Wakuu,Sasa mbona Urio ndio Gaidi mwenyewe maana meseji zote za Kigaidi anatuma yeye na Upande wa Mbowe hakuna meseji yoyote ya Ugaidi na hela zenyewe akitumiwa zingine anakula yeye.[emoji28][emoji28][emoji28]
Shahidi: "Naomba nitumie nauli ya Ku' mobilise nikutane nao Moro"
Kibatala: Nani alikuwa anaomba nauli
Shahidi: Mimi ndiye niliye kuwa naomba
Kibatala: Baada ya wewe kuomba nauli ndiyo Mbowe sasa akatuma TSh 500,000
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Nitafutie Meseji yoyote ambayo Mbowe anatoa wazo yeye la kutuma yeye TSh 500,000
Shahidi ametumia dakika 1 kutafuta hapa..
Shahidi: HAKUNA
Kibatala: Tafuta Meseji ya Tarehe 20 July 2020 Saa 2 na Dakika 24 na Sekunde 02
Shahidi: "Usiwe unatumia namba yako Kutuma Pesa, Tumia Wasaidizi Wako au Wakala Kutuma"
Kibatala: Ni nani aliyetuma Meseji hii
Shahidi: Mimi Denis Urio
Kibatala: Kuna Sehemu Yoyote Katika Kielelezo namba P 34 ambayo Freeman Mbowe amekueleza wewe Kwamba Mtumie Njia ya Mawasiliano Mbadala Kwa Sababu Simu Siyo Salama
Shahidi: Meseji ya Mwisho
Kibatala: haya tusomee
Shahidi: "Hellow Bro Nilishindwa Kupokea Simu yako Sababu Deshi Deshi"
Kibatala: kwa hiyo kwa Tafsiri yako Ndiyo Kasema kuwa Simu Siyo Salama
Shahidi: Ndiyo Nilivyo Tafsiri
Kibatala: Katika hiyo Meseji ya Mwisho Kuna Neno simu siyo Salama
Shahidi: Hakuna
Aisee,Mungu wa ajabu sana,Acha ikae hivyo.[emoji419]