Nyamizi tatizo siyo shahidi kutoa ushahidi wake kwa mujibu wa sheria...
Tatizo liko kwenye utaratibu uliotumika kupatikana kwa ushahidi ukimhusisha shahidi huyo na kampuni anayofanyia kazi. Hiki ndicho kinachohojiwa na upande wa utetezi dhidi ya shahidi huyu...
Mashaka ya upande wa utetezi yanakuwa makubwa zaidi pale ambapo mchakato wa polisi kutaka taarifa za mteja wa TIGO TZ ndg Freeman Mbowe una lineup kati ya polisi na Freddy Kapala pekee...!!
Yaani anaandikiwa barua yeye Freddy, anaipokea yeye Freddy, anaifanyia kazi yeye Freddy na mwisho kuijibu yeye moja kwa moja....
Kwa lugha rahisi ni kuwa, upande wa utetezi wanamuonesha shahidi huyu kuwa, hizo taarifa za mteja wenu huyu alizi - generate na kuwapa polisi kinyume cha Sera na utaratibu wa kisheria wa kampuni na nchi kwa ujumla...
Upande wa utetezi wanajaribu kumuonesha Freddy Kapala nia/kusudi la kutofuata utaratibu ilikuwa ni nini hataka kama kweli taarifa hizo ni za kweli. Je, hivi huyu siyo mhalifu [hacker] kweli kama wahalifu wengine..?
Katika maelezo yake hakuna mahali inaonesha CEO wake au Legal HOD wake au wenzake ndani ya idara walihusika moja kwa moja au kusaidiana naye...
Hii ni achilia mbali yeye Freddy kuhoji uhalali wa kisheria wa barua hiyo kutoka polisi, kwamba, imekidhi vigezo vya kisheria kuruhusu taarifa za mteja kupewa polisi....
Freddy hakujisumbua kabisa kutaka kujiridhisha hill. Yeye kafanya tu kwa sababu aliyetaka hizo taarifa ni polisi...!!
Kwa hiyo, huu ndiyo msingi wa mashambulizi dhidi ya mashahidi kama Freddy kwenye kesi hii...
Kwa lugha rahisi tunaweza kusema kuwa, hawa ni mashahidi wa kutengenezwa/kubumba na kwa vyovyote, upande wa utetezi hawawezi kumtumia shahidi kama huyu...!!