Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake. Shahidi Justine Eliya Kaaya, amtaja Ole Sabaya. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 28, 2021

Hii kesi inapaswa kufutwa haraka, imeshakosa mashiko!

Msingi mkuu wa hii kesi iliyokuzwa na kubatizwa jina la ugaidi ni kinaitwa njama za kutaka kumdhuru Jambazi na mnyang'anyi wa kutumia silaha Ole Sabaya!

Kwakuwa mahakama imeshajiridhisha kuwa Ole Sabaya ni Jambazi na mnyang'anyi wa kutumia silaha, na kila siku tunasikia kwenye vyombo vya habari kuwa majambazi wameuawa na polis tena kwa kuhisiwa tu kuwa ni majambazi, Hivyo Sabaya pia yumo kwenye kundi moja na hawa majambazi waliostahili kupigwa risasi, hivyo hata kama ni kweli kulikuwa na njama za kutaka kumdhuru, basi zinapaswa kuitwa njama za kutaka kumdhuru jambazi na sio kiongozi kama umma unavyotaka kuaminishwa!

Mahakama imeshadhibitisha pasipo shaka kuwa huyu hakuwa kionbgozi bali Jambazi na mnyang'anyi wa kutumia silaha hii ndio sababu UDC wake umeshindwa kutumika kumuokoa na hukumu hata baada ya kumtaja mkuu wa nchi kuwa ndiye aliyekuwa akimtuma kufanya ule ujambazi na unyang'anyi bado sheria ilimtia hatiani!

Hivyo hoja ya kusema Mbowe alitaka kumdhuru kiongozi haina uhalali wowote kwakuwa hata sheria imeshamuona Sabaya hakuwa kiongozi ali jambazi na mnyang'anyi tena aliyestahili kabisa kupigwa risasi kama majambazi wengine!
 
Nashindwa kuelewa mantiki ya kesi hii. Maana Agosti 2020 Mbowe anawaajiri hao komando kuandaa fujo, kuchoma vituo vya mafuta, kukata miti kwenye barabara Moro/Iringa na kumshambulia DC wa Hai?

Halafu mwaka 1 baadaye, wakati hakuna kituo 1 kilichochomwa, hakuna mti ulioanguka kwenye barabara hiyo, na Ole Sabaya alifurahia maisha hadi kupora wafanyabiashara wa Arusha, hao magaida wanakamatwa?

Na katikati hakuna hatua iliyochukuliwa kulinda usalama? Wala hakuna kitendo cha kigaidi kilichotekelezwa?
Abu Nuwasi au mwendesha mashitaka mkuu?

(Hasa kwa sababu mashitaka ya ugaidi yalitumiwa tayari Oktoba 2020, nisipokosei; ni yaleyale ya kuchoma vituo vya mafuta..... sivyo?)
 
Kwamba nikipata namba yako ya simu na ya jirani yako,eti tunataka kufanya Ugaidi
 
Asante..Mbowe alikuwa anapambana na jambazi!
 
hii kesi msingi wake eti ni kusudio la kutenda kosa, kwamba waletea mashitaka wanamshitaki Mbowe kwa kusudio la kufanya ugaidi.. sasa sijui sheria inasemeje hapo maana so far hakuna ugaidi wowote ulifanyika na mbaya zaidi hakuna vielelezo vya kuifanya mahakama iamni kwamba ugaidi ulipangwa, hakuna hata kimoja.
 
Toa mfano basi busara ipi itumike? Maana watu wameongea sana hata kipindi wakiwa bungeni lakini hakuna lolote, au kufanya kongomano sio busara?

Watu mnajifanya wajuaji sana kwenye hamna.
 
Hata jambazi bado anazo haki.......
 
usipokuwa na Tiket ina maana hukusafiri, na hata kama ungepata ajali hakuna bima ama chochote kwa haki yako ungepata - kifupi hukusafiri, mahakama haifanyi kazi kwa ku-assume, lete tiketi we shahidi acha longo longo.
 
Una akili ya kisoda sana, unafikiri huyo Shahidi hawezi kupangwa kusema hayo, kwanini alikaa ndani mwaka mzima na baadae kuachiwa?

Acha kuamini kila kisemwacho.
 
Au uongo jamani
Jenister na Amos Makalla chori chori uchi
Mafisi kibao: Kuhusu mke wa balozi wa china: Msema kweri mpenzi wa mungu!!
 
Nimeanza kuelewa kwanini Serikali kama za CCM zikipoteza madaraka wanaishia kupigwa marufuku kufanya siasa tena na viongozi wake na wananchama kufungwa au kuburuzwa mitaani, imetokea dunia nzima
 
Hairuhusiwi mahakama kuomba print out kutoka makampuni ya simu inayoonyesha calls za shahidi na Mbowe?..... naona wakili kauliza tiketi na shahidi hana, mahakama haiwezi kuthibitisha kwa kuangalia movement ya simu ya mhusika hiyo siku..vs mazungumzo yake anayotoa mahakamani... Kama ni uongo mahakama haiwezi kumpiga mvua shahidi kwa kuleta uongo mahakamani.?....

hakuna nilipoona makubaliano ya malipo kati ya huyo shahidi na Mbowe...unawezaje kuombwa tu important information za watu na kutoa kirahisi hivyoo bila makubaliano? ( anyway labda ndio watanzania tulivyo..)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…