Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Mbowe na Wenzake: Shahidi Afred Kapala wa tiGO atoa Ushahidi, Kesi kuendelea, Nov 03, 2021

Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Mbowe na Wenzake: Shahidi Afred Kapala wa tiGO atoa Ushahidi, Kesi kuendelea, Nov 03, 2021

Hata hiyo ya Platinum Member unaona wivu[emoji3][emoji3].Waulize Wakongwe JF watakuelewesha vizuri na kama unaona nafaidika mno basi chukua wewe kiroho safi[emoji3][emoji3]
Nimefarijika ujumbe umefika. Maana nikikulinganisha na akina Pascal Mayalla, Mshana Jr, na wengineo wengi! Naona tofauti kubwa sana kati yenu.

Anyway, this is JF! So i understand.
 
😂😂😂 Kama wakili wao hamjui mbowe sisi tutamjuaje nandi? Alafu wanatulashimishia, shenz kabisa!

Alafu utakuta hata huyo nandi mwenyewe hajui kama tigo wanalazimishia nyimbo zake kwa watu, si ajabu hapokei mirahaba stahiki. Mwana FA na AY waliwahi kuwashtaki tigo kwa mchezo kama huu wakalipwa shilingi bilioni 2.1 kesi ilisimamiwa na Alberto msando enzi zile akiwa na akili timamu.

Tigo inanuka! Ndio maana baada ya mwendazake kutupwa shimoni, mwenyekezaji wa ndani ya nchi wa MIC Tanzania Ltd Yusuph Manji alikuja chap akauzilia mbali hisa zake. Nadhani alishajua kuna bomu litalipuka soon, sasa hawa wamadagaska wameuziwa mbuzi kwenye gunia maskini ya mungu, labda rostam atumie mbinu za ziada.
Mkuu afu hizi system za mitandao zina weakness sana, wao wanajiona wapo salama kwasababu wana oparate shuguli zao kwenye nchi ambayo haina technology ya kutosha

Jana hapo kwenye laini yangu ya halotel nimepokea ujumbe kutoka NMB ambao unaonesha nimefanya malipo ya 349,500 na wakati huo simu yangu nimeiweka chaji.
Screenshot_20211102-170737.png

Hivi muda huu navyo jadiliana na wadau kwenye huu mjadala, nimepokea meseji nyingine yenye jina la NHIF ikionesha muamala wa malipo ya shilingi 50,400
Screenshot_20211102-170554.png

Sasa najiuliza, kama hii inewezekana kwangu mimi ambaye sina mgogoro wowote na mamlaka kubwa, inashindikana vipi kwa serikali?

Mtu anaweza kuja na madai kua nimefanya miamala hiyo na taarifa zangu zipo kwenye server kutumika kama ushahidi mahakamani na wakati hata mimi sijui kilichofanyika
 
Ndiyo maana nikamshangaa anaetaka kumtupia lawama huyu shahidi mfanyakazi wa Tigo,yeye kaitwa hapo kwa nafasi yake na kwa mujibu wa sheria za Nchi hii, kumtupia lawama ni kumwonea,hata angekuwa yeye anaemlaumu angetakiwa kufanya hivyo angetii pia.Si sawa kutupia lawama kila mtu kisa tu anatoa ushahidi kwa upande wa Jamuhuri,wengine wanalazimika kutoka na nafasi zao kama huyo mtafanyakazi wa Tigo.
Nyamizi tatizo siyo shahidi kutoa ushahidi wake kwa mujibu wa sheria...

Tatizo liko kwenye utaratibu uliotumika kupatikana kwa ushahidi ukimhusisha shahidi huyo na kampuni anayofanyia kazi. Hiki ndicho kinachohojiwa na upande wa utetezi dhidi ya shahidi huyu...

Mashaka ya upande wa utetezi yanakuwa makubwa zaidi pale ambapo mchakato wa polisi kutaka taarifa za mteja wa TIGO TZ ndg Freeman Mbowe una lineup kati ya polisi na Freddy Kapala pekee...!!

Yaani anaandikiwa barua yeye Freddy, anaipokea yeye Freddy, anaifanyia kazi yeye Freddy na mwisho kuijibu yeye moja kwa moja....

Kwa lugha rahisi ni kuwa, upande wa utetezi wanamuonesha shahidi huyu kuwa, hizo taarifa za mteja wenu huyu alizi - generate na kuwapa polisi kinyume cha Sera na utaratibu wa kisheria wa kampuni na nchi kwa ujumla...

Upande wa utetezi wanajaribu kumuonesha Freddy Kapala nia/kusudi la kutofuata utaratibu ilikuwa ni nini hataka kama kweli taarifa hizo ni za kweli. Je, hivi huyu siyo mhalifu [hacker] kweli kama wahalifu wengine..?

Katika maelezo yake hakuna mahali inaonesha CEO wake au Legal HOD wake au wenzake ndani ya idara walihusika moja kwa moja au kusaidiana naye...

Hii ni achilia mbali yeye Freddy kuhoji uhalali wa kisheria wa barua hiyo kutoka polisi, kwamba, imekidhi vigezo vya kisheria kuruhusu taarifa za mteja kupewa polisi....

Freddy hakujisumbua kabisa kutaka kujiridhisha hill. Yeye kafanya tu kwa sababu aliyetaka hizo taarifa ni polisi...!!

Kwa hiyo, huu ndiyo msingi wa mashambulizi dhidi ya mashahidi kama Freddy kwenye kesi hii...

Kwa lugha rahisi tunaweza kusema kuwa, hawa ni mashahidi wa kutengenezwa/kubumba, kwamba...

Kwamba, kwa kuwa polisi kwa kutumika kisiasa wanataka kum - incriminate Freeman Mbowe, wanaamua kutumia baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu wa kampuni za simu kuwapatia taaifa za mteja huyu kinyume cha utaratibu. Freddy anashambuliwa kwa sababu hii, si kwa sbb ni shahidi tu...

Kwa mantiki hata ushahidi unaopatikana kinyume cha sheria, hukosa nguvu kwenye mashitaka..

Na kwa vyovyote vile, upande wa utetezi hawawezi kumtumia shahidi kama huyu kama unavyodai wewe...!!
 
😂😂😂😂😂😂 Mkuu nikifunguka hapa naweza kula BAN ndefuuuu. Kwani hilo swali hata mimi nimewahi pia kujiuliza. Ni bora tu nipige kimya Mkuu.
Kuwa Platinum member unalipia kiasi fulani cha pesa.

Upo hapa siku nyingi, hapo nyuma JF ilikuwa inahitaji boost ya members kujiendesha, ndio zikaletwa hizi rank za Blonze, Silver, Gold na Platinum, kila moja unachangia kwa kiasi chake, nakumbuka mimi nilikuwa Gold member, sijui nini kilitokea wakazifuta hizo nyingine wakaacha hiyo Platinum.

Kwahiyo ukitaka hiyo tittle ya Platinum member wasiliana nao watakupa utaratibu kwa sasa ukoje? Ila mpunga unahusika.
 
Kibatala ndo ana maswali ya kijinga tu, kuna muda ukimfatilia unaona kabisa anaenda pale kuprolong muda tu.

Wakili:Huwa unavaa miwani?
Shahidi: Ndio huwa ninavaa.
Wakili;Lakini hapa haujavaa.
Shahidi:Niulize maswali ya maana bwana[emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23] mahakamani Kuna mambo Hadi maswali unnessary hivo ya nini?
 
mwanasheria anatia huruma, Tigo wameumbuka kutofuata sheria ya privacy ya info za mteja. Yaani police akienda kutaka data zozote, za mtanzania yoyote wanampatia.... Tigo nyie hapa mnalo.
wamejishusha na watashuka sana kimapato,kwa mtu anayejielewa lazima avunje line yao leo
 
Nimefarijika ujumbe umefika. Maana nikikulinganisha na akina Pascal Mayalla, Mshana Jr, na wengineo wengi! Naona tofauti kubwa sana kati yeni.

Anyway, this is JF! So i understand.

Haya kunywa maji ya baridi upunguze hasira Mkuu,hapa JF ni sehemu ndogo sana ya maisha yangu,So I don’t care about Status,ukiona hii inaweza kukuongezea mkate wako wa kila siku wewe chukua hata sasa hivi.Sihitaji kulinganishwa na mtu wala kuoata approval ya mtu yoyote.
 
Na ameapa ndani ya mahakama kwamba atasema "kweli, tena kweli tupu" Sasa kusema hamjui Freeman Mbowe ni uongo wa wazi kabisa na unamshushia hadhi ndani ya mahakama na katika ushahidi wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mahakama imsamehe tu huyo mwanasheria, lakini Tigo! Najipongeza sana kuvunja vunja laini yangu ya Tigo last Month!
 
Huyo shahidi ameanza kujitambulisha kwa mbwembwe hadi nikaogopa. Lakini maswali aliyoshushiwa sio mchezo ni haki hao jamaa wajiite wasomi
 
Lazima wateja walindiwe faragha zao kwa sheria madhubuti kama tunataka kuonekana watu wanaojiwelewa huko duniani.
mbona JamiiForum walikataa kutoa taarifa za wateja bila kufuata sheria?
 
Hii ilianzia kwenye kesi ndogo ya nyuma. Wao wanajikita kwenye maswali mepesi mambo makubwa yanawapita. Jaji aliwashangaa kwa jinsi walivyo ruhusu ushahidi kupokelewa wakati walikuwa na nafasi ya kuupinga na hii ilikuwa obvious hata kwa asiye mwanasheria. Sina uhakika wa maswali ya kunywa mo energy nk yalikuwa na tija kama ambavyo maswali yao hanaelea kwenye vitu vidogo na kuacha kuonyesha mapungufu ya mashataka. Kwa mfano wameng`ang`ania usiri wa taarifa za mteja wa TIGO ambao sidhani kama unaathari iwapo taarifa zilizotolewa zina ukweli. Suala la Usiri wa wateja na TIGO wangewaachia wateja huko nje ya kesi. Hapa issue taarifa ni ya ukweli au siyo na waprove hivo mahamakamani . Hii si kesi ya ushabiki kwani kosa moja mtu anafungwa hivyo umakini unatakiwa uonekane na sisi wafuatiliaji tuchambue kwa umakini badala ya ushabiki kutawala
Ume observe ka Mimi tangu Ile kesi ya mwanzo vi maswali vilikuwa minor na havikutokea hata msaada kwa washtakiwa kujinasua na jinsi case inavoenda mbona ni hatari hawaulizi ukweli wa kilichoulizwa na ku link na huo ugaidi maana kutuma tu laki tano vina relate vipi na ugaidi jamani.
 
Nyamizi tatizo siyo shahidi kutoa ushahidi wake kwa mujibu wa sheria...

Tatizo liko kwenye utaratibu uliotumika kupatikana kwa ushahidi ukimhusisha shahidi huyo na kampuni anayofanyia kazi. Hiki ndicho kinachohojiwa na upande wa utetezi dhidi ya shahidi huyu...

Mashaka ya upande wa utetezi yanakuwa makubwa zaidi pale ambapo mchakato wa polisi kutaka taarifa za mteja wa TIGO TZ ndg Freeman Mbowe una lineup kati ya polisi na Freddy Kapala pekee...!!

Yaani anaandikiwa barua yeye Freddy, anaipokea yeye Freddy, anaifanyia kazi yeye Freddy na mwisho kuijibu yeye moja kwa moja....

Kwa lugha rahisi ni kuwa, upande wa utetezi wanamuonesha shahidi huyu kuwa, hizo taarifa za mteja wenu huyu alizi - generate na kuwapa polisi kinyume cha Sera na utaratibu wa kisheria wa kampuni na nchi kwa ujumla...

Upande wa utetezi wanajaribu kumuonesha Freddy Kapala nia/kusudi la kutofuata utaratibu ilikuwa ni nini hataka kama kweli taarifa hizo ni za kweli. Je, hivi huyu siyo mhalifu [hacker] kweli kama wahalifu wengine..?

Katika maelezo yake hakuna mahali inaonesha CEO wake au Legal HOD wake au wenzake ndani ya idara walihusika moja kwa moja au kusaidiana naye...

Hii ni achilia mbali yeye Freddy kuhoji uhalali wa kisheria wa barua hiyo kutoka polisi, kwamba, imekidhi vigezo vya kisheria kuruhusu taarifa za mteja kupewa polisi....

Freddy hakujisumbua kabisa kutaka kujiridhisha hill. Yeye kafanya tu kwa sababu aliyetaka hizo taarifa ni polisi...!!

Kwa hiyo, huu ndiyo msingi wa mashambulizi dhidi ya mashahidi kama Freddy kwenye kesi hii...

Kwa lugha rahisi tunaweza kusema kuwa, hawa ni mashahidi wa kutengenezwa/kubumba na kwa vyovyote, upande wa utetezi hawawezi kumtumia shahidi kama huyu...!!

Asante sana kwa maelezo ya kina,walau wewe umejikita kwenye kujibu hoja yangu.Sasa ningependa kujua hapo unaposema aliandikiwa yeye kama yeye.Hivi kweli unaamini Police walimwandikia Freddy au waliiandikia Kampuni ya MIC (Tigo)? Na Je kama haya masuala yenyewe ndiyo huwa anayashughulikia moja kwa moja,kama yeye ndiyo HOD je?

Kuna sehemu nilikuwa nafanya kazi,taarifa za Wateja zilikuwa zinaombwa na TRA wanapokuwa wanawafanyia Auditing,walikuwa wana adress kwa MD lkn zile barua zilikuwa zinaletwa moja kwa moja na Secretary kwangu na nazishughulikia bila kupitia kwa MD,maana tayari MD alishatoa Order barua zote za nature ya kuomba taarifa za Wateja ziletwe moja kwa moja kwangu.Sasa ukipeleka hiyo taarifa,kama ilivyo utanishutumu mimi kuwa TRA waliniandikia mimi na nikashughulikia mimi moja kwa moja?
 
Kuwa Platinum member unalipia kiasi fulani cha pesa.

Upo hapa siku nyingi, hapo nyuma JF ilikuwa inahitaji boost ya members kujiendesha, ndio zikaletwa hizi rank za Blonze, Silver, Gold na Platinum, kila moja unachangia kwa kiasi chake, nakumbuka mimi nilikuwa Gold member, sijui nini kilitokea wakazifuta hizo nyingine wakaacha hiyo Platinum.

Kwahiyo ukitaka hiyo tittle ya Platinum member wasiliana nao watakupa utaratibu kwa sasa ukoje? Ila mpunga unahusika.

Asante sana kwa ufafanuzi wako Mkuu,haya uliyekuwa unataka kujua,Jibu hili hapa umepewa.
 
Kuwa Platinum member unalipia kiasi fulani cha pesa.

Upo hapa siku nyingi, hapo nyuma JF ilikuwa inahitaji boost ya members kujiendesha, ndio zikaletwa hizi rank za Blonze, Silver, Gold na Platinum, kila moja unachangia kwa kiasi chake, nakumbuka mimi nilikuwa Gold member, sijui nini kilitokea wakazifuta hizo nyingine wakaacha hiyo Platinum.

Kwahiyo ukitaka hiyo tittle ya Platinum member wasiliana nao watakupa utaratibu kwa sasa ukoje? Ila mpunga unahusika.
Nilikuwa najiuliza sana, unakuta platinum member lakini kichwa maji kabisa
 
Na ameapa ndani ya mahakama kwamba atasema "kweli, tena kweli tupu" Sasa kusema hamjui Freeman Mbowe ni uongo wa wazi kabisa na unamshushia hadhi ndani ya mahakama na katika ushahidi wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiapo alichoapa,mwisho anaposema Mungu nisaidie........ivi viapo vya kuapa kwa majina ya Mungu tuviheshimu sana
 
Hii ilianzia kwenye kesi ndogo ya nyuma. Wao wanajikita kwenye maswali mepesi mambo makubwa yanawapita. Jaji aliwashangaa kwa jinsi walivyo ruhusu ushahidi kupokelewa wakati walikuwa na nafasi ya kuupinga na hii ilikuwa obvious hata kwa asiye mwanasheria. Sina uhakika wa maswali ya kunywa mo energy nk yalikuwa na tija kama ambavyo maswali yao hanaelea kwenye vitu vidogo na kuacha kuonyesha mapungufu ya mashataka. Kwa mfano wameng`ang`ania usiri wa taarifa za mteja wa TIGO ambao sidhani kama unaathari iwapo taarifa zilizotolewa zina ukweli. Suala la Usiri wa wateja na TIGO wangewaachia wateja huko nje ya kesi. Hapa issue taarifa ni ya ukweli au siyo na waprove hivo mahamakamani . Hii si kesi ya ushabiki kwani kosa moja mtu anafungwa hivyo umakini unatakiwa uonekane na sisi wafuatiliaji tuchambue kwa umakini badala ya ushabiki kutawala

Mkuu umemaliza kila kitu.
 
Back
Top Bottom