Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Tabora: Tundu Lissu (CHADEMA), azindua Kampeni Kanda ya Magharibi katika viwanja vya Chipukizi

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Tabora: Tundu Lissu (CHADEMA), azindua Kampeni Kanda ya Magharibi katika viwanja vya Chipukizi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426

Kwa Mujibu wa ratiba ya kampeni iliyotolewa na Chadema inaonyesha kwamba Mh Tundu Lissu leo atakuwa Tabora

=====

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
CHADEMA TUNDU LISSU leo Septemba 3, 2020, atazindua kampeni kwa Kanda ya Magharibi, uzinduzi ambao utafanyika katika viwanja vya Chipukizi mkoani Tabora.
1599144323062.png

1599144405754.png

Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu, aliyeambatana na Mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais, Mhe. Salum Mwalim Juma Mwalim, ukiingia na kupokelewa katika Uwanja wa Chipukizi, mjini Tabora baada ya kufika mkoani humo akitokea Mkoa wa Shinyanga.
1599144276261.png

1599144524760.png

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu akiwasalimia maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Tabora waliofika kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea huyo kwa Kanda ya Magharibi (Kigoma, Tabora na Katavi) uliofanyika katika Uwanja wa Chipukizi, mjini Tabora leo Alhamis, Septemba 3, 2020.
1599144363880.png
1599144378748.png
1599144438822.png
1599144491342.png

Umati wa maelfu ya wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu, kwenye Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chadema, Kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma na Katavi) uliofanyika leo Alhamis, Septemba 3, 2020, katika Uwanja wa Chipukizi, mjini Tabora.
 
Kwa Mujibu wa ratiba ya kampeni iliyotolewa na Chadema inaonyesha kwamba Mh Tundu Lissu leo atakuwa Tabora

View attachment 1557221
Mradi wa maji toka ziwa victoria umeshammaliza. Ccm wanazoa kura zote Tabora. Maana huu mradi umewapa credit kubwa sana ya kisiasa Ccm. Akina mama wa kinyamwezi hawawezi kumsikiliza mtu anaesema kuletewa maji tabora ni maendeleo ya vitu.
 
Lissu Baba tukomboe katika hii vita ya kuminywa haki za binadamu. Ethiopia na madege yao Kama yote Pamoja na fly-overs lakini wanakimbia nchi kwenda kuwa manamba South Africa kwa uminywaji wa haki za binadamu nchini kwao.

Lissu tuvushe baba tuvuahe.
 
Usilinganishe Ethiopia na Tanzania. Njoo kahama watu wanakula mchele na kusaza ndio ulinganishe na nchi ambayo ina ukame miaka 40.
Haki za binadamiu zipi zinazominywa? Watu wanashinda kwenye vijiwe vya kahawa mpaka saa nne usiku wanajadili siasa.
 
Kila la heri Rais wa awamu ya sita Mhe Tundu Antipas Lissu....kama ambavyo hawaamini risasi 16 haijakuzima, vivyo hivyo hakuna wakukuzima October 28 kuingia Ikulu
Kila chama kiliambiwa kipeleke ratiba
Ndio walipeleka then NEC ilitumia hizo ratiba zao kuwapangia ratiba resmi ili kusitokee mgongano wa mikutano siku na sehemu kuwa moja
 
Usilinganishe Ethiopia na Tanzania. Njoo kahama watu wanakula mchele na kusaza ndio ulinganishe na nchi ambayo ina ukame miaka 40.
Haki za binadamiu zipi zinazominywa? Watu wanashinda kwenye vijiwe vya kahawa mpaka saa nne usiku.
Lema alikaa ndani kwa kuota ndoto
Sugu alifungwa bila hatia ni kwa amri kutoka juu.
Tundu Lissu alipokwa ubunge akiwa mgonjwa. Ni mengi sana.
 
Back
Top Bottom