Yaliyojiri msiba wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif

Yaliyojiri msiba wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif

Najaribu kuangalia maazishi ya makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar Ndg Maalim Seif nimegundua jambo moja. Kwakweli ndugu zetu waislam taratibu zao za maziko ni za hovyo kabisa. Hakuna kiongozi mkuu anayeongoza shughuli nzima, watu wametawanyika hovyo hovyo, haijulikani nani anayeongoza shughuli hata nyimbo wanazoimba ni mtu yeyote tu anajianzishia hovyohovyo kwa kifupi ni kama vile sio maazishi ya kiongozi wa kitaifa.

Kwakweli waislamu hawana utaratibu mzuri wa maziko ya viongozi wa kitaifa. Hata kama mtu amekwishafariki lakini ni wazi kwamba kwakuwa ni kiongozi wa kitaifa lazima ugeni utakuwa mkubwa na utaratibu wa kuongoza shughuli lazima uwepo na swala la muda wa maandalizi sidhani kama ni kigezo tosha kwani hii dini ni kubwa na ipo tokea zamani ilipaswa iwe organized kwa matukio kama haya.Yote kwa yote, Pumzika kwa amani Seif Sharif Hamad,Tanzania itakukumbuka daima.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Ha ha ha ha mkuu unazingua mambo siyo ya kuchekesha ila umefanya nicheke sana. Huo ndiyo utaratibu wao mkuu tuuheshimu
 
Najaribu kuangalia maazishi ya makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar Ndg Maalim Seif nimegundua jambo moja.Kwakweli ndugu zetu waislam taratibu zao za maziko ni za hovyo kabisa...
Wana utaratibu wao
JamiiForums1493745761.jpg
 
Attachments

  • JamiiForums1493745761.jpg
    JamiiForums1493745761.jpg
    61 KB · Views: 2
Hawapo HARUSINI HAPO.
nimeandika nikafuta
nimeandika tena nikafuta.

any way ngoja nikustahi kwa vile nina majonzi ya mwislam mwenzetu.

nikuambie tu: uislam hauwezi kufuata mila na desturi za wakristo na wana swala ( wagalatia )katika mazishi.

lakini pia uwe tajiri ama maskini utazikwa ndani ya mwana ndani.
 
Hakika,chanel ten,ni kituo cha utangazaji kisicho na mfano,jinsi walivyotuletea matangazo ya moja kwa moja,ya Maziko ya Makamo wa Kwanza wa Rais,wa Zanzibar,Marehemu Seif Sharif Hamad.Mtangazaji wa Studio,anatupa habari,za kueleweka na zilivyo nzuri,na zilizopangika,zimetufanya watazamaji,tusiondoke hata dakika moja.
Mbona unampalilia sana badala ya kuelezea yaliyojiri
 
Najaribu kuangalia maazishi ya makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar Ndg Maalim Seif nimegundua jambo moja.Kwakweli ndugu zetu waislam taratibu zao za maziko ni za hovyo kabisa...
Basi haya tuachie tu na utaratibu zetu za hovyo.

Sie tunachojali ni kumstiri Marehem na kumuombea dua na maghfira ili safari yake iwe nyepesi.

Allah Ampokee hali ya kuwa yupo radhi nae, Amiepushie mchanga mzito na Amjalie Malaika wema ndio wawe wamempokea. Laasir hii ya Alkhamis kuingia Jumua'a
 
Najaribu kuangalia maazishi ya makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar Ndg Maalim Seif nimegundua jambo moja.Kwakweli ndugu zetu waislam taratibu zao za maziko ni za hovyo kabisa....
Uandishi wako ni wa hovyi sana.

Huna vituo wala paragraph!
 
Najaribu kuangalia maazishi ya makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar Ndg Maalim Seif nimegundua jambo moja.Kwakweli ndugu zetu waislam taratibu zao za maziko ni za hovyo kabisa...
Jaribu kuheshimu taratibu za dini za wenzio hata kama unaichukia dini hiyo. Usioneshe chuki za wazi, kwani unapoonesha chuki za wazi basi tambua hata wenzako nao wataonesha chuki za wazi dhidi ya dini yako, kitendo ambacho utashindwa kukivumilia na kitakachofuata ni mvurugano. Tuishi humo.
 
Najaribu kuangalia maazishi ya makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar Ndg Maalim Seif nimegundua jambo moja.Kwakweli ndugu zetu waislam taratibu zao za maziko ni za hovyo kabisa...
Toka nimejiunga jf leo ndio nimekutana na comment ya hovyo hovyo
 
Back
Top Bottom