Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Sababu nipo Chini ya Kiapo Cha Mwajiri Wangu, Mafunzo ya Kijeshi itakuwa ni Shida Kwangu, Naomba Mwajiri Wangu, Nisije kutoka hapa Nikapelekwa Court Marshall

KAZI IPO

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Kesi ya kijinga sana na imechongwa na wajinga ili kulinda heshima ya chief Hangai aliepotoshwa.

Badala ya kushughulikia waliomdanganya Rais mnashughulikia watu wasio na hatia,mnatuletea mikosi tu ktk taifa kwa uonevu wa raia

Ndio maana mvua hainyeshi
 
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Sababu nipo Chini ya Kiapo Cha Mwajiri Wangu, Mafunzo ya Kijeshi itakuwa ni Shida Kwangu, Naomba Mwajiri Wangu, Nisije kutoka hapa Nikapelekwa Court Marshal...
kalainika ameanza kujieleza
 
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Sababu nipo Chini ya Kiapo Cha Mwajiri Wangu, Mafunzo ya Kijeshi itakuwa ni Shida Kwangu, Naomba Mwajiri Wangu, Nisije kutoka hapa Nikapelekwa Court Marshall
ha ha ha, sasa umekuja kutoa ushahidi upi - Mawakili wa utetezi watoe hoja ya kuukataa utetezi wa huyu jamaa. URIO unataka kumfunga mwenzako miaka 30 au maisha then unagoma kutoa ushahidi ? kweli ?
 
Ninachoona hapa shahidi anaogopa swali la kesho kutwa na kusema yeye kuwa yupo chini ya kiapo kujibu level ya mafunzo yake ni uwongo mkubwa. Court Marshal gani anayoisingizia yeye?

Ajibu swali ili mambo mengine ya endelee, na jaji pia kama kuna mchezo anaujua na anaufumbia macho. Kama hivyo shahidi hata uliswa maswali kwa kigezo cha kiapo cha jeshi. Kwani yy hadi kufika hapo kavunja viapo vingapi?
 
Nashon: Unafahamu a kwamba Baada ya Kesi hii Unaweza Kutoka Kama shujaa au Mtu asiye na Thamani Duniani

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Unafahamu Msemo unaosema Kuwa ni Heri Kufa Jasiri Kuliko Kuishi Katika Utumwa, Unafahamu Kwamba Kesi hii Inafuatiliwa Nchini na Duniani Kote

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Unafahamu Kwamba Ukieleza Ukweli yaliyo Nyima ya Pazia, Hata Jeshi Litakulinda

Shahidi: Hata sasa Nipo Pamoja na Jeshi

Nashon: Baada ya Kueleza hayo, Naamini Umetafakari Vizuri

Nashon: tuanze hapo Unaposema Jeshi lipo na wewe, Kivipi

Shahidi: Wanafahamu Kuwa nimekuja Kutoa Ushahidi

Nashon: Nikisema Kwamba Hujatoka kazini Kwako Utakataa

Shahidi: Ndiyo Nimetoka Kazini Kwangu

Nashon: Je Unaruhusa au Movement Order

Shahidi: Ndiyo ninayo
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Sababu nipo Chini ya Kiapo Cha Mwajiri Wangu, Mafunzo ya Kijeshi itakuwa ni Shida Kwangu, Naomba Mwajiri Wangu, Nisije kutoka hapa Nikapelekwa Court Marshall.
😛🤣😂

Kwani shahidi hakujua mgongano wa maslahi
 
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Sababu nipo Chini ya Kiapo Cha Mwajiri Wangu, Mafunzo ya Kijeshi itakuwa ni Shida Kwangu, Naomba Mwajiri Wangu, Nisije kutoka hapa Nikapelekwa Court Marshal...
pevu...... Jamaa kagoma - sasa wacha tuone MAHAKAMA KUU vs LUTENI WA JESHI anayeogopa kibarua chake kisiote nyasi ila ANATAKA mshitakiwa afungwe miaka 30 au Maisha ILA ushahidi wake usihojiwe, uchukuliwe kama ulivyo.
 
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Sababu nipo Chini ya Kiapo Cha Mwajiri Wangu, Mafunzo ya Kijeshi itakuwa ni Shida Kwangu, Naomba Mwajiri Wangu, Nisije kutoka hapa Nikapelekwa Court Marshall

KAZI IPO

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Jaji anachezewa. Hiyo ni CONTEMPT OF COURT ...... Amuweke ndani mpaka J3. Akitoka huko atajibu maswali yote bila kujali hicho kiapo chake
 
Jaji anachezewa. Hiyo ni CONTEMPT OF COURT ...... Amuweke ndani mpaka J3. Akitoka huko atajibu maswali yote bila kujali hicho kiapo chake
SHAHIDI hajui kwa nini aliapishwa kabla ya kuanza kutoa ushahidi wake - maana yake viapo vingine vinafutika kwa muda na kinachosimama wakati huo ni KIAPO cha Mahakama KUU.

Yawezekana kabisa kwamba huyu jamaa kalazimishwa kuja kutoa ushahidi - maisha yake ni magumu mno muda.
 
Mkuu, umefuatilia kesi hii toka jana? Wakili wa serikali alimuuliza, kwa cheo chake Urio, anaongoza askari wangapi, alijibu 30. Pia, koplo anaongoza 9.Haya maswali ya wakili wa utetezi, yana tofauti gani na hayo aliyoulizwa jana?
Kwa hiyo platoon inakuwa na askari 30? Huyu mwanajeshi wa wawapi,mpakani au fire? Kama section 1 inakuwa na askari 9 na kila platoon inakuwa na section 3 hiyo idadi ya askari 30 ametoa wapi?

Kama nyota 2 hajui vipi kwa staff sajent wake atakuwa anajua nn? Huyu hajatoka kikosini tokea akamatwe na madoso aliyokula ndio hizo zimemwongezea mtero(hofu)mahakamani
 
ha ha ha, sasa umekuja kutoa ushahidi upi - Mawakili wa utetezi watoe hoja ya kuukataa utetezi wa huyu jamaa. URIO unataka kumfunga mwenzako miaka 30 au maisha then unagoma kutoa ushahidi ? kweli ?
Jamaa anadai alikuwa kwenye operation Sudan lakini hakumbuki mu yeyote waliyekuwa naye huko .... Seriously?

Kama jamaa ana matatizo ya kumbukumbu kihivyo inakuwaje tumuamini kwenye ushahidi wake ....!!?
 
Back
Top Bottom