Huk Luk
JF-Expert Member
- May 5, 2022
- 1,291
- 15,947
Hii issue naifatilia huku nacheka sana.Ni 50% plus 1 vote.
Hapo ni kama mswahili umwambie atamke 11,000 na 10,001. Akitumia kiswahili cha "hovyo" kile cha "Elfu kumi na moja" huezi note tofauti ya hizo figure 2 hadi pale atakapozitamka kama "Kumi na Moja elfu kwa 11,000" kisha "Kumi elfu na Moja kwa 10,001" respectively.
Same na hii 50% + 1.
Walio sahihi ni kama wewe apo uliesema 50% ya kura zote jumlisha na kura 1 ya halali. Of course hapo inakuwa tayari ni zaidi ya nusu ya kura zote.
Hawa wengine wanaenda chaka kwa kuita 51% ya kura zote.
Yatupasa tujue (50+1)% na (50% + 1) ni vitu viwili tofauti kabisa. Tusiwe kama Magazijuto za primary zimetupiga knock out ukubwani. Lau ingekua ni 51% asilimia kusingekua na maana ya kuweka hii symbol ya % kabla ya alama ya +.
Mfano mwingine kama alio utoa CARDLESS
Kwamba zipo jumla ya kura 1000, Mshindi anatakiwa apate 50%+1 maana ake anatakiwa apate kura walau 501. Wala sio 510 ambazo ni 51% kama inavyotafsiriwa na baadhi ya watu hapa walio shindwa kuelewa maandishi.
Hapo kwenye mfano juu, hiyo 501 ya 1,000 ni 50.08% na the rest ni 49.92%. Ingekuwa ndio matokeo basi hapo ndipo mshindi angetangazwa.
Na kwa Ruto na mwenzie Raila, kama kura zingekua "exactly" Mil 14 (I mean Mil 14 net), basi mshindi anapaswa awe na kura 7,000,000+1 ili atangazwe mshindi.