Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake. Shahidi Justine Eliya Kaaya, amtaja Ole Sabaya. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 28, 2021

naamini lengo la fingerprint ni kuthibitisha kama bastola imeshawahi kushikwa na mmiliki aliyekutwa nayo....kama hana kibali kinachoonyesha ni mali yake anaweza kuikana sio yake bali alichomekewa.....Finger print inaweza kuthibitisha ameshawahi kuishika mara ngapi......HAPO SHAHIDI KATOKOTA kwa mtazamo wangu...
 
AMEN,AMEN
 
Huyu nasikia wamemficha sehemu na amepata vitisho vingi na amejazwa mamilioni ili aje atoe ushahidi wa kumkandamiza Mbowe.
huyo jamaa ni marehemu walishamwua kwa mateso wakati wa kuwabambikiza
 
Mwenzenu hapa naona hii kesi sielewi!Hii kesi naona kama imesukwa kitaalamu haswaa! Nina mashaka na hao washitakiwa watatu wa Ugaidi waliounganishwa na Mbowe!
Anyway waliosomea sheria mtatusaidia.
 
Sasa kama Jaji anamuomba shahidi msamaha kwa niaba ya utetezi kwamba aisamehe mahakama kwa maswali konki ya koromeo yaliyomtoa jasho la ulimi kingai unategemea kuna nini hapo zaidi ya malekezo
Sheria/Mahakama siyo sehemu ya kuoneshana umwamba wa kuuliza maswali ambayo yatafurahisha mashabiki wa kisiasa mitandoni...
 
kuna vitu huwa nawaza yaani mtu afukuzwe jeshini tu sababu ya battle kifusion, wakati jeshini kuna kazi nyingi za kufanya sio lazima kwenda vitani, hapa labda kuna kosa la kuhasi jeshi ambalo ndio kosa kuu , naamini huwezi kufukuzwa kwa sababu eti mizinga ikipigwa unapagawa maana jeshini unaweza jifunza hata kutengeneza magari wakakuweka ukawa fundi gereji ila sio kukusaliti kwa kukufukuza kwa sababu ambazo sio za msingi yaan ni sawa sawa mwanajeshi mwenye VVU eti afukuzwe kisa tu kaugua VVU, huyo haendi vitani lakini jeshini anabaki kama kawaida sasa iwe komandoo apa kunamashka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…