Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Hazikuwa na shamra shamra kama tulivyozoea, nyuso za waliohudhuria zilikuwa hazionyeshi bashasha yeyote hadi mshereheshaji akawa anawakumbusha kumpungia mkono rais.

Wananchi walikuwa wamenuna, viongozi walikuwa wamenuna hata wageni waalikwa nao walikuwa wamenuna.

Nafikiri rais aliliona hili hadi kupelekea kuzihamishia Dodoma kutoka kwenye uwanja wa Uhuru zilipozinduliwa 9 Dec 1961.
 
Naomba kukuuliza hivi Mkuu wa Mkoa Paul Makonda siku hizi na yeye amekuwa Mtu wa Itifaki? Kwani namwona anafanya Kazi za Watu wa Protocol na kimsingi yeye anatakiwa tu kumpokea mgeni, kupeana nae mkono kisha kuwaachia Watu wa ( Kazi Maalum / Itifaki ) kuendelea na majukumu yao waliyosomea na kubobea nayo lakini cha kusikitisha yeye huyo huyo RC Makonda anaenda kumpokea Mgeni kisha yeye huyo huyo tena anawasindikiza karibu na kupanda ngazi tena huku akitoa maelekezo. Huyu Mkuu wenu wa Mkoa aache kuwa na sifa na kimbelembele na nina uhakika hata Watu wa Itifaki alionao pale anawakwaza. Kwanini hajifunzi na habadiliki?
Hapo humtendei haki, labda hukuwa mfuatiliaji wa sherehe zilizopita kwa wakuu wa mikoa walio mtangulia, uzoefu wa ufuatiliaji wangu ni kuwa sherehe zote za kitaifa zinapo fanyika ktk mkoa, ambazo zitahudhuriwa na wakuu wa nchi hapo mkuu wa mkoa huwa ndio mwenyeji wa sherehe hizo, hivyo basi ndio mkuu wa itifaki na huwa anawajibika kupokea wageni, niliyaona hayo tokea enzi za uongozi wa mzee makamba na wengineo. Nawasilisha
 
Hongereni sana kwa kutimiza miaka 55 ya uhuru nchi isiyokuwa na umeme na wala maji safi. Uhuru usiokuwa na maana yoyote ile.


MUTAISOMA NAMBA.jpg
 
Licha ya Changamoto zetu kama Taifa,na Mafanikio yanayotajwa Lazima Kuulinda na Kuuenzi Uhuru Wetu Pia Kuakisi Tunu zake [HASHTAG]#55UHURUTanzania[/HASHTAG]
 
Kweli kuhamia Dodoma ni bad newz kwa wakaz weng wa DSM.
Ila hakuna namna
 
Back
Top Bottom