Yaliyojiri Uwanja wa Taifa: Taifa Stars 2 - 1 Equatorial Guinea

Yaliyojiri Uwanja wa Taifa: Taifa Stars 2 - 1 Equatorial Guinea

Timu ya taifa ya Tanzania imeanza vyema kutupa karata yake ya kufuzu michuano ya AFCON 2021 kwa kuifunga timu ya Equatorial Guinea kwa bao 2-1.

Katika mchezo huo, Equqtorial Guinea ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 15 ya mchezo kupitia kwa mchezaji Pedro Obieng, wakati Stars walipata magoli yao kipindi cha pili ambapo dakika ya 68 nyota Simon Msuva aliipatika Tanzania goli la kusawazisha kabla ya Salum Abubakari "Sure Boy" kufunga goli la ushindi kunako dakika ya 90.

Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa Stars 2 na Equatorial Guinea 1. katika mchezo unaofuata Stars atakutana na timu ya Taifa ya Libya.

1573844667815.png
 
Sema hili la pili tumewabaka maana ilitakiwa tucheze fair play baada ya mchezaji wao kuumia na kipa kuutoa mpira nje. Ila mwisho wa siku fair play siyo lazima.

Kongole stars.
 
Tungefungwa mngesikia kocha mbovu vililive sipati picha watu wangemlaumu Kaseja.Yote kwa yote pongezi kwa Taifa stars na benchi zima la ufundi
 
Haikua mechi rahisi. Hawa jamaa kama waarabu, wamepoteza sana muda. Refa naye filimbi muda wote. Hivi vitu viwili vilikua vinawavuruga sana wachezaji wetu. Kila wakijaribu kupanga mipango filimbi mara mtu kalala chini. Kongole kwa Stars japo kocha inabidi awakumbushe kuimaliza mechi mapema leo nusura tuumbuke
 
November 15, 2019

Tanzania 2 : 1 Equatorial Guinea

Dakika 90' + 4 za nyongeza = 95' Full time mpira umekwisha hapa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Magoli ya Tanzania Simon Msuva 68' na Abubakar Salum 93' huku Equatorial Guinea likifungwa na Obiang'.


Hali ilivyokuwa kwa dakika:
Dakika 68'
Goal ! Simon Happygod Msuva awanyanyua vitini waTanzania kwa goal safi kabisa uwanja wa Taifa Dsm



Goal ! Abubakar Salum dakika ya 93' shuti lake kali yaipatia Tanzania pointi zote tatu.

Tanzania 2 : 1 Equatorial Guinea
Super Coach wa Tanzania Etienne Ndirangiye na wa Equatorial Guinea walambishwa kadi za njano dakika ya 95' ktk mchezo huu kuelekea fainali huko Cameroon 2021.
 
Kocha awe anamuanzisha huyu Nchimbi kama namba 9, then Samata awe 10 maana anajitahidi kuleta pressure kwa mabeki kwa wapinzani
 
Tungefungwa mngesikia kocha mbovu vililive sipati picha watu wangemlaumu Kaseja.Yote kwa yote pongezi kwa Taifa stars na benchi zima la ufundi

Hata kama tumeshinda lakini Kaseja hawezi kukwepa lawama kwa aina ya goli alilofungwa. Wenzake wa hadhi yake, mpira kama ule huucheza.
 
Huyu Nchimbi ni wa kuanza first eleven kama namba 9 , Samatta awe namba 10.....Msuva winga ya kulia, hapo tutakuwa na striking nzuri
 
Hizi ni juhudi serikali ya awamu ya tano. Pia hongera kwa Humphrey Polepole kwa shuti lililozaa bao la ushindi. Hapa kazi tu.
Mkuu usiifananishe taifa star's na mambo ya hovyo hovyo!!
 
Nasapoti hivyo, me nilijua nchimbi asipofunga, basi atatoa asist coz jamaa anajua kujiweka kwenye njia za mpira.
Kocha awe anamuanzisha huyu Nchimbi kama namba 9, then Samata awe 10 maana anajitahidi kuleta pressure kwa mabeki kwa wapinzani
 
Huyu Nchimbi ni wa kuanza first eleven kama namba 9 , Samatta awe namba 10.....Msuva winga ya kulia, hapo tutakuwa na striking nzuri
Au samata aanzie benchi kabsa [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom