Nyamizi, tazama "NIA" ya polisi kwa Freeman Mbowe ni nini. Mpaka hapa, mtu yeyote anajua kuwa, nia ya polisi by either HOOKS or by CROOKS ni kum - incriminate Mbowe na kisha ahukumiwe kifuñgo jela. Vita ya kisiasa hii....
Rudi tena kwenye "DHAMIRA/NIA" ya polisi...
Na kujibu hoja yako hii, YES, likely waliandikiwa Tigo. Hii haizuii barua kupokelewa na mtu wao anaowafanyia kazi yao haramu bila hata entire Tigo management kujua. Ni likely kuwa wamejua sasa na uharibifu kwa kampuni tayari umefanyika.!!
Kwenye hili haiwezekani ashughulikie peke yake. Kumbuka hili ni jambo la kisheria. Hawezi kuamua mtu mmoja. Lakini ktk scenario hii, hili liliwezekana. Wenzake wote katika idara hata HOD wake hajui..!
Ndiyo maana mawakili wa utetezi wanambana kwenye eneo hili ili kumwezesha Jaji aone tatizo la ushahidi huo, kuwa haujakidhi sheria, umepatikana kwa njia haramu ili kukidhi NIA OVU...!
Kama ilikuwa addressed kwa MD na kisha kukupa "Go ahead", hapo hakuna tatizo. Lakini kumbuka, always inategemea na ishu hiyo inahusu nini...
Kuna ishu zingine huwezi kuzishughulikia wewe moja kwa moja bali baada ya kufanya part yako, ni lazima tena urudi kwa MD wako ili kufanya assessment ya aidha mteja apewe au asipewe kwa kuzungatia impact ya kisheria ...
Huyu Freddy ni tofauti na wewe. Kwanza ishu yenyewe aliyokuwa anaishughulikia ni very sensitive, ishu ya UGAIDI lakini imefanywa kihunihuni kwa mlango wa nyuma. Huyu haraka haraka mtu yeyote anaweza kuelewa kuwa huyu ni part & parcel ya syndicate hii ya kutengeneza/kubumba kesi. Hata huko Vodavom, Airtel, Halotel, Zantel, kwenye mabenki na taasisi zingine wapo wamepandwa huko...!
Tukubali kuwa, polisi walikuwa wanamtumia Freddy Kapala kwa nia ovu kwa mlango wa nyuma bila kufuata sheria. Huu hauwezi kuwa ushahidi genuine...!!