Yaliyojiri Uwanja wa Aman: Simba SC Vs Yanga,Kombe la Mapinduzi 10/1/2017

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Leo ni nusu fainali iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa katika Kombe la Mapinduzi ambayo inawakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba.
Mechi inachezwa saa mbili usiku kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Kimuhemuhe ni kikubwa sana kwa mashabiki wa Simba kutokana na rekodi ya timu yao.Mashabiki wengi wa Simba wamepanda boti kuelekea Zenji kwa ajiri ya kuipa nguvu timu yao. Kwa upande wa Yanga mashabiki wamebaki kulaumiana kutokana na kumbukumbu mbaya ya Kipigo cha "Mama mkanye Mwanao" ilichopokea vizuri kwa roho safi toka Azam FC

Mtangazaji wenu nitawaletea moja kwa moja matumikio muhimu kabla,wakati wa mechi na baada ya mtanange

Usiondoke

Updates
Yanga imepokea kipigo cha penati 4 kwa 2.
Ball Possession Simba 54% -Yanga 46%

Sasa Mnyama Mkali Simba anatinga fainali na Azam FC
 
Tutasubiri mpambano huu, tunaingiza timu tukiwa na majeruhi wengi lakini Simba msitegemee ushindi.
 
Kuna hatari ya mtu kupigwa 6 Leo

Naogopa sana

Ngoja tusubiri
 
Umeleta Uzi Bila Taarifa Kamilifu, Mechi Saa Ngp? Refa Ni Nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…