Baada tu ya kumaliza kuona demo ya Makomandoo iliyoisha hivi punde nimeamua rasmi kuachana rasmi na Demu wangu mmoja ambaye Bwana wake nae ni Komando. Bado nayapenda sana maisha halafu sioni sababu ya Mimi kuteseka wakati muhusika mwenyewe tu kaweza kuivumilia misumari kama 200 imchome mgongoni mwake huku wenzake wakimtimba na kumkanyaga na Jamaa kaamka akiwa yupo fiti tu. Sasa sijui akinifumania nae Demu wake atanifanyeje! Mpenzi wangu nakupenda sana ila Mumeo Komandoo huyo anapendwa zaidi na misumari na yale matofali hivyo isiwe taabu / shida tuachane tu tafadhali.