Yaliyojiri VPL: Simba SC vs Yanga SC - 20 October 2013

Yaliyojiri VPL: Simba SC vs Yanga SC - 20 October 2013

Status
Not open for further replies.
attachment.php
 
Katika siku ambazo nilikuwa na tension ya mpira ni jana. Maana nilianza kupata sms za kubezwa kuanzia saa 12 ahsubuh, yaami ilikuwa taabu sana.

Muda wa mechi sikuwa na raha yalemaneno niliyobezwa yalikuwa yanaring in my brain na mapicha ya kumdhalilisha mnyama yaani hata mlo wa mchana sikula.

Niliamua kutouangalia neikaenda zangu vikobaaa....niko njiani nasikia goooo...ikabidi nisogee tumefuungwa, niko kwenye kikao nasika tena gooo tumefungwa, nikachungulia JF na kisimu changu laaaa nikakuta wakina Heaven on earth, na webzake ndo wanashindilia mwiba moyoni nika log out fastaa. Nimeamini nina mapenzi makubwa na SIMBA

Naanza safari ya kurudi home shosti ananipigia simu eti cha tatu hicho kaoge....yaani nusu nimtukane. Mwingine tena haloow leo lazima uumwe..nikamwambia mmpira ni 90min, akasema mmeshapigwa v3 unaongea dkk 90.

Njiani tena nikakutana na mwenye kiredio chake ile napishana nae tuu nasikia gooo, yaani nilihisi mapigo ya moyo yana potea..nasikilizia la nne au? Aaa kumbe MNYAMA ameanza kuchomoa, baada ya muda tena nasikia gooo chapili. Nakaribia home nasikia tena gooo afu watoto wananilaki mama mama simba wamesawazisha matatu mama timu yako. Kajasho kembaba kalinitoka kafuraha lakini na kushushia punzi maana.

Nimetumia almost masaa mawili kufuatilia thread, kwa nionavyo yaani kweli kipindi cha kwanza SIMBA tulikuwa na simanzi sana. Nina furaha ya ajabu si kwa sbb ya droo but kwa simba kucheza mchezo wa maana na kuweza kurudisha mabao ma 3 kwa staili ya aina yake.

Kwa upande mwingine nijambo lisilofichika kuwa pamoja na droo YANGA wameaibika.....POLENI

Salamu kwa wazalendo wa ukweli wa SSC Ndeticha, @Exellent Katavi, Asprin, Masuke, Filipo, KakaKiiza, Mzee wa Rula, stevoh na all SIMBA SPORTS CLUB Fans...pamoja sana.

Yanga SIMBA mtaipenda tu.... Balantanda nimekukubali sana..thumb up for you mkuu

Hivi sasa ni saa 01:54 tukutane baadayeee....kwa heri kwa sasa.

Pamoja mkuuu
 
Last edited by a moderator:
Sizinga uliona eeeeh! Mi baada ya kipindi cha kwanza nilisepa kimya kimya kwenda kulala nikafikiri hapa leo bila kupigwa 6 kazi,jamaa angu alinipigia nakunieleza eti kaka njoo ucheck game imebadilika simba inatawala kwa mbwembwe zote sikuamini mikamuuliza matokeo vp? Akanijibu kuwa yanga 3 na simba 2 kaka sikuamini ilinibidi nichukue usafiri wangu na kurejea camp na kutizama match hadi mwisho,duh kweli Mungu ni mwema
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom