Yaliyojiri VPL: Simba SC vs Yanga SC - 20 October 2013

Status
Not open for further replies.
Yanga wametia aibu jamani, yaani Mnyama kachomoa magoli yote 3! Haijawahi tokea namna hii. Ama kweli Yanga ni dhaifu! Hata hivyo nawapa hongera watani wa jadi, raha ya mpira magoli.

Kinachonisikitisha ni hawa watoto wa Simba kuwadindia watu wazima kinatisha, raundi ya pili watakuwa wameshapevuka na huenda Yanga wakalizwa.
 
Masuke.............Unashangilia sare??????????

I see.....
 
Wachezaji wa yanga wamekimbia,hawataki kabisa kuzungumza na media!du aibu sana.kiufupi simba ndo wameshinda hii mechi.

we endelea kujipa moyo...nadhani umesahau kuwa ndio mshatolewa kileleni hivyo...
 
Nadhani wewe umeanza kushabikia juzi.....Una habari Yanga wamewahi kuchomoa mechi na Simba Sheikh Amri Abeid Arusha matokeo yakawa 4-4......

Simba bana, badala ya kujiuliza ni kwa nini mliruhusu ba0 3-0 1st Half mnaanza kuiponda Yanga kwa kuruhusu magoli matatu......Ulitaka Yanga ishinde???/
 
Wapi huko walizima?

Simba madume wewe....hata kama hujapenda ukweli ndo upo hivyo...ila pole saana
Eti simba madume,mngepigwa tatu dk 45 za mwanzo?kwa hiyo mmefurahia sare,uanaume wenu upo wapi?
 
Sikuwa na hofu na niliamini tumepigwa matatu lakini sikuamini tulipowapiga matatu. Horengera sana kesho sijui ningesemaje ofcn!
 
Wachezaji wa yanga wamekimbia,hawataki kabisa kuzungumza na media!du aibu sana.kiufupi simba ndo wameshinda hii mechi.


Frankly speaking nchi itaendelea kudumaa na haitokaa ipate mafanikio katika soka, inasikitisha sana mtu mzima kuwa kama zuzu kushangili droo badala ya kulika kitimoto benchi la ufundi ni kwa nini timu iruhusu kufungwa goli 3 kwa dakika 45? Hii ni kwa timu zote mbili.
 
Masuke.............Unashangilia sare??????????

I see.....

Mkuu Balantanda kwa haya matokeo ni kama tumeshinda vile, Ruvu shooting walitufunga goli moja na tulitoka jasho kusawazisha goli moja tu leo tumesawazisha goli tatu tena ya ukuta unaominiwa kuwa ni imara kabisa kwa nini tusifurahi, hata kama Simba tungekuwa tumeanza kuongoza na nyie mkasawazisha ningeona kama vile tumefungwa tu. Kuna post moja niliuliza naweza kuwapongeza kabla ya dakika 90, hakuna aliyenijibu sijui mlijua hamtashinda hii mechi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…