Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Kwa ushahidi wa leo dhahiri hii kesi haina tija kwa taifa bali ni muendelezo wa chama kutumia dola kusalia madarakani kama alivyosema Bashiru.
 
Huyu jamaa Urio nae inabidi achukuliwe hatua kali baada ya hii kesi kwisha,Huko kuwasiliana na kiongozi wa kisiasa ni kosa kubwa jeshini,huyu akina kagame waihitaji siri za nchi jamaa anaweza akatuuza akihaidiwa donge nono
 
Na biblia mkononi kaapa kiapo
 
Upepo wa kesi mbona kama unaonesha hapa source ya yote ni urio. Urio anafahamiana na mbowe, alikutana na mbowe akiwa na p.o.p baada ya kuvunjwa mguu na wahuni akasema 'kaka unaonewa sana'.

Huyu urio alitumwa kwa mbowe kwa mission maalumu sema ilibuma tu. Tuhuma zinarudi kwake yeye ndio gaidi
 
Je, unajua ingridients za makosa ya ugaidi???
Je, mtu anaweza kutenda makosa ya kula njama za ugaidi bila kuwa na washirika wengine???
Je, unajua iliishia wapi ile kesi ya ugaidi wa mchongo waliompa Rwakatare ??
Kuna course wanasheria hua wanaisoma inaitwa Evidence Law. Huko utakutana na kitu kinaitwa "accomplince" in the comission of a crime. Kama unapenda udadisi soma uyakua umepata jibu la hoja yako
 
Mkuu acha porojo,Sasa Mbowe si anashitakiwa Kwa kula njama!Sasa hizo njama kafanya na nani?It's either yeye na waliokula nao njama ni guilty or innocent Kwa Pamoja!Sema kama ni guilty,sentence zao zinaweza kuwa tofauti!
Hii kesi ni big failure!Nilishangaa inakuwaje nchi kama USA zinatuma balozi kumfariji Mbowe wakati wao ndio wahanga wakubwa wa ugaidi na ndio walioleta hadi sheria za ugaidi Kwa hizi third world countries!
Kadri ushahidi unavyoendelea kutolewa ndio unaona hata wao waliona hii kesi ni ubabaishaji tu!
 
Kwa nilivyofatilia siku ya jana, nilisikia akisema kwamba wale askari wote walijua wanaenda kufanya kazi ya ulinzi tena akawatahadharisha ya kwamba kama kuna kitu watakiona huko sio cha kawaida au tofauti na majukumu ya kazi yao ya ulinzi basi haraka watoe taarifa kwake. Nadhani hadi pale Morogoro wale makomandoo hawakua wakijua lolote kuhusiana na kazi ya ugaidi
 
Kulikuwa hakuna kazi ya ugaidi uncle... Siyo kwamba hawakujua, haikuwepoo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…