Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

sasa maswali kama haya yamesaidia nini mbowe? kama eye witness na mtu aliyekuwa anawasiliana naye na kukutana naye anasema mpango wa ugaidi ulikwepo, hata kama kamati ya ulinzi na usalama au yeyote hata kuwa na taarifa inahusu nini? ndio wanasheria wenu hao. hapo laymen huko mtaani wanashangilia ati ameuliza maswali magumu.
Nani kakuambia ugaidi unathibitishwa kwa maneno ya kusikia..?
 
Luteni ama Afisa wa JWTZ anaona uhalifu unataka kutendeka, option anayochukua ni kumtafuta DCI ambaye yupo mbali badala ya kwanza kuriport kambi iliyo karibu kabisa na eneo ambalo walifanya mkutano na Mbowe ili kuzima tukio nzima kwa uharaka.

Sasa tukisema huyu Luteni ni BOYA kabisa tutakuwa tumesema urongo ndugu zangu ?
 
kikubwa alichofanikiwa kuthibitisha hapo ni kwamba, at least kulikuwa na communication kati yake na mbowe jambo ambalo linaweza kuback up oral testimony yake, ukizingatia kwamba ukishaona mahakama imemuamini kwenye kitu kimojawapo hapo (ambacho kwenye communication na ukiunganisha na alichokisema ling'wenya), basi credibility imeshajengwa. na ili mahakama imkatae inatakiwa kutoa sababu ambayo hapo sijaiona kama itakuwepo wakati kwenye ushahidi wa yeye kuwasiliana na hao ameshathibitisha kwa print out hizo za simu. every witness is entitled to credence, na ukiamua kutomwamini lazima utoe sababu, la sivyo anakuwa credible na ushahidi wake which includes oral testimony unatakiwa uaminiwe na ufanyiwe kazi. kwa mwanasheria hapo ameshanielewa.
Ma bush lawyer wa lumumba mnajua kuhara pumba mkuu. Ya sheria waachieni wa taalam wa sheria.
 
Shahidi katoroka, anasakwa arejeshwe kizimbani.
elimu ya jamaa ndiyo kikwazo - Three ya 25 ni parefu hapo !! as results tunapata Afisa wa JWTZ asiye na uelewa wa mambo.

Hawezi kukimbia kashaingia kwa 18 za Kibatala - bado kidogo tu ataanza kumwita Kibatara Mweshimiwa..... 😁😁😁
 
Habari Wakuu,

Leo tena shahidi wa 12 Denis Urio anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Fuatana nami kupata yatakayojiri

UPDATES:

Jaji ameingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili

  • Pius Hilla
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Ignasi Mwinuka
  • Mawakili wa Serikali Waandamizi na Tulimanywa Majige, Wakili wa Serikali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ikikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili

  • Seleman Matauka
  • Alex Massaba
  • Paul Kisabo
  • Sisty Aloyce
  • Maria Mushi
  • Khadija Aron
  • Michael Lugina
  • Evaresta Kisanga
  • John Mallya
  • Nashon Nkungu
  • Dickson Matata

Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo Tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea

Shahidi anapanda Kizimbani

Jaji: Shahidi Jana Ulikuwa Unatoa Ushahidi Wako, Unaulizwa Maswali Chini ya Kiapo na Leo Utaendelea Kuulizwa Maswali Chini ya Kiapo

Wakili John Mallya: Shahidi tunaendelea tulipo Ishia Jana, Mheshimiwa Jaji Naomba Jibu lake la Mwisho

Jaji: ni Kwamba Asipotumia Jina Namba zake Jina lake halitoonekana...

Malya: hivi kazi ya VIP PROTECTION Inafanyikaje

Shahidi: Mheshimiwa Jaji kazi ya VIP PROTECTION Inafanyika kwa mtu yoyote, Kwa Kufuata Sheria na Kanuni za Nchi

Malya: Ni sahihi Kwamba kazi Wanazofanya VIP protection Ni lazima wawe naye Kwa Wajibu wa Kum' protect

Shahidi: Ni sahihi Malya: hawa VIP protection Ni sawa na Body guard?

Shahidi: Sijawahi Kusikia Body Guard mimi

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba 26

Malya: Umesema kuwa hawa VIP protection Wanakuwa pamoja na Wanayem' protect, sasa ni somee Meseji ya Tarehe 20 July 2020, Ya Saa Mbili Asubuhi

Shahidi: Hawa wawili Kuanzia Siyo Mbaya Hawawezi Kutelekezwa, Nitakuwa nao Full time

Malya: Kwa Kazi gani

Shahidi: Ulinzi Ndiyo

Malya: Je, kuna meseji nyingine yoyote kwamba kuna mahali Mbowe anasema nitawatuma Kufanya kazi nyingine au uhalifu?

Shahidi: kwenye meseji hazipo

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo Namba 35

Malya: Tumeletewa report kule ulikopeleka simu , Je hii namba ina Jina gani?

Shahidi: Imeandikwa FREE... Ambayo ni namba ya Freeman Aikael Mbowe

Malya: Very Good shahidi umeniongezea information nilikuwa sijui, sasa washa simu yako

Shahidi anabonyeza simu, anasema tayari

Malya: Unasema Ulikuwa Unawasiliana na Mbowe Kupitia Mtandao Wa Telegram

Shahidi: Ndiyo Mtandao Wa Telegram

Malya: Naomba usogee kwa Mheshimiwa Jaji pale kamuonyeshe namba unayosema ume-chat na Mbowe. Je, hapa kuna Jina FREE linaonekana, ukiwa umefungua meseji?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji HAKI YA MUNGU hii ni akaunti ya Mbowe siyo Group, nafungua

Malya: Jina Free Ukifungua Meseji linaonekana au halionekani?

Shahidi: Halionekani lakini ni Akaunti ya Mbowe

Malya: Je, ulitoa Ufafanuzi/Maelezo kuwa Jina FREE halionekani?

Shahidi: Si nilimjibu mimi Bwana, Mimi siyo Mtaalamu Wa IT, Sasa nitoe Maelezo Ya nini

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba atoe jibu

Jaji: Umeelewa Swali? Kwamba Wakati Unasoma Ulitoa Ufafanuzi? Kuwa jina halionekani

Shahidi: Ufafanuzi huo sikutoa

Mahakama: (Kicheko)

Malya: Haya Ulisema Kwamba Mbowe alikuwa nakupa Wishes za Christmas na Mwaka Mpya, je Meseji zimeanza lini

Shahidi: Tarehe 20 July 2020

Malya: Alikuwa anakutakia Heri ya Mwaka Mpya Kupitia nini

Shahidi: alikuwa ananipigia Simu

Malya: Alikuwa anakupigia simu kwa njia ipi

Shahidi: Kwa Telegram

Malya: Je, unafahamu kwamba ukipiga Simu Telegram unabakia na Calls Record

Shahidi: Sina Utaalamu huo

Malya: Je Jana Wakati wa Ushahidi Wako Kama Ulituonyesha WhatsApp Calls na Meseji za Mbowe

Shahidi: aliyechunguza ndiye anafahamu

Malya: Kwa hiyo Mtaalamu anaweza Kuwa amepunguza au ameongeza?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi hajasema hivyo

Malya: Nitauliza Upya Kuokoa muda, Kilichokufanya Jana usitoe Calls za WhatsApp

Shahidi: nilisema kwamba Mimi Nilikuwa na wasiliana na Mbowe Kwa WhatsApp, Meseji na Telegram

Malya: Sawa Jana Ulionyesha WhatsApp Call wakati wa Ushahidi Wako?

Shahidi: Sikuonyesha

Malya: Ulionyesha namba zingine ambazo Ulikuwa Mbowe alikuwa anakupigia Simu

Shahidi: Sikuonyesha

Shahidi: (Ghafla) Sikuonyesha Kwa sababu..

Malya: sitaki sababu hapa

Shahidi: Sikuonyesha Kwa sababu

Malya: Sijakuuliza kuhusu sababu

Jaji: Shahidi sikiliza swali ndiyo ujibu

Malya: Naomba Kielelezo Namba 28

Malya anamkabidhi shahidi

Malya: Jana ulishindwa Kuiwasha hii simu

Shahidi: Sikushindwa, haikuwaka

Malya: Ulitoa Explanation Kwanini ilishindwa Kuwaka

Shahidi: Nilieza Kwamba simu ina ibovu wa Display, Ukiwasha Hai Display Kitu chochote

Malya: Kama kuna Taarifa ya Muhimu ambayo Mbowe anataka Kujitetea Kutumia hiyo Simu atafanyeje, Utampa akatengeneze

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakati natoa Ushahidi Wangu Kuhusu Kukabidhi Simu, Nilisema, Nilienda na Simu moja, Sikujua Kama Nilitakiwa Kukabidhi Simu, Nikauliza kwa sababu gani wakasema sababu ya Uchunguzi, Tarehe 10 nilipeleka simu zingine, na Mimi nilipeleka Simu Ikiwa imedondoka haifanyi kazi

Malya: Aliyechunguza hajasema Kwamba Simu Mbovu, Isipokuwa wewe unaogopa kwa sababu unajua Kilichopo humo hutaki kionekane

Shahidi: Washa wewe

Malya: Mimi siwezi Kuwasha Simu yako

Shahidi: basi awashe hata Mheshimiwa Jaji

Malya: wewe Ndiyo Mwenye Simu Shahidi: basi hayo Mengine ni Maoni

Malya: Kuna report ya hii Simu, Je Jana Ulionyesha Call Logs za mbowe

Shahidi: Sikuonyesha

Malya: Calls za Khalfani Bwire Jana Ulionyesha

Shahidi: Sikuonyesha, Sababu sikuulizwa

Malya: Je, jana Ulionyesha Meseji za Ling'wenya Kuhusu Kuwasiliana nao wasikengeuke

Shahidi: Sikuonyesha sababu sikuziona

Malya: Ni sahihi unasema Kwamba a baada ya kuwapeleka Vijana Wanne Kwa Mbowe Mwisho wa Kuwasiliana naye ilikuwa Tarehe 24

Shahidi: Ndiyo

Malya: Wakati Mbowe anaacha Kupokea Simu yako alikuwa tayari na Vijana Wanne

Shahidi: Ndiyo

Malya: Soma hapa

Shahidi: Kaka Wale Mtu 3 au 4 Ni Muhimu

Malya: Sasa kama Umeshampa Mtu Nne ukitaka uwasiliane naye nini

Shahidi: Nilichokitaka Kwake baada ya kukikosa nikakipata kwa Bwire

Malya: Kwa hiyo Wakati anaacha Kuwasiliana na wewe Hitaji lake alikuwa ameshalimaliza

Shahidi: Ndiyo

Malya: Miji ya Arusha, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza ina masoko mangapi?

Shahidi: Mimi sifahamu anafahamu Mbowe

Malya: Miji niliyotaja ina vituo vya mafuta vingapi?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji najibu swali kama Ifuatavyo anayejua idadi ya vituo vya mafuta ambavyo alipanga kulipua ni Freeman Mbowe

Malya: Shahidi Miji hiyo ina Mikusanyiko Mingapi

Shahidi: Mheshimiwa Jaji mimi sijui ina mikusanyiko mingapi, Ila Mheshimiwa Mbowe ndiye anajua kwa sababu alipanga kulipua

Malya: Ulifika Ofisi za DCI Je Ulifika ukiwa na Simu zako

Shahidi: Ndiyo

Malya: Je, ulieleza Jana Kama Ulikuwa na Simu zako

Shahidi: Mheshimiwa Jaji nilifika kwa DCI nikampa Taarifa, akasema endelea nao

Malya: Maelezo Yako Mazuri ila siyahitaji, Swali langu Ulieleza Kama Ulimuonyesha DCI Simu zako na Mawasiliano ya Mbowe?

Shahidi: Sikueleza

Malya: Unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Kurekodi?

Shahidi: Mimi sifahamu

Malya: Je, unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Upelelezi

Shahidi: Mimi sifahamu Kwa sababu, Kazi yangu haikuwa Kufanya Upelelezi Bali Kutafuta Watu wa Kufanya Kazi

Malya: Wakati Khalfani Bwire, Je alikwambia Vifaa wanavyokwenda Kuvitumia

Shahidi: Hakuniambia

Malya: Wakati Unaingia Jeshini ulikuwa na Certificate ya Form Four na Certificate Ya Ufundi

Shahidi: Ni sahihi ya Diesel Engine

Malya: Bwire alikuja Nyuma yako

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Ulikwenda South Africa Kufanya Mafunzo lini

Shahidi: 2010

Malya: Ukawa Mwanafunzi Bora

Shahidi: Hapana

Malya: Kwanini ulipewa zawadi ya Bunduki

Shahidi: Mheshimiwa Jaji, Inaonyesha Jinsi gani Wakili anataka Kuniweka Maneno Mdomoni, Labda yeye ndiyo alipewa Bunduki baada ya kufuzu Law School, anataka Kuficha Uhalifu

Malya: Ulipewa award gani

Shahidi: Sikupewa Award

Malya: Lakini wewe Ulifuzu

Shahidi: Ndiyo

Malya: Wakati Unakwenda Darfur Mara ya kwanza ulikuwa koplo?

Shahidi: Ni sahihi

Malya: na kwenye Jeshi koplo siyo Afisa

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakili ananitaka nieleze Kamisheni ya Kijeshi

Jaji: amekuuliza koplo ni Afisa siyo Afisa

Shahidi: Ni Afisa

Malya: Wakati Unakwenda Darfur ulikuwa na Ling'wenya kinachokufanya umkane Ni Kitu gani

Shahidi: Sijamkana, Siwezi Kukumbuka kama Nilikuwa naye

Malya: Shahidi Wewe ni Luteni Wa Jeshi, Je una Degree?

Shahidi: Hapana

Malya: Huna Digrii lakini ni Luteni wa Jeshi

Shahidi: Ndiyo

Malya: Adamoo na Ling'wenya Mlipoachana Morogoro alikwenda Wapi

Shahidi: Walikwenda Dar es Salaam

Malya: Naomba Kielelezo D1, Maelezo aliyo andika Kingai ambapo anasema alimuhoji Ling'wenya akakiri, Soma hapa

Shahidi: Luteni Urio alitupa nauli TSh 87,000 nauli ya kwenda Moshi

Malya: na wewe Umesema Walitoka Kwako Walikwenda Wapi

Shahidi: Nimekwambia Dar es Salaam Siyo Moshi

Malya: Kwenye Nauli uliwapa TSh ngapi

Shahidi: TSh 199,000

Malya: hapo Wao Wameamdika uliwapa TSh Ngapi

Shahidi: Nauli TSh 87,000, Ndivyo walivyo andika wao

Malya: Ulielezea Shahidi Kwenye Ushahidi Wako namba Uliyotumia Kuwasiliana na Bwire ni Namba gani

Shahidi: Sikueleza

Malya: Wakati Mnaenda Kuonana na Swila Mara ya Kwanza Ilikuwa lini

Shahidi: Tarehe 11 August 2020

Malya: Ndiyo Siku hiyo ulitoa Maelezo Yako

Shahidi: Ndiyo

Malya: Nimesikia Siku Unakutana na DCI Mlikutana baadae akaja Kingai

Shahidi: sahihi

Malya: Ulielezea Kuna mtu Yoyote alikuja Kuwa Join Baadae

Shahidi: Kuwa Join wapi?

Malya: Kwenye Kikao cha Siku hiyo na DCI na Kingai

Shahidi: Hakuna Mtu yoyote alikuja Kutujoin Siku hiyo

Malya: Kwenye Meseji ya Mwisho ambayo Mbowe alikutumia, Ukasema Hukueleza, ni kwanini hukutuma Meseji Nyingine Kuuliza Una maana gani

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Baada ya Kupita Muda Hakuna Mawasiliano, Nilimuuliza Bwire Boss wako anajua, Sasa ningejibu Meseji ya Nini

Malya: Na ni Ushahidi Wako Kwamba Ofisi za Swila ni Ghorofa ya Nane Makao Makuu

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Mheshimiwa nafikiri Sina Swali la Ziada kwa Shahidi huyu

Anasimama Adv. Dickson Matata

Matata: Nikumbushe Ulionana na Mbowe Tarehe ngapi

Shahidi: Mwezi Wa Saba, 2020 Sikumbuki Tarehe gani

Matata: Na Ulipo Onana naye ndiyo alikwambia anahitaji Vijana Wa Kuambatana naye wa Kuchukua dola

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Kwa Maelezo yako Ndiyo alikwambia anahitaji Vijana hao Vijana Kwa ajili ya Kumsaidia Kuwashambulia Viongozi ambao hawaupendi Upinzani

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Na Ndipo alipokwambia Kwamba anataka Kuhakikisha anachoma Masoko na Vituo Vya Mafuta

Shahidi: Naomba Ni'refresh alisema Kwamba ataleta Taharuki Kwa Kufanya hayo Uliyo niambia

Matata: juzi Ulisema Kwamba Ulifanya Kitu kinaitwa Tactical appreciation, na Mimi Leo nataka tufanye Tactical appreciation ya Kisheria, Wakati anakwambia Mlikuwa Wawili

Shahidi: Ndiyo

Matata: Kwa Lugha Nyingine Hapakwepo na Watu wengine

Shahidi: Sahihi

Matata: tofauti na Siku hiyo, Kuna Siku yoyote aliwahi Kukwambia Jambo hilo au kukuandikia Barua

Shahidi: Hakuna

Matata: Kwa hiyo kwa tafsiri nyingine hatutopata ushahidi wa maandishi au wa sauti au meseji unaoweza kuthibitisha kuwa alikwambia hayo maneno?

Shahidi: Hakuna sauti

Matata: Baada ya Kukwambia Ukaona Inafaa ukatoe Taarifa, Ukaenda kwa DCI, Kwanza Ulimpigia Simu halafu akakupa appointment

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Na Kwamba Baada ya Kumueleza akamuita Kingai

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Utakubaliana na Mimi Kwamba DCI ni Mtu Mwenye Ujuzi Katika Upelelezi

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Kingai alikuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Unafahamu Kwamba anakuwa na uzoefu wa Upelelezi

Shahidi: Kwanza Nilikuwa sijui kuwa ni Mpelelezi

Matata: Mtu akiwa Mpelelezi Wa Mkoa ana uzoefu au hana Uzoefu

Shahidi: anakuwa na Uzoefu

Matata: Wewe Kama Komandoo, Katika Kikao hicho na Baada ya Hapo, Hukuona wewe au DCI na Kingai, Hukuona Kuwa Kuna Umuhimu kuwa Msiridhike Kile ambacho umesema, Je Hukuona Kuwa Kuna Umuhimu Wa Kurekodi Voice Notes

Shahidi: Mamlaka labda Ndiyo haikuona Umuhimu

Matata: Wewe Uliona Kuna Umuhimu au Hakuna Umuhimu, Kwamba Usiridhike na Maneno Utengeneze Voice Record

Shahidi: Niliona Kuna Umuhimu

Matata: kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vitasema Exactly Kuwa anataka Kulipua
Masoko

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Mbowe alikuwa alishaniambia Kwa Meneno, asingerudia

Matata: Narudia Swali langu, kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vita, sema Exactly Kuwa anataka Kulipua Masoko

Shahidi: Sikuwa na Vifaa Vya kunasa Sauti

Matata: Freeman Mbowe akikataa leo hakusema, ni ushahidi gani unao mbele ya Mahakama Kwamba Mbowe alisema hayo maneno uliyosema?

Shahidi: Ni ushahidi wa meseji ya kusema "muda umeisha"

Matata: hiyo meseji inayosema muda umeisha ina sehemu inasema kulipua masoko

Shahidi: Hakuna mahali inasema

Matata: hiyo Meseji ina sehemu inasema kushambulia viongozi ambao hawapendi upinzani?

Shahidi: Hakuna mahali inasema hivyo

Matata: Hiyo meseji kuna sehemu inasema kulipua vituo vya mafuta

Shahidi: hakuna mahali inasema hivyo

Matata: Tutoke hapo, Unasema Ulienda Kwa DCI na Kabla ya kwenda Ulimpigia Simu,

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Ulielezea Mahakama Kwamba Ulikuwa Unafahamiana na DCI

Shahidi: Nilieleza, Kuna Mtu aliuliza Kama Nilienda Ofisi ya DCI Mara ngapi

Matata: Mimi Sitaki Habari ya Kwenda Ofisini, DCI Anabadirika, nakuuliza Kama Ulielezea Kwamba Unafahamiana na DCI

Shahidi: Sikueleza

Matata: Ulieleza Mahakamani hapa Kwamba Namba yake Ulipata Wapi

Shahidi: Sikueleza

Matata: Hata hiyo namba yenyewe Ulitaja

Shahidi: Sikutaja

Matata: Ushahidi gani Unathibitisha Kwamba Ulimpigia Simu

Shahidi: Ushahidi ninao kwa sababu nina namba zake na Nilifika Ofisini Kwake

Shahidi: Je ulivitaja hivyo Vitu Wakati Unahojiwa na Upande wa Mashitaka

Shahidi: Sikuvitaja

Matata: Unasema Kwamba Ulienda Kesho Ukasema Una Appointment naye Ukakutana na Secretary Wake

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Kwa Maana hiyo Ulifuata Utaratibu wa Umma Wa Jinsi ya Kuingia Ofisi Fulani

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Ulisema Kwamba Ulipofika Ulifuata taratibu za Ofisi za Umma

Shahidi: Nilieleza Kwamba, Nilionyesha Kitambulisho kama Askari

Matata: Ulisema Kwamba Askari apaswi Kufuata Utaratibu Wa Kuingia Ofisi Za Umma

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Mimi Nilieleza Kuwa ni Askari, yeye Ndiye alitakiwa aniambie Kufuata Utaratibu

Matata: Wakati Unahojiwa na Wakili wa Serikali Abdallah Chavula, Ulisema Kwamba Nyie Askari hamfuati Utaratibu

Shahidi: Sikueleza

Matata: Ulileta Visitors Book Kuonyesha Kweli Ulienda Ofisi Za DCI

Shahidi: Hapana Sikuleta

Matata: Shahidi Wewe ni Mwanajeshi, Ulitakiwa Kufuata Taratibu zote za Kijeshi

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Unapotoka Mkoa Mmoja Kwenda Mkoa Mwingine, unatakiwa Kuwa na Movement Order

Shahidi: Inategemea na Siku Ngapi, Kama Chini ya Siku Tatu unaweza Kwenda bila Movement Order kama zaidi ya Siku Nne Unatakiwa Kuwa na Movement Orde

Matata: Wakati Unahojiwa na Wakili Abdallah Chavula Uliyasema hayo

Shahidi: sikuyasema

Matata: Unapokuwa Askari Unapoenda Ofisi za Umma si lazima Uwe na Pass

Shahidi: Ni kwenye Kitabu Unachotaka,

Matata: Si lazima uonyeshe Pass

Shahidi: Ndiyo ni lazima

Matata: Umeleta Mahakamani hapa Pass Kwamba Umeruhusiwa Kutoka kazini Kwako

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Sijaleta Sikujua I nahitajika Mahakamani

Matata: Tarehe 11 ulienda kwa Inspector Swila na Tarehe 12 Ulimpelekea Simu

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Ulileta Mahakamani Hapa Pass za Umeruhusiwa

Shahidi: Sikuleta, Sikupewa Maelezo

Matata: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo Namba 20

Matata: Naomba Nikuonyesha Kielelezo namba 20 ambacho Kina Miamala yako ya namba ya Airtel

Matata: Jana Wakati Unahojiwa ulisema Freeman Mbowe alikurushia Kwa Mara ya Kwanza TSh 500,000

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Na Ukatoa TSh 499,000

Shahidi: Kweli

Jaji: Umeelewa Swali? Anasema Umetumiwa TSh 500,000, Swali Ukatoa kwenye hiyo Fedha kiasi gani?

Shahidi: Ni TSh 499,000

Matata: Kwa Mantiki Nyingine Hukutoa yote Kwa sababu Kuna Makato kidogo

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Kwa hiyo Ulichukua TSh 500,000 Ukatoa TSh 499,000 Je Makato TSh ngapi?

Shahidi: TSh 1000

Matata: Naomba Nikuonyeshe Kwa Siku hiyo, Mheshimiwa Jaji Namuonyesha Muamala Wa Siku hiyo ambapo anasema alitoa Muamala Wa TSh 499,000

Matata: Sasa Shahidi angalia Tarehe 20 July 2020, Kwenye Miamala sehemu ambayo Umeenda Kwa Wakala Ukatoa TSh 499,000

Jaji: anakuuliza Hapo Hapo hapo Kwenye hiyo Nyaraka

Shahidi: Hapa Kwenye Miamala Haipo hiyo 499,000

Matata: Mheshimiwa Jaji naomba ni Muonyeshe Hapo hapo, Kuna Majedwali ambayo Yanaonyesha Receiver Balance kabla ya kutumiwa TSh 500,000 kutoka Kwa Mbowe.. Utakubaliana na Mimi Kwenye akaunti yako palikuwa na TSh 49,646

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Baada ya Kuweka TSh 500,000 balance Ikawa TSh 549,646

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Na Tarehe hiyo hiyo Ukatoa TSh 300,000

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Na Balance Yako Ikabakia 243,646

Shahidi: Ni sahihi

Matata: hebu chukua salio uliokuwa nalo la 549,646 Kutoa 300,000 ukabaki na 243,646 tuone Makato ni TSh ngapi

Amesimama Mmoja Wakili wa Serikali Robert Kidando

Wakili wa Serikali Robert Kidando: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Naona Hajajengewa Misingi Kwamba wakili anauliza ikiwa hayo Makato yapo au hayapo..

Matata: Mheshimiwa Jaji Mimi lengo langu nikutaka kujua kwanini Shahidi atoe TSh 499,000 akatwe TSh 1,000 na atoe TSh 300,000 akatwe Elfu Sita na usheeee..

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hicho ndicho alichopaswa Kuulizwa

Matata: Je Shahidi Utakubaliana na Mimi Kwamba Ukitoa TSh 300,000 ikibakia TSh 243,646 Je Elfu 6 inaenda Wapi?

Shahidi: Siwezi Kujua Kama ni Makato au imeenda wapi

Matata: Kwani hiyo Tsh 1000 Mwanzo Ulijuaje Kama ni Makato

Shahidi: (Kimya)

Jaji: Swali lako la Mwisho liasema Kuhusu Elfu 6 nimesharekodi

Mallya anasaidia kufafanua kidogo

Matata: Shahidi Ulitoa maelezo hii TSh 1,000 Ilienda wapi

Shahidi: Sijawahi Kutoa

Matata: Shahidi sasa ulitoa...sorry Mheshimiwa Jaji Kidogo

Matata anapekua Nyaraka hapa

Matata: Shahidi Umesema Freeman Aikael Mbowe alikuwa na Mpango Wa Kulipua Vituo Vya Mafuta, Je Wakati Unahojiwa ulitaja Majina ya Vituo Vya Mafuta

Shahidi: Hakuniambia Vituo Vya mafuta anavyoenda Kulipua Bali alitaja Mikoa tu

Matata: Kwa hiyo ukiulizwa Alitaka Kulipua Vituo gani Morogoro hutakuwa na Majibu

Shahidi: Sitokuwa na Majibu kwa kweli

Matata: Tukisema Utaje Vituo Vya Mafuta alivyo taka Kulipua Mkoa wa Mwanza Utakuwa na Majibu au hutakuwa na Majibu

Shahidi: Mimi sina Majibu, Majibu atakuwa nayo Freeman Mbowe

Matata: Ukiulizwa pia Kuhusu Mkoa wa Dar es Salaam Vituo Vipi Vya Mafuta alitaka Kulipua

Shahidi: Mimi sina Majibu, Majibu anayo Freeman Mbowe, Mimi alinificha

Matata: Ukiulizwa ni eneo gani alipanga Kukata Miti kati ya Mkoa wa Morogoro na Iringa

Shahidi: Hakuniambia ni Eneo gani

Matata: Ukiulizwa, Ukiachana Na Sabaya ni Viongozi gani wengine Walipanga Kuwashambulia

Shahidi: Sikutaja Jina la Kiongozi Yoyote, Hakuniambia Kiongozi Yupi

Matata: Mpaka anakushirikisha bila Shaka alikuwa anakuamini

Shahidi: Ndiyo

Matata: Ukiachana na suala la Kumtafutia Vijana, Je alikueleza kuhusu kumtafutia vilipuzi

Shahidi: Hakunieleza

Matata: Kuhusu kumtafutia silaha za kuwashambulia viongozi

Shahidi: Hakunieleza

Matata: Naomba Kurejesha Kielelezo cha simu .. Ahsante

Mallya: Mheshimiwa Jaji, hata hivyo haiwaki.

Matata anaketi..

Anasimama Wakili Peter Kibatala

Kibatala:
Shahidi Nikikuita baba Careen ni sawa?

Shahidi: Ni sawa

Kibatala: Baba Junior

Shahidi: Ni Sawa

Kibatala: Baba Jackson

Shahidi: Ni sawa

Kibatala: Jackson amezaliwa Lini

Shahidi: 17 December 2020

Kibatala: Hospitali gani

Shahidi: Hospitali Ya Mkoa Morogoro

Kibatala: Nani na nani alikwepo

Shahidi: Mke wangu na Jirani

Kibatala: Wewe ni Mkristo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: unasali Kanisa lipi

Shahidi: Parokia Ya Ngerengere, Kigango cha Kizuka

Kibatala: Paroko wako Unamfahamu

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Kwani Kanisani Umeenda Mara ya Mwisho lini?

Shahidi: Juzi juzi

Kibatala: Paroko anayehudumu Ngerengere Unamfahamu

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Katekista anayemsadia Paroko

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: narudia tena Mara ya Mwisho Kanisani Umeenda Lini

Shahidi: Sikumbuki Kusema Kweli

Kibatala: Una Gari ya silver

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Aina gani

Shahidi: Rav 4

Kibatala: Namba zake zipi

Shahidi: T 114 DHL

Kibatala: Toka Mwaka 16 August 2020 hiyo Gari ipo Wapi

Shahidi: Kazini Kwangu Ngerengere

Kibatala: Toka Tarehe 16 August 2020 Gari hii ilikuwa parked Wapi

Shahidi: Nilikuwa natumia, Kila Nilipo ipo

Kibatala: Baada Tarehe 16 August 2020 Gari hii umeitumia

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Umekuja kutoka Morogoro kutoa ushahidi kwenye hii Kesi, na kwamba siyo kutoka kambi fulani ya Jeshi ulikokuwa umetekwa?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji (Shahidi kamuita Jaji hapa ana jambo gani?)

Kibatala: Ndugu shahidi RELAX..

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Mawakili Uliwakataza Kutoa Mawazo yao Bali Kuulizwa maswali

Kibatala: Shahidi hiyo Gari Ipo wapi

Shahidi: Kambini Kizuka

Kibatala: Umepeleka lini hiyo Gari

Shahidi: Ijumaa Wiki Iliyopita

Kibatala: Utaratibu gani Umetumika kupark hiyo gari

Shahidi: Park at Your Own Risk

Kibatala: Kwa hiyo wewe Kama afisa wa Jeshi unataka Kuniambia Kuwa Una park Gari at Owner's Risk Kambini, Upo serious kweli wewe?

Shahidi: Lipo Katika Parking ya Staff

Kibatala: Bado Kwamba Unaendelea Kusema Gari ipo Parking Owner's Risk?

Shahidi: Hapana Nimeliondoa jibu la Owner's Risk

Kibatala: Jibu lako la Kwanza kwamba Uli park Chini ya Owner's Risk Ulilitoa Chini ya Kiapo?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: haya, Turudi tena Kwamba Gari Umei' park Kwa Utaratibu gani

Shahidi: Pale Hakuna Ku'Register, Nilitoka Kwenye Oparation Nikaambiwa Nije kutoa Ushahidi

Kibatala: hapo Maana yake ni Owner's Risk

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: si Ndiyo umeliondoa hilo Jibu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Naiachia Mahakama Twende Eneo Lingine

Kibatala: Mwanzo Ulisema Ulikuwa unapanda Tax huna Gari

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Basi Ujue kwanini Nimekuuliza Kuhusu Gari

Kibatala: Shahidi Fungua Yohana Sura ya 8, Mstari wa 31 Mpaka 39

Shahidi anasoma biblia hapa..

Amemaliza..

Kibatala: Unafahamu Maan ya hilo Neno

Shahidi: Ndiyo Nafahamu

Kibatala: Maana yake ni nini

Shahidi: Tusiogope, Tuseme Kweli

Kibatala: Soma pia Waefeso Sura ya 4 Mstari Wa 25 Mpaka 32

Shahidi anasomeshwa Biblia tena

Kibatala: Je, unafahamu Maana ya hilo Neno

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Maana Yake ni nini

Shahidi: Tusiseme Uongo na tupendane

Kibatala: Kwa Hiyo Unafahamu Kwamba Maisha ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya yapo Mikononi Mwako

Shahidi: Ndiyo najua

Kibatala: na Ulisema Kwamba Mara Ya Kwanza Ulikutana na Mbowe Lini

Shahidi: JULY 2020

Kibatala: Tarehe Ngapi

Shahidi: Sikumbuki ni Tarehe za Kati kati

Kibatala: zipi hizo

Shahidi: Tarehe 10 Mpaka 15

Kibatala: Hizo ndiyo Tarehe za Katikati

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na wewe ni Luten wa Jeshi la Wananchi Tanzania tunalolipenda wote

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Elimu yako ni Form Four

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ulipata Divisheni Ngapi

Shahidi: Three ya Point 25

Kibatala: unajua Division Four Inaanza point ngapi

Shahidi: Point 28 ila Sikumbuki Vizuri

Kibatala: Kwa hiyo Unakumbuka au hukumbuki

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Umesoma wapi.?

Shahidi: King'ori Sekondari

Kibatala: Headmaster Wako ni nani

Shahidi: Simkumbuki

Kibatala: Graduation Mlifanya lini

Shahidi: Hatukufanya Graduation

Kibatala: Ukimaliza Form Four lini

Shahidi: Mwaka 1999

Kibatala: Yule Mchungaji Wako anayefundisha Mzumbe Mara ya Mwisho Kuwasiliana naye ni Lini

Shahidi: Sina Mchungaji

Kibatala: Na Nabii Tito anayefundisha Mzumbe Umeacha Kusali Kwake lini

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Habari Nzito ya Mbowe Ulimshirikisha Paroko au Mchungaji

Shahidi: Sikumshirikisha Mtu

Kibatala: lakini Ulishindwa kulala

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: lakini Ukaenda Kumshirikisha nani

Shahidi: DCI na Kingai

Kibatala: Mwingine Je?

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Msemo wa Kwamba Askari hawezi Kuwa Raia ila Raia anaweza Kuwa Askari Maana yake nini

Shahidi: Kwamba Ukishakuwa Askari huwezi kuwa Raia, Ila Raia anaweza Kwenda kujifunza Kuwa Askari

Kibatala: Jeshi la Wananchi Tanzania Mnafundishwa Kuwa Jeshi la Polisi ni Jeshi Kweli au si Kweli

Shahidi: Kweli

Kibatala: Raia Akiona Uhalifu unatendeka anaweza Kuzuia Uhalifu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwamba Mwajeshi Akiona Uhalifu Unatendeka anaweza Kuzuia au anaacha utokee alafu ana report Taarifa Polisi

Shahidi: Anazuia Uhalifu

Kibatala: ila wewe Ulikuwa na Mbowe anakwambia Mambo ya Kigaidi ukamuacha

Shahidi: Ndiyo Maana Nilienda Ku report Polisi

Kibatala: Kwani Jeshini si Kuna sehemu ya kwenda Kutoa Taarifa za Kihalifu

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Jeshi la Wananchi Tanzania Kuna Kitengo Kina shughulika na Ugaidi

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kuna Jeshi la Navy ambalo kazi yao Ni Kushughulika na Ugaidi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: na bado wewe ni Luteni wa Jeshi kabisa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwani kwa ufahamu wako wewe Jeshi halishirikiani na Jeshi la Polisi

Shahidi: Kama ikihitajika

Kibatala: Kwani Shahidi Kwa Mfano Mbowe angelipua Kituo cha Mafuta Puma pale Mwenge, Jeshi Pale Jirani Wangedhurika au Wasingedhurika

Shahidi: Wangedhurika

Kibatala: Bado Ukaona Usiwaambie Jeshi

Shahidi: (Kimya)

Kibatala: unasema Kwamba Mbowe alikwambia Kukata Miti wapi

Shahidi: Kukata Miti Kwenye Barabara zote zinazo ingia Mjini

Kibatala: pale Kambi ya Jeshi Lugalo Kuna Barabara ya Kuingia Mjini au Hakuna

Shahidi: Ipo

Kibatala: Kama Wangekata Miti pale Barabara ya Lugalo Jeshi lingedhurika au lisingedhurika

Shahidi: Lingedhurika

Kibatala: Lakini Bado wewe Ukaona Usiwaambie Jeshi

Shahidi: Nilipeleka Taarifa Polisi Kwa sababu wao Wana husika na Uchunguzi

Kibatala: Kati ya Wewe Ulipo pale Mgulani Kambini na Ofisi za DCI, Wapi Ilikuwa Rahisi Kwako Ku report?

Shahidi: Kambini Mgulani

Kibatala: Unafahamu Kitu kinaitwa Logic na Common sense

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: haya pale kwa DCI umesema Kwamba Kuna Scanner, Umejitambulisha Kuwa wewe ni Luteni na ukafanyeje

Shahidi: Nikatoa Kitambulisho

Kibatala: Baada ya Pale Ulimwambia Jaji Kwamba Jina lako liliingizwa Kwenye Register

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Unafahamu Kwamba sisi tumefika Kwa DCI Mara ngapi

Shahidi: Hapana, Sijui

Kibatala: Nikikukwambia Kwamba pale kwa DCI Nilifika Kumsindikiza Edward Lowassa Mwaka 2017

Shahidi: Ndiyo nitakubali

Kibatala: Unafahamu Kuwa DCI ni Mwanajeshi

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Ulimwambia Jaji Kwamba Kuna Mtu alipiga Simu Kwanza Kuhakiki appointment Yako

Shahidi: Hapana Sikumwambia

Kibatala: Unafahamu Kwamba Wanajeshi hasa DCI ambaye ndiye Kama WAZIRI Mkuu wa Jeshi la Polisi ni watu wa tahadhari kwa sababu ni Watu wana deal na Uhalifu Nchi Nzima?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je, Umemwambia Jaji Kwamba Kuna Kitambulisho Ulipewa cha Kuvaa

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kwa DCI Kuna Askari Kwa ajili ya Kimsindikiza Wanaenda Kwa DCI

Shahidi: Sikumwambia Jaji

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kuna Askari Wa Kukusindikiza Mpaka Kwa PS wa DCI

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Waiting Area ya Ofisi za DCI Makochi ni Rangi gani

Shahidi: Ya Brown

Kibatala: Unauhakika Kwamba Siyo Mekundu

Shahidi: (Kimya)

Kibatala: Ukifika kwenye Ofisi za DCI PS anakuwa Upande Upi

Shahidi: Upande huu, (anaonyesha Kushoto)

Kibatala: Umebadilsha Sasa hivi eeh?

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba niilipokuwa Ulipokuwa wait Area Kwa DCI iwapo Body Guard Wake Ukiwa Una subiri Kuingia

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Je Jana wakati wa Ushahidi Ulizungumzia Meza na Viti, Je Ulizungumzia DCI kuwa Ni Mnene, Mfupi, Mwembamba au Lah

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Je Ukaona ni Muhimu tufahamu Viti na Meza na siyo DCI ambaye Ulimfuata

Shahidi: DCI SI anajulikana

Kibatala: anajulikana na nani

Shahidi: Watanzania wote

Kibatala: Je Ulimwambia Jaji Kwamba Utaratibu gani Ulitumia Kutoka

Shahidi: Sijamwambia

Kibatala: Ulimwambia Jaji Kuwa Ulipokuwa Unatoka Ulisaini Out

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Unasema Ulifika Ofisi ya DCI Saa ngapi

Shahidi: Nimefika Majira ya Saa Mbili au Saa Tatu

Kibatala: Je Unafahamu Kwamba Huo Ndiyo Muda wa Kufika DCI

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Kwamba Chini ya Kiapo hapo Luteni Kwamba Siku hiyo DCI alipanda Ngazi Kwa Mguu Mpaka Ghorofa Ya Saba

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwa hiyo ufahamu Kwamba DCI alikuwa na Umri Miaka zaidi ya 50 na Sasa amestaafu Kwamba alipanda Ngazi

Shahidi: Sifahamu alifikaje Juu

Kibatala: kwa hiyo Wewe Unasema Kwamba DCI Kiongozi Wao Kama. Waziri Mkuu, Kuwa Lift yake Ilikuwa bovu

Shahidi: Hapana, Sifahamu

Kibatala: Jana Ulionyeshwa Simu zako, na Moja ilikuwa na Display ya Mke Wako

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Wakati Simu zako zote Nne Umepewa, Je Ni wakati gani Uliomba nafasi ya Kungalia Simu yako Namba ya Kingai Kama Kweli uliwasiliana naye?

Shahidi: Hapana Sikumwambia jaji

Kibatala: Je Kwa DCI pia ulimuomba Jaji nafasi ya Kungalia namba ya DCI Kwenye Simu yako?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Sasa Ni saa Saba Kamili, Kama Wenzetu wataridhia Twende Health Break na naomba Niependekeza Kwako Dakika 45

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi

Jaji: Kwa Maana hiyo tuta' break Kwa Muda wa Dakika 45 na Saa Saba na Dakika 45 tutarudi

Jaji amerejea

Kesi imetajwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wa Jamhuri tumetimia Kama Ilivyo kuwa Mwanzoni tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Quorum yetu ipo Kama Mwanzo, Wakili John Mallya amepata Udhuru atarejea Baada ya Dakika 10 badala yake naomba Wakili Michael Lugina awakilishe Ingawa ni wakili wa Mshtakiwa Wa Nne

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Naona italeta Shida, Kwa sababu Wakili Michael Lugina Tayari ameshaingia Kwenye Quorum, Mshtakiwa Wa Pili anahitaji Kupata Full representation..

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Maoni yangu Mimi, Mimi Ndiyo Nina Cross Exermine, Ila Ooohh Kwa Bahati Nzuri ndiyo anaingia... Huyu hapo.. Ikupendeze Kurekodi kuwa Sote Tupo na tupo tayari Kuendelea

Jaji anaandika Kidogo, Mahakama ipo Kimya wakati huu

Jaji: Shahidi nakukumbusha kuwa Ulikuwa Chini ya Kiapo wakati Unatoa Ushahidi Na Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo Wakati Unatoa Ushahidi

Jaji: Shahidi nakukumbusha kuwa Ulikuwa Chini ya Kiapo wakati Unatoa Ushahidi Na Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo Wakati Unatoa Ushahidi Wakili

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kwa Hisani ya Mwisho Nikumbushwe Swali lake

Jaji: Kama Iwapo Alikuwa na Simu zake na Kama Aliomba Mahakama atoe humo namba za DCI Akasema Hapana

Kibatala: Unafahamu Kwamba Utambulisho Wa su Moja dhidi ya Nyingine ni IMEI, Je unafahamu

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Wakati Unaongozwa na Mawakili Wenzetu wa Somi waliluomhoza Kutoa Nyaraka fulani hivi

Shahidi: Ndiyo Nakumbuka

Kibatala: Kwahiyo Nyaraka Ile Ilikuwa ni Kuthibitisha Kuwa palikuwa na Makabidhiano kati yako wewe na Inspector Swila

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Inaitwa Techno nini Vile

Shahidi: Tecno CAMMO

Kibatala: Niambie Kama wakati Unaonyeshwa Simu zako zote Nne, Je ulitambua Simu Moja Moja Kwa kutumia IMEI namba Shahidi Hapana, Nilitambua Moja tu

Kibatala: Kwahiyo Kama tuna Simu Nne, Tatu hukuzitambua kwa IMEI namba ya Simu Moja Moja

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: kwa hiyo hii Tecno CAMMO ulitambua Kwa IMEI namba

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwa Ushahidi Wako wote hapa umesema Kwamba Unaishi Ngerengere, Je Kuna sehemu Umesema Kwamba unaishi kihonda

Shahidi: Nina Makazi Mawili Ngerengere na Kihonda

Kibatala: Je Ulisema Jana na Leo Kabla Sijakuuliza

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Je Kuna Mahala Popote Ulitambua Maneno CAMMO Kama Yapo

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Kuna Maneno gani badala yake

Shahidi: Tecno tu

Kibatala: Je, Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali Abdallah Chavula Ulimfafanulia Mheshimiwa Jaji Kwamba hiyo Tecno ndiyo Tecno CAMMO

Shahidi: Sikufafanua

Kibatala: Wakati Wa Ushahidi Wako Wote Unaongozwa na Wakili Wa Serikali Abdallah Chavula, Uliongozwa kutoa Betri na Kusoma IMEI namba na Kumwambia Mheshimiwa Jaji Kama IMEI zinafafana na Inspector Swila Wakati wa Makabidhiano?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Soma Hapa Pameandikwa Kwamba wewe Luteni Urio unaishi Wapi

Shahidi: Kihonda

Kibatala: Je, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kwenye Kielelezo Kuwa wewe Luteni Urio Unaishi Kihonda Shahidi anatikisa kichwa hapa, namna gani..

Kibatala: Mahakamani, Usijibu kwa Kichwa

Shahidi: Sikumwambia Mheshimiwa Jaji

Kibatala: Soma Hapa

Shahidi: CD/IR/2097/2020

Kibatala: Ni nini hiyo

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je Ulifafanua ni nini hicho

Shahidi: Sikufafanua

Kibatala: Kuna IMEI namba Ngapi hapo

Shahidi ameshika Kielelezo cha karatasi moja

Shahidi: Sijui ni IMEI namba ngapi

Kibatala: Unafahamu Inspector Swila alikozitoa hizi IMEI namba au hufahamu

Shahidi: Kwenye Simu yangu

Kibatala: Je, Zipo ngapi hizo IMEI namba zipo ngapi

Shahidi: Sifahamu
four four luteni?
 
sasa maswali kama haya yamesaidia nini mbowe? kama eye witness na mtu aliyekuwa anawasiliana naye na kukutana naye anasema mpango wa ugaidi ulikwepo, hata kama kamati ya ulinzi na usalama au yeyote hata kuwa na taarifa inahusu nini? ndio wanasheria wenu hao. hapo laymen huko mtaani wanashangilia ati ameuliza maswali magumu.
Ndugu mahakama haifanyi kazi bila ushahidi..maneno ya Urio kuwa Mbowe alimwambia mpango wa ugaidi bila ushahidi maneno matupu tu hayasaidii hasa kama hakukuwa na mtu mwingine zaidi ya wao wawili tu..maana Mbowe anaweza kuja nae akasema hakuwahi kumuambia Urio huo mpango....hapa inaonesha wewe ndio layman unaoshangilia ushahidi usiokuwa na mashiko wa Urio
 
Ushahidi wa Lt Urio ni ushahidi wa kijinga jinga zaidi na anaendelea kulidhalilisha jwtz
 
Shahidi wa 12 Luteni Urio, kwa kifupi analiaibisha JWTZ.​

Kwani wakuu, jamuhuri ina mashahidi wangapi na huyu boya ni shahidi wa ngapi??
Nasikia wapo kama 24 ila huyu boya ni shahidi wa 12 na ndio alikuwa makao makuu ya mashahidi wote hao wengine ni matawi tu,na yeye ndio alijinasibu kupewa kazi nzito na Mwamba ya kutafuta 'magaidi' na kwamba amefanya vikao vya faragha kupanga mikakati ya kutwaa nchi.

Matokeo yake kaishia kunywa Malta na kutuletea porojo za 'muda umekwisha mara sijui mtu tatu' na kuwachomekea kesi nzito vijana wasio na hatia waliokuwa wanajitafutia kwa ajili ya familia zao.
 
lazima watanzania wote kwa pamoja tuungane kupinga na kuondoa viashiria vyote vinavyo weza kuharibu Amani ya Nchi.

Vitendo vya kigaidi vya ndani ni chanzo kikubwa cha kuhatarisha usalama na utulivu wa nchi.

Hivyo ni lazima viashiria vyote vitokomezwe bila ajizi.
Viashiria vipi? Amani ipi imevunjwa? Kuwabambikia kesi kuwatesa kuwapiga watu wakubali ugaidi hewa ndiyo uvunjifu wa Aman i
 
Lt. Denis Leo Urio kasababisha watu wajifikirie upya kuhusu uLuteni, uKomandoo na JWTZ kwa ujumla...
Sasa itabidi Comandoo wote wafanyiwe semina kubwa ikibidi hata na makomandoo wa kimataifa ili kuondokana na Aibu hii ya kulidhalilisha jwtz kwa kushiriki kesi za Mchongo na hap Polisiccm
 
Huyu shahidi anadai Mbowe ndio anajua idadi ya vituo vya mafuta ambavyo anataka kulipua Halafu yeye haoneshi kwenye mawasiliano yao kama hayo walikuwa wanayapanga. Sasa tumuamini Nani. Yeye anadai Mbowe alitaka kufanya ugaidi lakini tangu wakutane hakuna sehemu wamejadilaina ugaidi na hata wale makomndoo tangu wanaletwa kwa Mbowe hawakuwa wanajua kwamba wanafanya ugaidi. Swali ni huu ugaidi ulianzia wapi?
Hakuna ugaidi wowote bali aliyetengeneza ugaidi hewa ni DC Sabaya na kingai kwa Lengo la kumfurahisha marehemu Magufuli
 
Shahidi wa Jamhuri Luteni Urio ana simu ambayo haiwaki tangu Jana na amedai haidisplay. Ilikuwaje wakashindwa kutengeneza. Maana inaonekana upande wa utetezi wanahitaji zaidi simu hiyo, inaonekana kuna ushahidi mkubwa unafichwa kwenye simu hiyo.
Aaache uongo asituletee yale ya nimesahau password ya bandarini mtu alibanwa mbavu na jpm afungue computer akasema nimesahau password.
 
Kesi ya makomandoo iliisha jana baada ushahidi wa Urio, kesi ya Mbowe imebaki sehemu ndogo sana, Mbowe kusema tu hakumwambia shahidi Urio, then kesi yote itakua imeisha mana Urio keshasema Hana uthibitisho wowote na hawakuwai kujadili tena kuhusu ugaidi.
isitoshe huyo Lt Urio aliteswa na kupigwa sana ili akubali ugaidi hewa inashangaza Leo kawa upande wa kingai na mahita watesi waonevu
 
Waswaap call recording zake wataupata ushahidi wote.
Naona wahuni wanaenda umbuka
 
Back
Top Bottom