Habari Wakuu,
Leo
14/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3. Mawakili wa Serikali waliomba ahirisho la kesi hadi leo Februari 14, 2022 kutokana na Shahidi Tumaini Swila kushindwa kufika Mahakamani siku ya Februari 10, 2022 kutokana na ugonjwa. Awali Februari 9,2022 aliomba ahirisho kwakuwa alikuwa hajisikii vizuri.
Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake 3: Shahidi wa 13, Tumaini Swila ashindwa kufika mahakamani. Kesi imeahirishwa hadi Februari 14, 2022
Baki nami.
Updates:
Jaji ameingia Mahakamani Muda huu Saa 4 Kamili Asubuhi
Kesi Namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu.
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili
- Pius Hilla
- Abdallah Chavula
- Jenitreza Kitali
- Nassoro Katuga
- Esther Martin
- Ignasi Mwinuka Mawakili Wa Serikali Waandamizi na
- Wakili Tulimanywa Majige
Wakili Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili
- John Malya
- Faraji Mangula
- Nashon Nkungu
- Fredrick Kihwelo
- Livino Haule
- Edward Heche
- Sisty Aloyce
- Seleman Matauka
Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo shahidi namba 13 ameweza Kufika Kwa ajili ya Kuendelea Kutoa Ushahidi Wake ambapo Upande Wa Utetezi Walikuwa wanahoji Maswali ya Dodoso. Tupo tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi pia tupo tayari Kuendelea
Inspector Tumaini Sosthenes Swila anapanda Kizimbani na Kaunda Suti ya Kijivu kisha anasimama..
Jaji: Shahidi nakukumbusha kuwa kabla Shauri halijahairishwa ulikuwa Chini ya Kiapo na leo Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nakumbuka Nilipo Ishia naomba Nipewe Kielelezo Namba P4, P5 (Risasi na Maganda Yaliyo tumika)
Kibatala: Shahidi Unakumbuka Mara ya Mwisho Zoezi lilisimama Kwa sababu Ulisema unataka Kupata huduma za Afya
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Na kweli ulitoa Kauli hiyo Ukiwa kwenye Kiapo
Shahidi: Ni kweli
Kibatala: Una Daktari Wako au Una Daktari Wako Mahususi
Shahidi: Kimya
Shahidi: Nahudumiwa na Madaktari tofauti
Kibatala: Unahudumiwa kwa Muda gani
Shahidi: Zaidi ya Miaka Miwili
Kibatala: Wanaitwa nani
Shahidi: Namkumbuka Mmoja anaitwa Mohammed
Kibatala: Mohammed nani
Shahidi: Simkumbuki
Kibatala: na Amekuhudumia kwa Muda gani huyo usiyemkumbuka
Shahidi: Miaka 2
Kibatala: Je unafahamu Niliandika Barua katika Hospitali ambayo Ulisema Kwamba wanakuhudumia
Shahidi: Sijapewa
Kibatala: Kwa hiyo ujui Kwamba Hospitali imesema ipo tayari Kusema wapo tayari Kuja Kutoa Ushahidi
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Ni hali ya Kawaida kutomfahamu Mtu anayekuhudumia Miaka 2
Shahidi: kawaida
Kibatala: ulilazwa au ulipumzika nyumbani
Shahidi: Nilikuwa nimepumzika Nyumbani
Kibatala: Nyumbani kulikuwa na Daktari anayekuhudumia
Shahidi: Hapana
Kibatala: Tukoke hapo Nitarudi baadae