Yaliyojiri mechi ya Mgambo JKT Vs Simba at Mkwakwani

Yaliyojiri mechi ya Mgambo JKT Vs Simba at Mkwakwani

Leo ndio Leo pale Mkwakwani Mambo atakapomkaribisha Mnyama aliye kwenye form ya hatari sana pale Mkwakwani.

Simba itaingia katika mchezo wa leo ikiwa na morali ya hali ya juu baada ya kushinda mechi 3 mfululizo zilizopita chini ya staa hatari zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, Emmanuel Okwi aka Super Okwi.

Ikumbukwe Mgambo hajawahi kupoteza mechi dhidi ya Simba anapokuwa Mkwakwani. Hivyo mechi ya leo itakuwa ngumu.

Mechi ni saa kumi jioni.

Kikosi cha Simba
1.Mapunda
2.Kessy Ramadhani
3.Tshabalala
4.Isihaka
5.Moshid
6.Abdi Banda
7.Ramadhani Singano
8.Jonas Mkude
9.Ibrahim Ajibu
10.Said Ndemla
11.Okwi

Mnyama aliye kwenye form ya hatari! MKWAKWANI Ha Ha Ha Ha
 
Mpira si uishe tu..matokea hayo yanatosha jamani...sisi mikia tupo radhi
 
Niliwaambia Mikia furaha yao si ya kudumu, huwa ni ya muda tu.
 
Niliwaambia Mikia furaha yao si ya kudumu, huwa ni ya muda tu.

Tatizo lao mashabiki wa mikia akili zao zipo kwenye sifuri saba moja tatu, ukiwaambia hayo maneno na rahisi kwao kusahau
 
uwanja wa mkwakwani ni mbovu sana...TFF hebu angalieni hii
 
Back
Top Bottom