Hajto
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 5,646
- 5,606
Kwa sheria za kijeshi nijuavyo mimi,ukiwa mazingira ya kambini hutakiwi kutoka na ikitokea kutoka kuna kitabu unaandika mahala unapoendana ukirudi ni ivyoivyo,kosa lake Urio alitakiwa palepale mwanzo alivyopigiwa simu na mbowe angeijulisha mamlaka yake kama mkuu wa kikosa ama kiongozi mkuu wa zamu wa siku iyo,usiri wake hata uko kumtafutia mbowe walinzi ni kosa kubwa sana kwake.Luteni ni Nani Jeshini? Nini Kilimfanya Urio Aende Moja kwa Moja Kwa DCI na Si Mwingine yeyote? Nini kilimfanya Afikirie kwamba Mtu wa Kwanza ni DCI
Nakumbuka kuna siku nipo mwenge stand ikapita pikipiki kwa kasi ikamgonga mjeda mkono kwa mbali damu zikawa zinamtoka,mjeda yule ikabidi amuite trafiki,akampa maelezo aende kituoni kisha apewe p3 ya kutibiwa ila alitoa sababu kutibiwa kwake yule mjeda lazima aende kambini kwake kutibiwa,akasema sheria zao mjeda akitaka kutibiwa kuwe na sababu iliyomfanya kutibiwa pale,so akatoka nae pale bodaboda mpaka kituoni,kisha akatoka nae tena hapo kituoni hadi kambini kwae kutibiwa...mpaka hapo ndio nikajua sheria za jeshi ni ngumu sana