Yaliyojiri msiba wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif

Yaliyojiri msiba wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Leo ni mazishi ya makamu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad na mwili umeshawasili msikiti wa Maamur kutoka Lugalo. Watu kadhaa wamefika ikiwemo kiongozi wa ACT, Zitto Kabwe, mufti wa Tanzania na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

========

Zitto Kabwe: Assalam Aleykum, kwa niaba ya chama napenda kuwashukuru nyote kabisa katika kuungana nasi kwenye ibada hii ambayo tutafanya Dar es Salaam kwa nyinyi ambao mmeweza kufika, tunashukuru sana. Tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa kumpa uhai kamilifu Maalim Seif Shariff Hamad, kwa hakika ameyaishi maisha yake kwa ukamilifu na sote kwa pamoja tuendelee kumuombea Dua na wale wanaoweza waendelee kumtolea sadaka, nawashukuruni sana.

MJUMBE: Nimetumwa kwa niaba ya familia, serikali na chama, kama kuna mtu yeyote anaemdai au kudaiwa Maalim Seif Shariff Hamad, deni hilo tunaomba sasa lihame Rasmi, litahamia kwa familia.

Lakini inawezekana mmekosana katika mambo yenu ya kisiasa, natumia nafasi hii kumuombea radhi, kama kuna yeyote aliemkosea au kukosana na Maalim Seif namuombea msamaha.

Mwili unatolewa msikiti wa Maamur kuelekea uwanja wa ndege kisha Unguja, Zanzibar.


MATUKIO YA KUWASILI MWILI WA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD UWANJA WA NDEGE WA ZANZIBAR​



02625-dsc0047.jpg


e888a-dsc0064.jpg

Mwili wa Marehemu aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ukishushwa katika Helikota ya JWTZ baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar ukitokea Jijini Dar es Salaam.






Rais wa Zanzibar a na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Aliu Mwinyi na (kushoto)Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleimn Andulla na (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magjaribi Unguja Mhe.Idreisa Kitwana Mustafa na Viongozi wengi wa Serikali na Chama wakiupokea Mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ulipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amari Karume Jijini Zanzibar, kwa ajili ya kuangwa na Wananchi wa Zanzibar katika viwanja vya Mnazi mmoja na kusafirika kwenda Pemba kwa maziko leo jioni.
52078-dsc0184.jpg








Wananchi wa Zanzibar wakiwa katika viwanja vya Mnazi mmoja wakisubiri kusalia mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,katika viwanja hivyo kabla ya kusafirishwa kwenda Pemba kwa maziko.

F87A0105-2.jpg


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijumuika pamoja na Wananchi wa Zanzibar katika Sala Maalum ya Kusalia Mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad iliyosaliwa kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo Febuari 18,2021.

F87A0144-2.jpg


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Wananchi mbalimbali wa Zanzibar katika Viwanja vya Mnazi mmoja baada ya kumalizika kwa Sala Maalum ya Kusalia Mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad iliyosaliwa kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo Febuari 18,2021.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

F87A0068-2.jpg
F87A0074-2.jpg
F87A0081-2.jpg

DSC0202-scaled.jpg


MAKANALI na Mameja wa JWTZ wakiwa wamebeka jeneza la Mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad uliopowasiliu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kwa ajili ya kuagwa na Wananchi wa Zanzibar katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
DSC0218-scaled.jpg


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi na Viongozi wengi wakijumuika na Wananchi wa Zanzibar katika Sala ya kuusalia mwili wa marehemu aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ilioongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, iliofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Zanzibar leo 18-2-2021.(Picha na Ikulu)
DSC0245-scaled.jpg


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi na Viongozi wa Dini na Serikali wakiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Abdalla Talib, baada ya kumalizika kwa Sala ya kuusalia mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, iliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
DSC0251-scaled.jpg
WANANCHI wa Zanzibar wakiitikia dua
DSC0283-scaled.jpg
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwasilia Viongozi na kuwaaga baada ya kumalizika kwa Sala ya kumuimbea aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, iliofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 
... sijui Maalimu atazikwa wapi mzee wa watu. Dar au Pemba? Hivi vifo vingeepukwa kama hatua za kujikinga zingechukuliwa seriously! Apumzike kwa amani.
 
kwa hakika msiba ni mzito sana sana.

Jabali limeanguka, Wazanzibari na Watanzania tunajiuliza twenda api sasa?

ila kwenye dhiki huja faraja.

huenda kupitia tukio hili siasa zetu zitabadilika, utendaji wetu na mahusiano yetu yatabadilika.

kifo ni sehemu kuu ya mabadiliko katika dunia.

tufute machozi tusimame tukijitafakari na kujipanga upya.
 
إِنَّا لِلَّٰهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ‎
 
kwa hakika msiba ni mzito sana sana.

Jabali limeanguka, Wazanzibari na Watanzania tunajiuliza twenda api sasa?..
Siasa za Zanzibar ilikuwa ni Maalim Seif Sharif Hamad na Seif Sharif Hamad ndie alikuwa siasa za Zanzibar.

Maalim Seif, umepigana vita vilivyo vizuri, mwendo umeumaliza.

Vizazi na vizazi vitakukumbuka Maalim Seif kwasababu umeacha alama isiyofutika kwenye siasa za Taifa hili

Nenda kapumzike Maalim Seif!!!!!
 
Back
Top Bottom