Sasa ni wazi hii nchi haitakaa ipate maendeleo. Kila cku vikao - ni vikao vya kuzindua mara michezo mara makongamano, mara usalama barabarani, mara cjui nini - ili mradi rais yuko busy ktk misafara ya uzinduzi, kila siku.
Imekuwa mahali muafaka pa kujipatia mi-posho kwa wajanja (washauri). Wakati haya yakiendelea, viongozi kila mahali wanahama ofisi, wamehudhùria misafara - na sio kwenye wilaya husika tu, hata za jirani na mikoa jirani, hata madaktari hawako salama. Piga hesabu za gharama uone kodi zetu zinapoishia!
Njoo kwenye teuzi! Kila kiongozi kuteuliwa na rais, kuanzia wilayani hadi taifa, wako wabunge wa rais, mahakimu wa rais, Mkuu wa Majeshi, wa Mapolisi, Jaji Mkuu, wa Usalama, Takukuru na viongozi mbalimbali na mateuzi haya huambatana na posho zao. Sasa, ikiwa wote wanateuliwa na rais, nani wa kumkemea nani! Yaani tukubali tu kuwa sasa, umebaki mhimili mmoja wenye nguvu na hauko kikatiba - chama dola.
Hebu fikiria, ili uwe rais, lazima upitishwe na chama chako. Kwa CCM, ukishapitishwa mgombea na ukishinda, unakuwa Mkt wa chama na kwa wadhifa huo una uwezo wa kutumia chama kumtimua yeyote uanachama - iwe Spika au Jaji Mkuu au yeyote yule. Ikishafika hapo, kama ilivo sasa, the president is Supreme. Viongozi wote wanatakiwa kuufyata mbele ya rais.
Kwa mfumo huo, kipi kitafanyika kwa ufanisi, labda kuimba mapambio hasa ule wa "Rais Wetu ni Mteule wa Mungu" na ule wa "Mamlaka zote zimetoka kwa Mungu" ambazo kwa sasa zinaimbwa kotekote hata kwenye vilio, ili tu kumfurahisha mkulu.
Kila baada ya uchaguzi, mchakato wa kushinda uchaguzi unaofuata huanza na fedha toshelezi kwa ajili hiyo husakanywa kila mahali, hata zile zinazoitwa za maendeleo zinakuwa halali yao - sasa kwa staili hiyo, lini tutapata maendeleo?!
Piga ua, tatizo kuu ni katiba. Kwa hii isiosomeka kutokana na viraka, rais atafanya lolote kama apendavyo na tukiendelea hivyo tutaendelea na utamaduni wa kuimba mapambio kama majuha fulani ambao kwao ni Tz na maendeleo tutayasoma kwenye magazeti - hususan "Uhuru" au kuyasikia toka midomo ile ambayo tumekuwa tukiisikia ya wanasiasa wetu kila wakati - na tutegemee tena hayo ktk shereha ijayo, kuyasikia na sio kuyaona...nk
MIAKA 60 YA UHURU NA ITUFUNGUE TUONE MAENDELEO MUAFAKA - UMUHIMU WA KATIBA MPYA, period.