Umeona holes nyingi sana! Kibaya zaidi ni kuhusu hao washukiww kuwa watatu mpaka hatua za mwisho. Huku timu za wakamataji zikiwa mbili na zote hazielezi mtu wa tatu alikuwa nani!! Binafsi nadhani huyu wa tatu alikuwa Urio na ndio informer so wasingeweza kumkamata!! Sasa ninadhani hata jaji hawezi kuwa na picha ya sehemu ya tukio. Mara grocery, kibanda umiza, mara wamekaa tu, mara walikuwa wakisajiri laini za simu! Mara watatu wamekaa na kutambulika, lakini kuanzia hapo ghafla ni watu wawili. Mara wameenda Arusha kumtafuta Lijenje lakini wakiwa hawajui jina la dadake wala anaishi wapi lakini walienda anyways!!
Mashahidi wengine wanasema ilikuwa ni madawa ya kulevya, namba 08 kawa smart - kasema inafikiriwa ni madawa ya kulevya. Na bado hizo kete haziko mahakamani kama madawa au si madawa. Risasi tatu dhidi ya moja iliyoletwa mahakamani.
Sitashangaa nikisikia jamaa walikuwa na silaha wanayoimiliki isiyo halali lakini hawakuwa wahalifu. Ikimbukwe walikuwa sio hata waajiriwa wa Mbowe bado so sijui silaha hiyo ingehusika vipi na magogo ya barabarani, maandamano yasiyo na kikomo. Jamhuri itashindwa kuunganisha silaha hii na ugaidi!! Ni
kwa sababu kumiliki silaha hakumfanyi aliyenayo kuwa mhalifu kimatendo. Kumiliki kihalali hakumfanyi mtu kudhaniwa hataitumia kuua mtu mwingine - actually wanapewa ili wauwe. Je bastola hii ilikusudiwa kumuua mtu specific, that is hard to prove mpk sasa.