Pre GE2025 Yaliyojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wataalamu,
Nikishasema na nitarudia tena ,hawa jamaa huwa wanashinda kwenye mitandao ya kijamii kueneza chuki na siasa ambazo hazina kichwa wala miguu.

Wanapokuwa kwenye mitandao huwa wanajiamisha kuwa wanakubalika kwenye mioyo ya Watanzania kumbe sio kweli hata kidogo.

Kitendo cha hawa makamanda uchwa kushindwa kuendeleza mapambono yako ya kwenye mitandao na kuungana na wapuuzi wenzao kwenye maandamano uchwara ni ushahid tosha kuwa hiki chama ni famba (paper tiger).

Ni wakati muafaka kwa wale angalau wanayo akili ya darasani ambao wanahesabika (wasomi ) kama mzee Lissu kuangalia uhalisia wa hiki chama.
 
Hakuna mtu muoga sana kama Mtanzania, hata mimi ni muoga sana.

Hata hao askari wenyewe ni waoga tu. Kama wasingekuwa waoga wangekataa kutumika na ccm. Au wangekaza/wangekataa kukubali maagizo toka juu.

Bado hakijatokea kizazi ambacho kipo tayari kupigwa, kufungwa, kufa juu ya masuala ya kisiasa.



Hakuna vijana wa kufatilia au kutaka kuhusika na masuala ya aina hiyo.
Vijana wako bize na mipira, miziki, mitandao,mikeka ya kubeti, minguvu ya kiume, mapenzi, kukata mauno, matamasha, tamthilia na misambwanda


Narudia tena



Hakuna mtu muoga sana kama Mtanzania, hata mimi ni muoga sana.
Hata Chadema ni waoga sana ndio maana HAWAWEZI kuandamana Leo.
 
Leo ni siku iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania. Siku ya maandamano ya wananchi wakiongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Chama hiko; amefafanua kwamba lengo la maandamano hayo ni kupinga wimbi na matendo mabaya yanayoendelea nchini ya utekaji nyara, kupotea kwa watu na mauajo ya raia. Wananchi wamelinyooshea kidole jeshi la polisi kutokana na mazingira ya upoteaji wa watu. Watu wengi wameripotiwa kupotea baada ya kuitwa vituo vya polisi.

======

Siku ya waliyosema chadema kufanya maanadamano kwaajili ya kupinga utekaji na watu kuuliwa na watu wasiyojulikana imefika,

Tangazo hili lilitolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Septemba 11, 2024, ambapo alisema wataingia barabarani endapo wanachama wao waliopotea hawatarudisha na kama serikali haitawajibika ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa viongozi husika.

Ratiba ya maandamano ilitolewa Jumamosi tar 21 Septemba 2024 baada ya kuwa serikali haijatekeleza takwa lolote kati ya yale yaliyotolewa na CHADEMA kuhakikisha kuna uwajibikaji.

Fuatilia uzi huu kwa matukio ya moja kwa moja kwa siku ya leo na yatakayojiri kwenye maandamano hayo.


=======UPDATES======
View attachment 3103938
Magomeni muda huu. Naelekea katikati ya mji nifike Mnazi Mmoja

Asubuhi imeanza kwa taarifa ya Lissu kuzingirwa na polisi na kutakiwa kwenda kuripoti katika ofisi ya RCO Kinondoni, ambapo amekubali kwenda kuitikia wito.


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameeleza kupitia mitandao ya kijamii kuwa tangu jana usiku mpaka asubuhi ya leo Septemba 23, 2024 Jeshi la Polisi limefunga barabara zote zinazoelelea nyumbani kwa mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe.

Chama hicho kimeeleza kuwa watumiaji wote wa barabara hiyo wanasimamishwa na kukaguliwa, wakiulizwa kama wanaenda kwenye maandamano.

CHADEMA wameripoti kuwa mapema leo Jeshi la Polisi wameingia nyumbani kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara kisha kuondoka nae bila kusema wanampeleka wapi.

CHADEMA imeripoti kuwa Jeshi la Polisi limemzuia Dr. Lilian Mtei, Mke wa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe akiwa anatoka nyumbani kwake Mikocheni, Dar es salaam.

Mbona mwenyewe kashasema wamemueleza wanampeleka wapi.
 
kumeanza kuchangamka
20240923_102045.jpg
 
Ipo hivi, CHADEMA walitangaza maandamano wakakaa kimya na kuendelea na shughuli zao za kila siku. Lakini tangu siku ile ya kutangazwa maandamano Polisi wamekuwa wakizunguka huku na kule mitaa yote ya Dar es salaam na hata Mikoa mingine.
Wamebeba silaha nzito nzito, mbwa, magari ya washawasha nk. Baadhi ya polisi yawezekana wametoka mikoa mingine.
Ebu tujiulize kidogo;
*Katika mkasa huu, nani mwoga zaidi?
*Nani ametumia gharama kubwa zaidi?
*Nani amedharaulika zaidi?
*Kimataifa nani amajijenga zaidi na nani amedharaulika zaidi?
*Kwa tathmini ya haraka, CHADEMA wana akili zaidi na wamejijenga zaidi kuliko watesi wao.
Gharama zipi? ...gharama za polisi ni kodi zetu wananchi
 
Kwani lengo la Chadema kutangaza maandamano ilikuwa ni Polisi kukusanyika Dar? Chadema walisema ije mvua, lije jua wataandama. Sasa sababu za eti Polisi wamekusanyika zinatoka wapi?
Polisi wanasaidia kuandamana mikoa yote na hasa Dar huku wamebeba mizigo mizito huku wamevaa mavazi yanayolowesha pumbu kwa jasho! Nashauri chadema watangaze kuendelea na maandamano Dar kwa siku 30 na baadaye watangaze kuhamia Mwanza. Arusha, Mbeya. Yaendelee kucheza shere! hayo mabumunda
 
Back
Top Bottom