Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

Habari Wakuu,

Leo tena shahidi wa 12 Denis Urio anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Fuatana nami kupata yatakayojiri

UPDATES:

Jaji ameingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Mawakili wa Serikali Waandamizi na Tulimanywa Majige, Wakili wa Serikali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ikikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili

Seleman Matauka
Alex Massaba
Paul Kisabo
Sisty Aloyce
Maria Mushi
Khadija Aron
Michael Lugina
Evaresta Kisanga
John Mallya
Nashon Nkungu
Dickson Matata

Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo Tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea

Shahidi anapanda Kizimbani

Jaji: Shahidi Jana Ulikuwa Unatoa Ushahidi Wako, Unaulizwa Maswali Chini ya Kiapo na Leo Utaendelea Kuulizwa Maswali Chini ya Kiapo

Wakili John Mallya: Shahidi tunaendelea tulipo Ishia Jana, Mheshimiwa Jaji Naomba Jibu lake la Mwisho

Jaji: ni Kwamba Asipotumia Jina Namba zake Jina lake halitoonekana...

Malya: hivi kazi ya VIP PROTECTION Inafanyikaje

Shahidi: Mheshimiwa Jaji kazi ya VIP PROTECTION Inafanyika kwa mtu yoyote, Kwa Kufuata Sheria na Kanuni za Nchi

Malya: Ni sahihi Kwamba kazi Wanazofanya VIP protection Ni lazima wawe naye Kwa Wajibu wa Kum' protect

Shahidi: Ni sahihi Malya: hawa VIP protection Ni sawa na Body guard?

Shahidi: Sijawahi Kusikia Body Guard mimi

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba 26

Malya: Umesema kuwa hawa VIP protection Wanakuwa pamoja na Wanayem' protect, sasa ni somee Meseji ya Tarehe 20 July 2020, Ya Saa Mbili Asubuhi

Shahidi: Hawa wawili Kuanzia Siyo Mbaya Hawawezi Kutelekezwa, Nitakuwa nao Full time

Malya: Kwa Kazi gani

Shahidi: Ulinzi Ndiyo

Malya: Je, kuna meseji nyingine yoyote kwamba kuna mahali Mbowe anasema nitawatuma Kufanya kazi nyingine au uhalifu?

Shahidi: kwenye meseji hazipo

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo Namba 35

Malya: Tumeletewa report kule ulikopeleka simu , Je hii namba ina Jina gani?

Shahidi: Imeandikwa FREE... Ambayo ni namba ya Freeman Aikael Mbowe

Malya: Very Good shahidi umeniongezea information nilikuwa sijui, sasa washa simu yako

Shahidi anabonyeza simu, anasema tayari

Malya: Unasema Ulikuwa Unawasiliana na Mbowe Kupitia Mtandao Wa Telegram

Shahidi: Ndiyo Mtandao Wa Telegram

Malya: Naomba usogee kwa Mheshimiwa Jaji pale kamuonyeshe namba unayosema ume-chat na Mbowe. Je, hapa kuna Jina FREE linaonekana, ukiwa umefungua meseji?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji HAKI YA MUNGU hii ni akaunti ya Mbowe siyo Group, nafungua

Malya: Jina Free Ukifungua Meseji linaonekana au halionekani?

Shahidi: Halionekani lakini ni Akaunti ya Mbowe

Malya: Je, ulitoa Ufafanuzi/Maelezo kuwa Jina FREE halionekani?

Shahidi: Si nilimjibu mimi Bwana, Mimi siyo Mtaalamu Wa IT, Sasa nitoe Maelezo Ya nini

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba atoe jibu

Jaji: Umeelewa Swali? Kwamba Wakati Unasoma Ulitoa Ufafanuzi? Kuwa jina halionekani

Shahidi: Ufafanuzi huo sikutoa

Mahakama: (Kicheko)

Malya: Haya Ulisema Kwamba Mbowe alikuwa nakupa Wishes za Christmas na Mwaka Mpya, je Meseji zimeanza lini

Shahidi: Tarehe 20 July 2020

Malya: Alikuwa anakutakia Heri ya Mwaka Mpya Kupitia nini

Shahidi: alikuwa ananipigia Simu

Malya: Alikuwa anakupigia simu kwa njia ipi

Shahidi: Kwa Telegram

Malya: Je, unafahamu kwamba ukipiga Simu Telegram unabakia na Calls Record

Shahidi: Sina Utaalamu huo

Malya: Je Jana Wakati wa Ushahidi Wako Kama Ulituonyesha WhatsApp Calls na Meseji za Mbowe

Shahidi: aliyechunguza ndiye anafahamu

Malya: Kwa hiyo Mtaalamu anaweza Kuwa amepunguza au ameongeza?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi hajasema hivyo

Malya: Nitauliza Upya Kuokoa muda, Kilichokufanya Jana usitoe Calls za WhatsApp

Shahidi: nilisema kwamba Mimi Nilikuwa na wasiliana na Mbowe Kwa WhatsApp, Meseji na Telegram

Malya: Sawa Jana Ulionyesha WhatsApp Call wakati wa Ushahidi Wako?

Shahidi: Sikuonyesha

Malya: Ulionyesha namba zingine ambazo Ulikuwa Mbowe alikuwa anakupigia Simu

Shahidi: Sikuonyesha

Shahidi: (Ghafla) Sikuonyesha Kwa sababu..

Malya: sitaki sababu hapa

Shahidi: Sikuonyesha Kwa sababu

Malya: Sijakuuliza kuhusu sababu

Jaji: Shahidi sikiliza swali ndiyo ujibu

Malya: Naomba Kielelezo Namba 28

Malya anamkabidhi shahidi

Malya: Jana ulishindwa Kuiwasha hii simu

Shahidi: Sikushindwa, haikuwaka

Malya: Ulitoa Explanation Kwanini ilishindwa Kuwaka

Shahidi: Nilieza Kwamba simu ina ibovu wa Display, Ukiwasha Hai Display Kitu chochote

Malya: Kama kuna Taarifa ya Muhimu ambayo Mbowe anataka Kujitetea Kutumia hiyo Simu atafanyeje, Utampa akatengeneze

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakati natoa Ushahidi Wangu Kuhusu Kukabidhi Simu, Nilisema, Nilienda na Simu moja, Sikujua Kama Nilitakiwa Kukabidhi Simu, Nikauliza kwa sababu gani wakasema sababu ya Uchunguzi, Tarehe 10 nilipeleka simu zingine, na Mimi nilipeleka Simu Ikiwa imedondoka haifanyi kazi

Malya: Aliyechunguza hajasema Kwamba Simu Mbovu, Isipokuwa wewe unaogopa kwa sababu unajua Kilichopo humo hutaki kionekane

Shahidi: Washa wewe

Malya: Mimi siwezi Kuwasha Simu yako

Shahidi: basi awashe hata Mheshimiwa Jaji

Malya: wewe Ndiyo Mwenye Simu Shahidi: basi hayo Mengine ni Maoni

Malya: Kuna report ya hii Simu, Je Jana Ulionyesha Call Logs za mbowe

Shahidi: Sikuonyesha

Malya: Calls za Khalfani Bwire Jana Ulionyesha

Shahidi: Sikuonyesha, Sababu sikuulizwa

Malya: Je, jana Ulionyesha Meseji za Ling'wenya Kuhusu Kuwasiliana nao wasikengeuke

Shahidi: Sikuonyesha sababu sikuziona

Malya: Ni sahihi unasema Kwamba a baada ya kuwapeleka Vijana Wanne Kwa Mbowe Mwisho wa Kuwasiliana naye ilikuwa Tarehe 24

Shahidi: Ndiyo

Malya: Wakati Mbowe anaacha Kupokea Simu yako alikuwa tayari na Vijana Wanne

Shahidi: Ndiyo

Malya: Soma hapa

Shahidi: Kaka Wale Mtu 3 au 4 Ni Muhimu

Malya: Sasa kama Umeshampa Mtu Nne ukitaka uwasiliane naye nini

Shahidi: Nilichokitaka Kwake baada ya kukikosa nikakipata kwa Bwire

Malya: Kwa hiyo Wakati anaacha Kuwasiliana na wewe Hitaji lake alikuwa ameshalimaliza

Shahidi: Ndiyo

Malya: Miji ya Arusha, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza ina masoko mangapi?

Shahidi: Mimi sifahamu anafahamu Mbowe

Malya: Miji niliyotaja ina vituo vya mafuta vingapi?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji najibu swali kama Ifuatavyo anayejua idadi ya vituo vya mafuta ambavyo alipanga kulipua ni Freeman Mbowe

Malya: Shahidi Miji hiyo ina Mikusanyiko Mingapi

Shahidi: Mheshimiwa Jaji mimi sijui ina mikusanyiko mingapi, Ila Mheshimiwa Mbowe ndiye anajua kwa sababu alipanga kulipua

Malya: Ulifika Ofisi za DCI Je Ulifika ukiwa na Simu zako

Shahidi: Ndiyo

Malya: Je, ulieleza Jana Kama Ulikuwa na Simu zako

Shahidi: Mheshimiwa Jaji nilifika kwa DCI nikampa Taarifa, akasema endelea nao

Malya: Maelezo Yako Mazuri ila siyahitaji, Swali langu Ulieleza Kama Ulimuonyesha DCI Simu zako na Mawasiliano ya Mbowe?

Shahidi: Sikueleza

Malya: Unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Kurekodi?

Shahidi: Mimi sifahamu

Malya: Je, unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Upelelezi

Shahidi: Mimi sifahamu Kwa sababu, Kazi yangu haikuwa Kufanya Upelelezi Bali Kutafuta Watu wa Kufanya Kazi

Malya: Wakati Khalfani Bwire, Je alikwambia Vifaa wanavyokwenda Kuvitumia

Shahidi: Hakuniambia

Malya: Wakati Unaingia Jeshini ulikuwa na Certificate ya Form Four na Certificate Ya Ufundi

Shahidi: Ni sahihi ya Diesel Engine

Malya: Bwire alikuja Nyuma yako

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Ulikwenda South Africa Kufanya Mafunzo lini

Shahidi: 2010

Malya: Ukawa Mwanafunzi Bora

Shahidi: Hapana

Malya: Kwanini ulipewa zawadi ya Bunduki

Shahidi: Mheshimiwa Jaji, Inaonyesha Jinsi gani Wakili anataka Kuniweka Maneno Mdomoni, Labda yeye ndiyo alipewa Bunduki baada ya kufuzu Law School, anataka Kuficha Uhalifu

Malya: Ulipewa award gani

Shahidi: Sikupewa Award

Malya: Lakini wewe Ulifuzu

Shahidi: Ndiyo

Malya: Wakati Unakwenda Darfur Mara ya kwanza ulikuwa koplo?

Shahidi: Ni sahihi

Malya: na kwenye Jeshi koplo siyo Afisa

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakili ananitaka nieleze Kamisheni ya Kijeshi

Jaji: amekuuliza koplo ni Afisa siyo Afisa

Shahidi: Ni Afisa

Malya: Wakati Unakwenda Darfur ulikuwa na Ling'wenya kinachokufanya umkane Ni Kitu gani

Shahidi: Sijamkana, Siwezi Kukumbuka kama Nilikuwa naye

Malya: Shahidi Wewe ni Luteni Wa Jeshi, Je una Degree?

Shahidi: Hapana

Malya: Huna Digrii lakini ni Luteni wa Jeshi

Shahidi: Ndiyo

Malya: Adamoo na Ling'wenya Mlipoachana Morogoro alikwenda Wapi

Shahidi: Walikwenda Dar es Salaam

Malya: Naomba Kielelezo D1, Maelezo aliyo andika Kingai ambapo anasema alimuhoji Ling'wenya akakiri, Soma hapa

Shahidi: Luteni Urio alitupa nauli TSh 87,000 nauli ya kwenda Moshi

Malya: na wewe Umesema Walitoka Kwako Walikwenda Wapi

Shahidi: Nimekwambia Dar es Salaam Siyo Moshi

Malya: Kwenye Nauli uliwapa TSh ngapi

Shahidi: TSh 199,000

Malya: hapo Wao Wameamdika uliwapa TSh Ngapi

Shahidi: Nauli TSh 87,000, Ndivyo walivyo andika wao

Malya: Ulielezea Shahidi Kwenye Ushahidi Wako namba Uliyotumia Kuwasiliana na Bwire ni Namba gani

Shahidi: Sikueleza

Malya: Wakati Mnaenda Kuonana na Swila Mara ya Kwanza Ilikuwa lini

Shahidi: Tarehe 11 August 2020

Malya: Ndiyo Siku hiyo ulitoa Maelezo Yako

Shahidi: Ndiyo

Malya: Nimesikia Siku Unakutana na DCI Mlikutana baadae akaja Kingai

Shahidi: sahihi

Malya: Ulielezea Kuna mtu Yoyote alikuja Kuwa Join Baadae

Shahidi: Kuwa Join wapi?

Malya: Kwenye Kikao cha Siku hiyo na DCI na Kingai

Shahidi: Hakuna Mtu yoyote alikuja Kutujoin Siku hiyo

Malya: Kwenye Meseji ya Mwisho ambayo Mbowe alikutumia, Ukasema Hukueleza, ni kwanini hukutuma Meseji Nyingine Kuuliza Una maana gani

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Baada ya Kupita Muda Hakuna Mawasiliano, Nilimuuliza Bwire Boss wako anajua, Sasa ningejibu Meseji ya Nini

Malya: Na ni Ushahidi Wako Kwamba Ofisi za Swila ni Ghorofa ya Nane Makao Makuu

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Mheshimiwa nafikiri Sina Swali la Ziada kwa Shahidi huyu

Anasimama Adv. Dickson Matata

Matata: Nikumbushe Ulionana na Mbowe Tarehe ngapi

Shahidi: Mwezi Wa Saba, 2020 Sikumbuki Tarehe gani

Matata: Na Ulipo Onana naye ndiyo alikwambia anahitaji Vijana Wa Kuambatana naye wa Kuchukua dola

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Kwa Maelezo yako Ndiyo alikwambia anahitaji Vijana hao Vijana Kwa ajili ya Kumsaidia Kuwashambulia Viongozi ambao hawaupendi Upinzani

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Na Ndipo alipokwambia Kwamba anataka Kuhakikisha anachoma Masoko na Vituo Vya Mafuta

Shahidi: Naomba Ni'refresh alisema Kwamba ataleta Taharuki Kwa Kufanya hayo Uliyo niambia

Matata: juzi Ulisema Kwamba Ulifanya Kitu kinaitwa Tactical appreciation, na Mimi Leo nataka tufanye Tactical appreciation ya Kisheria, Wakati anakwambia Mlikuwa Wawili

Shahidi: Ndiyo

Matata: Kwa Lugha Nyingine Hapakwepo na Watu wengine

Shahidi: Sahihi

Matata: tofauti na Siku hiyo, Kuna Siku yoyote aliwahi Kukwambia Jambo hilo au kukuandikia Barua

Shahidi: Hakuna

Matata: Kwa hiyo kwa tafsiri nyingine hatutopata ushahidi wa maandishi au wa sauti au meseji unaoweza kuthibitisha kuwa alikwambia hayo maneno?

Shahidi: Hakuna sauti

Matata: Baada ya Kukwambia Ukaona Inafaa ukatoe Taarifa, Ukaenda kwa DCI, Kwanza Ulimpigia Simu halafu akakupa appointment

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Na Kwamba Baada ya Kumueleza akamuita Kingai

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Utakubaliana na Mimi Kwamba DCI ni Mtu Mwenye Ujuzi Katika Upelelezi

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Kingai alikuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Unafahamu Kwamba anakuwa na uzoefu wa Upelelezi

Shahidi: Kwanza Nilikuwa sijui kuwa ni Mpelelezi

Matata: Mtu akiwa Mpelelezi Wa Mkoa ana uzoefu au hana Uzoefu

Shahidi: anakuwa na Uzoefu

Matata: Wewe Kama Komandoo, Katika Kikao hicho na Baada ya Hapo, Hukuona wewe au DCI na Kingai, Hukuona Kuwa Kuna Umuhimu kuwa Msiridhike Kile ambacho umesema, Je Hukuona Kuwa Kuna Umuhimu Wa Kurekodi Voice Notes

Shahidi: Mamlaka labda Ndiyo haikuona Umuhimu

Matata: Wewe Uliona Kuna Umuhimu au Hakuna Umuhimu, Kwamba Usiridhike na Maneno Utengeneze Voice Record

Shahidi: Niliona Kuna Umuhimu

Matata: kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vitasema Exactly Kuwa anataka Kulipua
Masoko

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Mbowe alikuwa alishaniambia Kwa Meneno, asingerudia

Matata: Narudia Swali langu, kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vita, sema Exactly Kuwa anataka Kulipua Masoko

Shahidi: Sikuwa na Vifaa Vya kunasa Sauti

Matata: Freeman Mbowe akikataa leo hakusema, ni ushahidi gani unao mbele ya Mahakama Kwamba Mbowe alisema hayo maneno uliyosema?

Shahidi: Ni ushahidi wa meseji ya kusema "muda umeisha"

Matata: hiyo meseji inayosema muda umeisha ina sehemu inasema kulipua masoko

Shahidi: Hakuna mahali inasema

Matata: hiyo Meseji ina sehemu inasema kushambulia viongozi ambao hawapendi upinzani?

Shahidi: Hakuna mahali inasema hivyo

Matata: Hiyo meseji kuna sehemu inasema kulipua vituo vya mafuta

Shahidi: hakuna mahali inasema hivyo
Mjue shahidi ni komandoo na wala si mtu mjinga mjinga
angalia Comedian Mh. Matata anavyojiingiza mdomoni mwa komandoo Urio

Matata: kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vitasema Exactly Kuwa anataka Kulipua
Masoko

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Mbowe alikuwa alishaniambia Kwa Meneno, asingerudia

Matata: Narudia Swali langu, kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vita, sema Exactly Kuwa anataka Kulipua Masoko

Shahidi: Sikuwa na Vifaa Vya kunasa Sauti
 
Huyu Urio ana aibisha jeshi tu, majipu gani haya anajibu
Screenshot_20220128_114956.jpg
 
na mukae kwa kutulia sindano zinakuja ,mutu wenu shayidi ana kesi ya kujibu.tena amepasuwa simu isiwake ili siri zisijulikane.NURU ITALISHINDA GIZA
shahidi ana kesi ya kujibu? wakati hata kushitakiwa hajashitakiwa? na wanaoweza kuamua ashitakiwe au la ni wale waliomwita kama shahidi, na hapohapo unaamini una akili? mnafikiri kwa kutumia kamasi aisee.
 
Kesi ya makomandoo iliisha jana baada ushahidi wa Urio, kesi ya Mbowe imebaki sehemu ndogo sana, Mbowe kusema tu hakumwambia shahidi Urio, then kesi yote itakua imeisha mana Urio keshasema Hana uthibitisho wowote na hawakuwai kujadili tena kuhusu ugaidi.
Anasema uthibitisho wa Ugaidi wa Mbowe Ni msg iliyoandikwa 'Muda umeisha' [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Mh. Jaji kwa mamlaka uliyonayo maliza hii kesi - hamna kesi humu ni kupotezeana muda na kulighalimu taifa.

Matata: Freeman Mbowe akikataa leo hakusema, ni ushahidi gani unao mbele ya Mahakama Kwamba Mbowe alisema hayo maneno uliyosema?

Shahidi: Ni ushahidi wa meseji ya kusema "muda umeisha"

Matata: hiyo meseji inayosema muda umeisha ina sehemu inasema kulipua masoko

Shahidi: Hakuna mahali inasema

Matata: hiyo Meseji ina sehemu inasema kushambulia viongozi ambao hawapendi upinzani?

Shahidi: Hakuna mahali inasema hivyo

Matata: Hiyo meseji kuna sehemu inasema kulipua vituo vya mafuta

Shahidi: hakuna mahali inasema hivyo
 
Matata: Freeman Mbowe akikataa leo hakusema, ni ushahidi gani unao mbele ya Mahakama Kwamba Mbowe alisema hayo maneno uliyosema?

Shahidi: Ni ushahidi wa meseji ya kusema "muda umeisha"

Matata: hiyo meseji inayosema muda umeisha ina sehemu inasema kulipua masoko

Shahidi: Hakuna mahali inasema

Matata: hiyo Meseji ina sehemu inasema kushambulia viongozi ambao hawapendi upinzani?

Shahidi: Hakuna mahali inasema hivyo

Matata: Hiyo meseji kuna sehemu inasema kulipua vituo vya mafuta

Shahidi: hakuna mahali inasema hivyo

Kwahio kusema "muda umeisha" ndio ushahidi wa ugaidi[emoji28]dah!
Nchi inachezewa hii
 
Huwa tunaaminishwa tuna jeshi na askari bora kwa ukanda wetu wa east Africa,dah!! nimemsikiliza Luteni wetu anavyojichanganya kujibu maswali..namashaka sana na vikosi vyetu.
 
Yaani hadi kufikia leo hakuna sehemu hata moja inayojaribu kuonesha palikuwa na njama za kupanga vitendo vya kigaidi.

Halafu kamanda zero aliuhakikishia umma kwamba wanao ushahidi mzito na wa kutosha juu ya vitendo vya njama za ugaidi.

Halafu eti kamanda zero naye ni mwanasheria ambaye baada ya kusoma meseji hizo akajiridhisha kwamba wana ushahidi wa kutosha.

Hii kada yetu pendwa ya sheria inaharibiwa na vilaz.a wachache. Inakera sana.
 
Back
Top Bottom