Pre GE2025 Yaliyojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Leo ni siku iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania. Siku ya maandamano ya wananchi wakiongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Chama hiko; amefafanua kwamba lengo la maandamano hayo ni kupinga wimbi na matendo mabaya yanayoendelea nchini ya utekaji nyara, kupotea kwa watu na mauajo ya raia. Wananchi wamelinyooshea kidole jeshi la polisi kutokana na mazingira ya upoteaji wa watu. Watu wengi wameripotiwa kupotea baada ya kuitwa vituo vya polisi.

======

Siku ya waliyosema chadema kufanya maanadamano kwaajili ya kupinga utekaji na watu kuuliwa na watu wasiyojulikana imefika,

Tangazo hili lilitolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Septemba 11, 2024, ambapo alisema wataingia barabarani endapo wanachama wao waliopotea hawatarudisha na kama serikali haitawajibika ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa viongozi husika.

Ratiba ya maandamano ilitolewa Jumamosi tar 21 Septemba 2024 baada ya kuwa serikali haijatekeleza takwa lolote kati ya yale yaliyotolewa na CHADEMA kuhakikisha kuna uwajibikaji.

Fuatilia uzi huu kwa matukio ya moja kwa moja kwa siku ya leo na yatakayojiri kwenye maandamano hayo.


=======UPDATES======
View attachment 3103938
Magomeni muda huu. Naelekea katikati ya mji nifike Mnazi Mmoja

Asubuhi imeanza kwa taarifa ya Lissu kuzingirwa na polisi na kutakiwa kwenda kuripoti katika ofisi ya RCO Kinondoni, ambapo amekubali kwenda kuitikia wito.


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameeleza kupitia mitandao ya kijamii kuwa tangu jana usiku mpaka asubuhi ya leo Septemba 23, 2024 Jeshi la Polisi limefunga barabara zote zinazoelelea nyumbani kwa mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe.

Chama hicho kimeeleza kuwa watumiaji wote wa barabara hiyo wanasimamishwa na kukaguliwa, wakiulizwa kama wanaenda kwenye maandamano.

CHADEMA wameripoti kuwa mapema leo Jeshi la Polisi wameingia nyumbani kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara kisha kuondoka nae bila kusema wanampeleka wapi.

CHADEMA imeripoti kuwa Jeshi la Polisi limemzuia Dr. Lilian Mtei, Mke wa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe akiwa anatoka nyumbani kwake Mikocheni, Dar es salaam.

Kufanikiwa kwa vurugu ni mtaji wa pesa ndefu wa Mbowe na wenzake kutoka kwa taasisi za kidemokrasia za Ulaya na Marekani.

Watoto wa masikini wa nchi hii wanageuzwa mitaji na wafanyabiashara hawa wenye roho zilizojaa ukatili na ubinafsi.

Hawa ni wa kusikilizwa na kupuuzwa. Kifo cha Marehemu Kibao kisiwe ndio sababu ya watu kuacha kuzalisha mali na kufikira kufaidika na fursa za kiuchumi na kwenda kuvunjwa miguu na hao FFU.
 
Nini husumbuwa makonda,maana ana kihere here,kila kitu anataka kutia pua.
 
Hakuna cha chadema wala nini, hali ngumu mtaani inatutesa watanzania wote.


Tuseme ukweli tu 🤣
Sisi watanzania ni waoga mno, hata mimi ni muoga.



Mimi ni Muoga, wewe je?
Tukiandama hiyo hali ngumu inaisha? Nnihakikishie hilo niingie mtaani!!!

Ila unipe picha yako ili maisha yakiendelea kuwa magumu nisipate shida ya kukutafuta!! Ahahahahaha!!!
 
M
🤣🤣🤣🤣🤣
Hakuna cha kuupiga mwingi wala nini!

Tuseme ukweli tu 🤣

Sisi watanzania ni waoga mno, hata mimi ni muoga.



Mimi ni Muoga, wewe je?
Mimi sio muoga.
Ila Mbowe na Lissu hawawezi kunifanya niwe serious.
Kulia mzee wa Gia ya Angani.
Kushoto mzee wa MIGA.
🤣🤣 Hawapo serious kabisa na maslahi ya watanzania hawa wazee wa drama.
 
Back
Top Bottom