzalishaji?
Kama ni suala la kupanda kwa gharama za maisha kutokana na kodi na ushuru kwanini wafanyabiashara wasifanye migomo mana kwenye democracy kuna haki ya kugoma ikiwa kuna ukandamizaji unaendelea.
Suala la maandamano si swala la kulisifia na kulipokea kwa sherehe hivyo tizameni outcomes zake kuna Vifo vya raia wasio na hatia, wamama wazee na watoto wanaweza kuwa waathirika wakubwa.
Be rational, tumia njia yenye maumivu kwa pande zote ikiwa ni lazima Serikali itaumia na wananchi wataumia kwa muda mfupi ila haki lazma ipatikane mana ndiyo inaweza kuwa suluhisho la pekee kwa migomo hiyo hapa suala usalama ni muhimu.