Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Kha, sijui kwa nini siko moved na haya mambo. Najitahidi kuipenda hii nchi nsshindwa kabisa! Siko impressed hata kidogo na yoote yanayofanyika hapo! Kha!
 
In Tanzania pekee comando ana kitambi na bado anasifiwa (obesity ni malnutrition )
Basi bwana yakaletwa matofali yavunjiwe kichwani na kifuani, nyundo moja tuu kuleee! Kilichonifurahisha si tofali kuvunjika bali tofali kugeuka kama mchanga au unga. Wanaojua ujenzi wamenielewa hapo.
Tofali la kweli ukilipiga nyundo linavunjika sio kupukutika. Abrakadabra ya wazi hiyo, tusifanye komedi mpaka jeshini.
 
Baada tu ya kumaliza kuona demo ya Makomandoo iliyoisha hivi punde nimeamua rasmi kuachana rasmi na Demu wangu mmoja ambaye Bwana wake nae ni Komando. Bado nayapenda sana maisha halafu sioni sababu ya Mimi kuteseka wakati muhusika mwenyewe tu kaweza kuivumilia misumari kama 200 imchome mgongoni mwake huku wenzake wakimtimba na kumkanyaga na Jamaa kaamka akiwa yupo fiti tu. Sasa sijui akinifumania nae Demu wake atanifanyeje! Mpenzi wangu nakupenda sana ila Mumeo Komandoo huyo anapendwa zaidi na misumari na yale matofali hivyo isiwe taabu / shida tuachane tu tafadhali.
 
Achana na wale wa kutumia silaha lakini Komando walioonyesha sarakasi wamedhalilisha kabisa tasnia hiyo. Kilichoonyeshwa kama mbinu za kupigana au karate za makomando ni mambo ya mitaani na mtu yeyote anaweza kufanya huku mitaani wako wengi tu wanafanya hayo. Niko disappointed kwa sababu tulitegemea watu walioko kambini kulinda nchi wanashindwa ku exceed mbinu za waonyesha sarakasi wa mitaani na walioko kwenye madojo. Nashauri makomandoo wawatafute wachina au wajapani wawape training ambayo ina viwango na siyo kufanya uhuni mbele ya dunia. Rais asiruhusu hawa jamaa kuonyesha ujinga kama hawajajipanga kwani ina expose udhaifu wa jeshi letu kwa maadui. Kilichoonyeshwa mbele ya dunia kinaonyesha hatuko serious. Kenya wana maonyesho kama haya lakini ukiangalia una hold your beath kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Kwa mtazamo wangu kama hiki ndicho walichojiandaa nacho kuonyesha watanzania basi hii group inatakiwa iwe overhauled ili kurejesha heshima ya makomando na kuwapa watanzania matumaini kwa jeshi lao
 
Back
Top Bottom