Pre GE2025 Yaliyojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndugu zangu Watanzania,

Soma hapa
Screenshot_20240923-154507_1.jpg
 
🤣
Mimi ndio Muoga kweli kweli. Nishapigwa mabomu ya machozi, maji ya kuwashawasha, nikakoswakoswa na risasi. Nikaamua kuwa muoga 🤣🤣🤣.


Mimi ni Muoga sana, wewe je?
Aaaah 😂😂😂mie ata kusogea sitaki kujua kinachoongelewa maana mda wowote lamghambo linaweza kulia Ebu ona kama hii ya magomeni mpk mtu anaepita na mmbo yake anaitwa mwandamanaji hii sio sawa lkn serikali hii
 
Mbowe na mwanawe wamesindikizwa kistaarabu bila makofi.
 
Leo ni siku iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania. Siku ya maandamano ya wananchi wakiongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Chama hiko; amefafanua kwamba lengo la maandamano hayo ni kupinga wimbi na matendo mabaya yanayoendelea nchini ya utekaji nyara, kupotea kwa watu na mauajo ya raia. Wananchi wamelinyooshea kidole jeshi la polisi kutokana na mazingira ya upoteaji wa watu. Watu wengi wameripotiwa kupotea baada ya kuitwa vituo vya polisi.

======

Siku ya waliyosema chadema kufanya maanadamano kwaajili ya kupinga utekaji na watu kuuliwa na watu wasiyojulikana imefika,

Tangazo hili lilitolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Septemba 11, 2024, ambapo alisema wataingia barabarani endapo wanachama wao waliopotea hawatarudisha na kama serikali haitawajibika ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa viongozi husika.

Ratiba ya maandamano ilitolewa Jumamosi tar 21 Septemba 2024 baada ya kuwa serikali haijatekeleza takwa lolote kati ya yale yaliyotolewa na CHADEMA kuhakikisha kuna uwajibikaji.

Fuatilia uzi huu kwa matukio ya moja kwa moja kwa siku ya leo na yatakayojiri kwenye maandamano hayo.


=======UPDATES======
View attachment 3103938
Magomeni muda huu. Naelekea katikati ya mji nifike Mnazi Mmoja

Asubuhi imeanza kwa taarifa ya Lissu kuzingirwa na polisi na kutakiwa kwenda kuripoti katika ofisi ya RCO Kinondoni, ambapo amekubali kwenda kuitikia wito.


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameeleza kupitia mitandao ya kijamii kuwa tangu jana usiku mpaka asubuhi ya leo Septemba 23, 2024 Jeshi la Polisi limefunga barabara zote zinazoelelea nyumbani kwa mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe.

Chama hicho kimeeleza kuwa watumiaji wote wa barabara hiyo wanasimamishwa na kukaguliwa, wakiulizwa kama wanaenda kwenye maandamano.

CHADEMA wameripoti kuwa mapema leo Jeshi la Polisi wameingia nyumbani kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara kisha kuondoka nae bila kusema wanampeleka wapi.

CHADEMA imeripoti kuwa Jeshi la Polisi limemzuia Dr. Lilian Mtei, Mke wa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe akiwa anatoka nyumbani kwake Mikocheni, Dar es salaam.


WAKILI WA CHADEMA: TUNDU LISSU AMEKAMATWA AKIWA NYUMBANI KWAKE TEGETA
Wakili wa Chadema, Hekima Mwasipu amesema Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu amekamatwa na polisi asubuhi ya leo Jumatatu, Septemba 23, 2024.

“Lissu amekamatwa nyumbani kwake Tegeta na amepelekwa Kituo cha Polisi Mbweni na mimi kama wakili niko njiani nakwenda huko kujua sababu za kukamatwa kwake

MAKONDA: KAKA YANGU MBOWE KUMBE UPO ARUSHA NA HAUSEMI
Wakati Chama Cha Demokrasia na Maendelei Chadema kikitangaza kufanya Maandamano ya amani leo Jijini Dar Es salaam chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amechapisha mtandaoni mwake akisema anazo taarifa kuwa Mwenyekiti Mbowe yupo Arusha na hivyo kumualika ofisini kwake Jijini Arusha. Makonda ameandika "Kaka yangu Mbowe kumbe umeingia Arusha na hausemi. Karibu Ofisini basi ukiamua Kutoka"

MBOWE AJITOKEZA MAGOMENI, AKAMATWA NA POLISI

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amekamatwa na Polisi eneo la Magomeni, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 23, 2024.

Kabla ya Mbowe kukamatwa, alifika eneo hilo akiwa na gari dogo, kisha kuanza kuzungumza na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Mbowe, wameamua kuwekea mkazo suala la maaandamano, baada ya maombi ya mahitaji, ikiwemo kutaka kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, viongozi waandamizi wa ulinzi na usalama kama sehemu ya uwajibikaji.


Baba mlezi wa Deusdedith Soka amejitokeza katika maandamano ya amani Ilala Sokoni. Azungumzia kupotea kwa Soka.


Jeshi la Polisi likiendelea kuwakamata waandamanaji maeneo ya Ilala Boma.

JESHI LA POLISI LATHIBITISHA KUWAKAMATA WAANDAMANAJI 14 IKIWEMO VIONGOZI WA CHADEMA
Jeshi la Polisi limetoa taarifa rasimi ya kuwakamata watu 14 ikiwemo baadhi ya Viongozi wa Chadema, Mwenyekiti Freeman Mbowe, Lissu na Lema, ambapo wamedai kuwa viongozi hao wamekamatwa kufuatia mpango wa maandamano.

Wanawashikiria kwa sasa wanahojiwa kwa ajili ya hatua za kisheria.

Kamanda Muliro ametangaza kuwakamata viongozi mbalimbali wa CHADEMA ikiwemo Freeman Mbowe, Tundu Lissu pamoja na Godbless Lema.

Duniani kote kuna lugha maalumu ambayo huwa inatumika katika kuzungumza Kati ya Wananchi na Watawala wao ambao ni Madikteta. Wananchi wakati wanapozungumza kwa kutumia lugha hiyo maalumu, watawala wao huwa wanaelewa haraka Sana na mara moja huwa wanafikia muafaka mzuri Sana kati yao.
 
Kwenye suala la kutafuta haki kuna njia nyingine nyingi tu mana kuna majukwaa mengi ya UN yanayosikiliza na kusimamia haki za binadamu wote kwa kwa ujumla.

Kwanini watu wasitumie njia ya kuandaa midahalo ya kujadili changamoto za nchi zao na kuzifikisha katika manukwaa ya kimataifa pale inapobidi?

Bora kutumia njia ya migomo katika utendaji ili kupata suluhu ya matatizo katika nchi kuliko kuandamana kitu ambacho mwisho wake tunajiandalia njia za machafuko wenyewe.
Kwanini kama ni kupata haki ya kubadili katiba wananchi wenyewe wasiwe katika mstari wa mbele kwenye kuidai na isipopatikana basi ifuatiwe na migomo katika utendaji wa shughuli za uzalishaji kitu ambacho ni lazma Serikali iguswe moja kwa moja mana haiwezi kujiendesha bila ya fedha zinazotokana na uzalishaji?

Kama ni suala la kupanda kwa gharama za maisha kutokana na kodi na ushuru kwanini wafanyabiashara wasifanye migomo mana kwenye democracy kuna haki ya kugoma ikiwa kuna ukandamizaji unaendelea.

Suala la maandamano si swala la kulisifia na kulipokea kwa sherehe hivyo tizameni outcomes zake kuna Vifo vya raia wasio na hatia, wamama wazee na watoto wanaweza kuwa waathirika wakubwa.

Be rational, tumia njia yenye maumivu kwa pande zote ikiwa ni lazima Serikali itaumia na wananchi wataumia kwa muda mfupi ila haki lazma ipatikane mana ndiyo inaweza kuwa suluhisho la pekee kwa migomo hiyo hapa suala usalama ni muhimu.
"Njia pekee ambayo Wananchi wataitumia katika kuzungumza au kujadiliana na Watawala wao ambao ni madikteta ili kufikia muafaka wenye maslahi kwa pande zote mbili ni kwa kupitia mtutu wa bunduki."

Jeff's O'Brien.
 
kulinda serikali kuhofia kupinduliwa na wanajeshi maana mapinduzi ya kijeshi ndiyo yanayomtoa Rais madarakani lakini maandamano ya wananchi yanampa nafasi Rais ama kujiuzulu au kukubaliana na matakwa yao na sio matakwa ya Majeshi.
Juzi juzi tu hapo Bangladesh juhudi za wananchi zilimwondoa waziri mkuu madarakani bila ya ushiriki wa jeshi (nadhani); ingawaje huenda waliamua tu kukaa pembeni.
 
Back
Top Bottom