Pre GE2025 Yaliyojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Leo kulipaswa kuwa na maandamano ya Chadema jijini Dar es Salaam.
Huko mtandaoni tunaona watu kadhaa wakikamatwa ila sijapenda kabisa UPENDELEO MKUBWA WANAOUFANYA POLISI.
-. Mwenyekiti Mbowe amekamatwa na kuingizwa kwenye V8 anapigwa AC
-. Mtoto wake Nicole naye amekamatwa, ameingizwa kwenye Land Cruiser anapigwa AC
-. Lakini wananchi wa kawaida wamekamatwa wamelazwa kifudifudi nyuma ya Defender za polisi wakipogwa na jua kali.

KAMA NI KUTUKAMATA WOTE TUNGEWEKWA KWENYE AC, SIO VIONGOZI WANAKULA AC WANANCHI WANAPIGWA JUA
Kumbe wameandamana, wenzako wanasema hakukuwa na waamdamanaji!
 
Ila hii Manchester United ya mwaka huu sijui kama itapona kushuka daraja. Mechi 5 imedondosha point 8 na bado hajakutana na wale top 5 kila mwaka. Kimahesabu imeshashuka daraja (5X3)x2=30(Home and Away)+8(zilizokwisha dondoka)=38. Lengo la hizi hesabu ni kuwatahadharisha mashabiki wote wa Man U mjiandae kisaikolojia
Acha huu utoto dogo, kila uzi unapost huu ujinga!
 
Huku ni kujitekenya na kucheka mwenyewe.

Hiki kilichotokea leo Dunia nzima ilijua kitatokea, unext level wa CHADEMA unatokea wapi?

Watanzania kuogopa kuandamana baada ya kuwaona POLISI wametanda barabarani ni suala la kuisifia CHADEMA?

Hili ni suala la kuisikitikia CHADEMA, nguvu yao ya ushawishi haijai hata kwenye kisoda.
Hivi mkiwa mbogamboga akili huwa zinajaa fungus eti eh! Badala ya kujisitia kwa kuwa na nchi ya hovyo unabwabwaja kama ngedere mwenye mimba ya nyani!!
 
Haya yatakuwa maandamano endelevu....
Kila wiki..Siku Kama ya leo..Viva Tanganyika
 
Leo kulipaswa kuwa na maandamano ya Chadema jijini Dar es Salaam.
Huko mtandaoni tunaona watu kadhaa wakikamatwa ila sijapenda kabisa UPENDELEO MKUBWA WANAOUFANYA POLISI.
-. Mwenyekiti Mbowe amekamatwa na kuingizwa kwenye V8 anapigwa AC
-. Mtoto wake Nicole naye amekamatwa, ameingizwa kwenye Land Cruiser anapigwa AC
-. Lakini wananchi wa kawaida wamekamatwa wamelazwa kifudifudi nyuma ya Defender za polisi wakipogwa na jua kali.

KAMA NI KUTUKAMATA WOTE TUNGEWEKWA KWENYE AC, SIO VIONGOZI WANAKULA AC WANANCHI WANAPIGWA JUA
Mbowe anakula kilainiiiiii, wajinga ndio waliwaooo, siasa nayo ni kazi pia kama kazi zingine
 
😂😂😂
Kwahiyo mlitaka kutuponza Watanzania, lengo lenu lilikuwa kutukutanisha na POLISI barabarani?

Kwahiyo siku nyingine tukisikia CHADEMA wamehitisha maandamano Watanzania tupuuzie, sio?
Maana lengo lenu sio raia wa kawaida waandamane, mnataka POLISI waandamane. Si ndio?
Chadema wakiitisha maandamano walio wa Chadema wataitika, ila kwa case ya leo ushiriki wa polisi kutoka kila pande ya nchi hii kutaka kuja kutupiga na kutuumiza imekuwa ni blessing in disguise kwetu.
 
hakuna mtu muoga kama mbowe ila mjanja sana anawatanguliza nyumbu wasio na akili waende barabarani yeye hata kulala kwake kaogoma mhuni sana mbowe
Wewe ni mjinga! Huwezi panga maandamano au mapinduzi halafu ukalala kwako!
Hata Hayati Karume usiku wa Mapinduzi hakulala kwake,
Mbowe amewazidi maarifa Polisi kwani ameweza kufika eneo la tukio na tayari amefikisha ujumbe wake kwa Dunia!
Ameonyesha hawakuwa na ajenda mbaya dhidi ya Serikali , maana amesisitiza maandamano yao ni ya amani kumpinga utekaji, mauaji na uminyaji wa demokrasia.
Serikali ya Rais Samia ndiyo inadhalilishwa machoni pa Dunia kwa kukosa uvumilivu na matumizi ya nguvu kupita kiasi.
 
Yani hata wale wafanyakazi wa makao makuu ya chadema pia wamemsaliti mwenyekiti wao maana yupo peke yake
Kelele tu kwenye mutandao ikifikia siku ya maandamano aaaah wapo wavuvi camp wanatoa hangover
Watanzania kitu wanachoweza umbea ,fitina na majungu ila vitendo sifuri
 
Back
Top Bottom